Uchaguzi 2020 Zitto: Ilani ya ACT Wazalendo na utekelezaji wake

Uchaguzi 2020 Zitto: Ilani ya ACT Wazalendo na utekelezaji wake

Katika hili wamezengua sana hawa jamaa. Wote ACT na CHADEMA.

Kiufupi ni wamefanya tathmini na nahisi wamejiridhisha kwamba hawawezi kumuondoa Mheshimiwa rais Magufuli madarakani, hivyo wanachokifanya ni kujaribu tu kuwa chama kuku cha upinzani. Yaani CDM na ACT wote wanagombania nafasi ya pili.

Kadi yangu ya CCM sijailipia mwaka wa kumi sasa ila kwa upumbavu huu naenda kuilipia soon.

Wangari Maathai
Usitufokee
 
Kimsingi Zitto kaongea ya maana
Naona ana copy sana REA ambayo nayo ilikuwa idea yake

But what if mikopo isipopatikana?

Kukopa trillion 10 sio shughuli ndogo..

Ina maana miradi ya maji ndo itakufa?
 
Katika hili wamezengua sana hawa jamaa. Wote ACT na CHADEMA.

Kiufupi ni wamefanya tathmini na nahisi wamejiridhisha kwamba hawawezi kumuondoa Mheshimiwa rais Magufuli madarakani, hivyo wanachokifanya ni kujaribu tu kuwa chama kuku cha upinzani. Yaani CDM na ACT wote wanagombania nafasi ya pili.

Kadi yangu ya CCM sijailipia mwaka wa kumi sasa ila kwa upumbavu huu naenda kuilipia soon.

Wangari Maathai
Zito ni ccm b mkuu..ana ajenda zake
Ukweli hatupo serious ...!yaani niliwaza had nahis kuumwa
 
Kimsingi Zitto kaongea ya maana
Naona ana copy sana REA ambayo nayo ilikuwa idea yake

But what if mikopo isipopatikana?

Kukopa trillion 10 sio shughuli ndogo..

Ina maana miradi ya maji ndo itakufa?
Walau kaonesha na fedha zitapatikana wapi, hio ni trilioni 2 kwa mwaka. Bajeti ya sasa zaidi ya trilioni 2 ni mikopo. Nyingine zimejengea stigla na ununuzi wa ndege.

Walau wanaonesha tunakopa kwa miradi ipi, hayo madeni tutalipa sie wananchi.


Chama tawala nao watuambie fedha zitatoka wapi kwenye miradi yao ya kimkakati na sio kutustukiza na mikopo
 
Hapo kwenye kufuta madeni ya Elim ya juu naona ni kutaka kufurahisha voters tu..
Hii nchi bila massive taxation maendeleo mtaendelea kuyaongea tu..
Wale ambao wameshalipa utawa refund?
 
Una hoja ila utekelezaji kwa kodi zipi mkuu?

Maamuzi mengi makubwa ya kisera/sheria yanafanywa na serikali iliyo madarakani. Madiwani na Halmashauri zinaishia kutunga sheria ndogo zisizo na mashiko.

Tungekuwa na mfumo wa majimbo labda
Sio kweli masmuzi ya halmashauri hufanywa na baraza la madiwani na meya wao .Ujiji iko chini ya ACT wazalendo walitakiwa waeleze walichoweka kwenye Ilani iliyopita walikitekelezaje kwenye halmashauri Yao ambako wao ndio waamuzi
 
Hapo kwenye kufuta madeni ya Elim ya juu naona ni kutaka kufurahisha voters tu..
Hii nchi bila massive taxation maendeleo mtaendelea kuyaongea tu..
Wale ambao wameshalipa utawa refund?
Shida sionkufuta madeni mkopaji anahitaji vyanzo vya mapato kuyalipa wangejikita. Hapo zaidi sababu ukifuta Deni tu Hana ajira Hana he'll impact Ni zero!!! Ufute usifute status yake haibadiliki
 
Kila la kheri katika hili. ....Muhimu kama upinzani msigawane kura among yourselves fanyeni namna mufikie muafaka.
 
Sio kweli masmuzi ya halmashauri hufanywa na baraza la madiwani na meya wao .Ujiji iko chini ya ACT wazalendo walitakiwa waeleze walichoweka kwenye Ilani iliyopita walikitekelezaje kwenye halmashauri Yao ambako wao ndio waamuzi
Kodi na mikopo wanapitisha pia baraza la madiwani?

Mapendekezo yao ni ya nchi nzima, kuhusu utekelezaji wa Ujiji ni suala lingine.
 
Ndugu yangu na kaka yangu Zitto Kabwe
Ilani yenu ni nzuri na naamni kabisa inaakisi mahitaji ya Wananchi wengi kwa sasa.Natamani nipate nakala kamili ya ilani yenu kabla sijaweka uchambuzi wangu kamili hapa ilakwa sababu umeweka kitu kidgo basi naweza kutoa maoni kwa kuzingatia hiki kidgo ulichoweka.
Mikopo ya ELimu ya Juu
Ilani yenu imezungumzi kutoa elimu ya Juu bure swali ni kwa nini muitoe bure?kwa sababu tuna uwezo wa kulipa,sababu wananchi hawawezi kulipa au ni sababu gani?Dhana ya maendeleo lazima iwe shirikishi kutoa ahadi ya kutoa elimu bure nafikir ni wazo zuri ila wakati wake bado.Binafsi nafikiri zaidi kwamba kwa rasilimali tulizo nazo lazima tupange na tuchague kwa umakini.Sikubaliana na hoja ya kufuta madeni ya nyuma ya mkopo ingawa najua yanaweza kuvutia kisiasa.Katika eneo hilo la Mikopo mnaweza kuweka utaratibu kwa wale wahitimu ambao kweli hawana uwezo wa kulipia au wana kipato kidogo sana Mfano Mhitimu wa Chuo kikuu atalipa mkopo wake pale tu anapokuwa na PATO la TZS Milion 1.5 and above ila chini ya hapo hatalazimika kulipa ingawa anaweza kuamua kuchangua kwa kiwango ambacho hakitakuwa katika asilimia kwa hiyari yake.

Deni lake halitafutwa,litaendelea kuwepo active kwa kipindi cha miaka 15.Na iwapo mhitimu huyu ambaye hajalipa deni atakuwa na mtoto wake ambaye anahitaji mkopo basi credit rating ya baba yake itaathiri kiwango cha mkopo atakachopewa mwanae kwa kuzingatia uwezo wa mzazi kwa wakti huo na performance ya mtoto.Hu ni mtazamo na uhauri wangu kwenye swala hili.
Jambo la muhimu zaidi ni kuongeza financing katika mfumo wa elimu za ufundi stadi ni ikiwezekana mikopo itolewe katika ngazi hii ya elimu kwani tukiwa na mafundi stadi wenye ujuzi wanaweza kuzalisha ajira na bidhaa kuliko wahitimu ambao wengi wanahitaji white collar jobs ambazo ni very limited.

BIMA YA AFYA NA HIFADHI YA JAMII
Kwenye swala la Bima ya afya naona una nia nzuri ila hapo napendekeza zaidi uangalie kuhusu ukweli kwamba swala BIMA ya AFYA ni swala la kiutamaduni zaidi kuliko swala fedha.Kuunganisha bima ya afya na other aspect za social security ni hatari hasa ukizingatia kwamba zote hizo ni very sensitive and resource demanding sectors.

Binafsi naamini kwamba suala la Universal Health coverage linahitaji kuwezesha mtu mtu kupata BIMA kwa bei nafuu.Kwa mfano,Katika Mfumo wa TAX assessment katika Biashara uwekwe utaratibu kwamba Ukishapewa TIN number na kulipa kodi unakuwa entitle kupewa BIMA ya afya at percent ya TAX estimates zako kwa kuzingatia mapato yako.Mfano Kama mtu amekadiria kwamba kodi yake kwa mwaka ni TZS 500,000 basi atachangia kiasi sawa na mafanyakazi anayelipwa mshahara wa kiwango hicho with discount kidogo.na pia atachangia kwenye social security kiwango kidogo.Lengo ni kutengeneza MFumo wa BIMA ya AFYA na HIFADHI YA JAMII AMBAO ni inclusive.

SWALA LA MAJI SAFI NA SALAMA
Katika Swala hili PPP ndio solution,Serikali itoe incentive kwa watu binafsi kuwekeza katika kuchimba na kusambaza maji katika maeneo mbalimbali.Watu Binafis wataweka mitaji yao humo huku wakijua watapata mapato.Halihitaji Rocket Sayansi hili linahitaji NIA thabiti tu na ujasiri na uzalendo.Tukifanya hivyo watu watabeba maji ya chumvi kutoka Dar na kuyapeleka DODOMA.

Hii barabara ya KOROSHO sitaki kusema chochote ila embu anza kufikiri in terms of RAILWAY TRANSPORT nafikir tunahitaji nchi nzima iunganishwe na Mtandao wa Reli.

KUHUSU MAPINDUZI YA KILIMO
Hili lina mipango mingi lakini cha muhimu zaidi katika kilimo chetu ni masoko.Mfumo mzuri wa masoko ukiwepo watu watalima maana wanayo mitaji ila tatizo ni masoko bado serikali inmeshidwa kuweka mfumo mzuri wa kuhamasisha masoko ya nje.Mfano Rahisi ni swala la Commodity Exchange Market ambayo ilianza na kubaki kuwa exclusive na bureaucratic

Iwapo ungependa zaidi niitazame ilani yenu tena na kuitolea maoni zaidi tafadhali nimekutumia Messeji PM,Sasa usije kuwa kama ile aina ya iongozi ambao wakitumiwe messeji hawarudi kwa sababu wanafikiri kwamba wao ni wakubwa zaidi,wana elewa zaidi,wana akili zaidi,wanaweza zaidi,Be humble and GOD will show you the WAY

Ubarikiwe sana

Mbunge wa Wananchi
Kimbiji Kigamboni
 
Shida sionkufuta madeni mkopaji anahitaji vyanzo vya mapato kuyalipa wangejikita. Hapo zaidi sababu ukifuta Deni tu Hana ajira Hana he'll impact Ni zero!!! Ufute usifute status yake haibadiliki
Mwisho wa siku tunatengeneza very unproductive skilled labor....
Madeni yenyewe hayafiki $5000 per individual...
Sasa unataka kutoa kila kitu bure.... nchi yetu bado ni masikini sana.. huo mzigo mwisho wa siku wanabebeshwa wachache sana.. wafanyabiashara na watumishi wachache..
Hela za NSSF hazizungumziwi kabisa... siasa hizi
 
Kabisa mtu wangu.

Yaani hatupo serious kabisa. Ndio ile ishu nkakwambia tutaongea private.
Mie sipigi Kura...ujinga tu..kila nikikumbuka la lowasa nahis napata uchizi .. upinzani wanapisema wawe kitu kimoja wanaamanisha nn...maana lisu juzi nimemskia anasema hivyo mku5wa Act
 
ZZK heshima kwako..

Leo Mh Membe amechukua form kugombea urais kama mgombea kutoka ACT.
Bila shala kesho pia TL atachukua form kugombea urais kwa tiketi ya CDM.
Kifupi upinzani kupitia vyama viwili vyenye nguvu na wafuasi mnasimamisha wagombea wawili kwa nafasi moja kwa maana you compete each other hamuoni hapa mnagawa kura za upinzania na kumpa urahisi mgombea wa CCM?..

Hamuoni hali hii ya nyie wenyewe kuwa washindani na pia kushindana na JPM mwenye kura zisizogawika nyingi mnakatisha tamaa wapenda mabadiriko na kuona haina maana tena kuendelea kussuport upinzani wenye kuangalia maslahi binafsi?

Kama upinzani mmeshindwa kukaa chini na kukibaliana hamuoni hali hii inatia shaka kwenye mustakabali mzima wa kuwapa nchi kama si watu mnaoweza kujadili, kukubaliana na kuamua?.

Nini Lengo la ACT kuilekea uchaguzi mkuu?

Je ACT mmemfanyia Mh Membe vetting ya kutosha na kujiridhisha anafaa kugombea uraisi??.

sasa ukawa walishindwa unadhan saaahv kila mtu kivyake ndo wataweza, infact ccm wamungana na vyama vingine sasa sjui wanasubiri ushindi gan
 
Back
Top Bottom