Zitto Kabwe adai nyumba yake ilichomwa moto ili kumzuia asiende kumuona Lissu hospitali Nairobi

CCM wanaoua, wanaoiba kura jee?
 
..SERIKALI iwashughulikie waliotumwa kuchoma nyumba ya Zitto Kabwe.

..Tusimlaumu Zitto kwani yeye hana vyombo na mamlaka ya kukamata wahalifu na kuwashitaki.
Kama 'wamemu-approach kumuomba radhi' awaripoti kunakohusika ili wakamatwe na kufikishwa mahakamani.
 
Kwa hali inavyoonekana Chadema watakuwa wabaya zaidi ya CCM wakipewa nchi.
Pole sana ndugu yangu,
Ni dhahiri kuwa, wewe na aina yako mmejawa na hofu ya visasi kutokana na matendo yenu kwa wa Tanzania wenye mawazo mbadala ya kuongeza kasi ya kuimarisha uhuru wa kweli, haki kwa wananchi na kuleta maendeleo ya watu wa nchi hii.
KATIBA MPYA itakuongoza na kukusaidia kuachana na ramli za kishetani. AMEN.
 


Hata Libya nao walitaka mabadiliko na wameyapata, sio kila mabadiliko ni neema mabadiliko mengine ni laana ukizingatia ni watu gani wanaopigia debe hayo mabadiliko.

Mangi apewe nchi!!?? We upo sawa kweli??!🤣
 
Hata Libya nao walitaka mabadiliko na wameyapata, sio kila mabadiliko ni neema mabadiliko mengine ni laana ukizingatia ni watu gani wanaopigia debe hayo mabadiliko.

Mangi apewe nchi!!?? We upo sawa kweli??!🤣
Ondoa hofu na hata mawazo potofu kwa wa aina yako. Katiba mpya ndio tiba kwako na Taifa zima.
 
Ondoa hofu na hata mawazo potofu kwa wa aina yako. Katiba mpya ndio tiba kwako na Taifa zima.


Katiba mpya sio dawa ya kwanza, dawa ya kwanza ni utashi wa dhati wa kisiasa (sincere political will) kwani hata kama katiba itakuwa nzuri lakini viongozi wakawa Madikteta na Corrupts kama Hitler nk, katiba inakuwa si kitu cha msaada, ningewaeleweni kama mngepambana kisiasa ndani ya katiba hii hii na mkashika dola halafu mkaandika katiba mpya hapo ningewaeleweni lakini mnapigania katiba mpya mkiwa nje ya uongozi hapo ni kwamba nia yenu ni kutumia kichaka cha katiba mpya ili mshike madaraka kirahisi na ndio maana CCM hawataki katiba mpya kwani wameshashtukia ujanja wenu wa kutaka kuwang'oa madarakani kupitia hiyo katiba mpya, na hata kama nyinyi mtaingia madarakani kupitia hii katiba mbaya na nyinyi mtakuwa wagumu zaidi ya CCM mkiambiwa katiba mpya iandikwe.

Madaraka ni matamu asikuambie mtu.

Na huo ndio mchezo wa kisiasa hususani huku kwetu Africa, mbaya zaidi Mangi ashike nchi.😀
 
Eti; "Sisi ndio tumeumizwa sana"--- hii ndio kauli ya kibinafsi ya chadema kama kwamba hakuna watu wengine walioumizwa sana na utawala wa Magu.

Acheni ubinafsi katika kutetea maslahi ya umma.

Narudia hakuna aliyeumizwa kwenye utawala wa Jiwe kama Chadema. Hayupo! Mimi nadhani wengi wameamua kujikalia kimya. Kuhusishwa na hiki chama ilikuwa ticket ya kifo au kufilisiwa au vyote. People can spin the way they want it, ila chadema walilipa gharama kubwa sana ya kuwa na mawazo tofauti na utawala wa Jiwe.

Jiwe aendelee kupumzika alipoandaliwa na muumba wake.
 


Huo ni ubaguzi wa "maumivu", hivi ukiweka idadi ya Watz nje ya CDM waliouawa (hakuna maumivu makubwa kuliko kifo) na idadi ya Wana CDM waliouawa ipi ni idadi kubwa??!, hao Watz wengine waliouawa nani awasemee kama mnajibagua katika mambo yaliyoikumba nchi yote au ndio ule usemi wa; "yaa rabbi nafsi yangu"??!---- in this case CDM should adopt universality- as the major opposition party-- to express the matter nationally and internationally.

Huwezi akatamka hadharani eti; "sisi ndio tumeumizwa sana" ili iweje??!--- ili mpewe madaraka kushika nchi kama retribution and consolence ya kuumizwa kwenu??!

Katika utawala wa kidhalimu yule anayepigana zaidi ndiye huyo atakayelipia zaidi adhabu, hii ni kama askari jeshi katika mstari wa mbele wa mapambano kama wakifa je itakuwa vyema kwa kamanda wao aanze kulialia hadharani eti wao ndio wamekufa zaidi kuliko watu wengine ??!!,---- Vipi mbona Kamanda Mbowe anajishusha hivyo??!, yale Magwanda na Ukamanda wake ni wa nini kama ni mliaji hadharani kiasi hicho??!! 🤣
 
Mnapoteza nguvu zenu bure kupambana na wimbi la kuimarisha HAKI nchini. Katiba ya wananchi yaja kuisafisha nchi. Enenda ukatubu uwe safi, uondokane na hofu kama za mafarisayo. Utaishi kwa amani.
 
Mnapoteza nguvu zenu bure kupambana na wimbi la kuimarisha HAKI nchini. Katiba ya wananchi yaja kuisafisha nchi. Enenda ukatubu uwe safi, uondokane na hofu kama za mafarisayo. Utaishi kwa amani.


Shida ni kwamba huwa hamkubali ukweli, unakuwa kama mkananayo na msadukayo??!!, nenda kabatizwe katika maji ya Bahari huenda ukakubali ukweli kwani ukweli will set you free.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…