Zitto Kabwe afunguliwa kesi na Harbinder Singh kisa sakata la IPTL

Kiongozi Mkuu mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa zamani Zitto Kabwe amefunguliwa Kesi na Harbinder Singh Seth akidaiwa kumkashifu mfanyabiashara huyo na kumvunjia heshima mbele ya jamii

Akizungumza na wanahabari leo Zitto Kabwe amesema kuwa kesi hiyo imetokana na yeye kuzungumzia sakata la IPTL (Kampuni ya kufua umeme) ambapo Seth ameomba kulipwa ‘mabilioni’ ya fedha

"Nimewaita hivi leo kwasababu ya kesi ambayo nimefunguliwa na mtu anayeitwa bwana Harbinder Singh Seth kuwa nimemkashifu na kumshushia heshima mbele ya jamii kwa vile eti nimezungumzia sakata la IPTL (Kampuni ya kufua umeme), na ameomba mahakama mbali na mambo mengine nimlipe ‘mabilioni’ ya fedha"

"Tuhuma hizo za bwana Seth kwanza si za kweli, kwasababu sijamkashifu na wala kumshushia heshima, lakini ninampongeza sana na kumshukuru kwa ujasiri wake wa kunishitaki kwasababu kesi hii itatoa fursa ya kumaliza jambo hili linaloweka wingu kwa muda mrefu sana katika taifa letu, lakini pia kesi hii itanipa nafasi ya kuweka ukweli wote wazi na mwisho kuufukia kabisa huu mzoga unaoitwa sakata la IPTL"

"Binafsi sikatai kuandika maneno ambayo bwana Seth (Harbinder Seth- Mmiliki wa kampuni ya IPTL ya ufuaji wa umeme) ananituhumu nayo kwamba nimemkashifu , maneno hayo niliyaandika na kuyachapisha katika akaunti yangu ya X zamani Twitter, na maneno yale yanaakisi picha halisi na yenye ukweli wa jambo zima hili la IPTL"

"Pili maneno haya mimi niliyaongea kwa nia njema kabisa, ya kutaka kupata ufumbuzi wa sakata hili, na tatu, maneno yale niliyasema kwavile mimi nilibahatika kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyoshughulikia sakata la IPTL"

"Kama unakumbuka wakati ule maarufu lilivyojulikana kama sakata la Escrow, hivyo nilitumia fursa hiyo kuwaeleza Watanzania wenzangu ukweli wa jambo hili, kwasababu ninafahamu ukweli wa jambo hilo, na ni wajibu wangu kama raia kulinda rasilimali za taifa dhidi ya njama zozote zile za kupora rasilimali hizo kwa kisingizio cha uwekezaji".

Si wanajuana hao?
 
Duh hii nchi hii....

Huenda miaka Kenda ijayo tutakuwa tunazungumzia mwanasiasa fulani kufunguliwa kesi na ADANI au yoyote yule tutakayempa TANESCO badala ya kuongelea authenticity ya hawa mafisadi na jamaa zao walamba asali wanaonufaika na hii Mikataba ya Ki Mangungo....
 
Hajahabarisha anajitetea! Hiyo sio habari ni utetezi, angepaswa akautoe mahakamani. Soma utetezi wake. Wakili wake, angeweza habarisha kwa niaba yake.

Tayari ukiangalia lugha ya mwili ya mwanasiasa huyu mkongwe ameshajua mchezo wa nyuma ya pazia, dola inamtumia raia mmoja dhidi ya mwingine kuekekea uchaguzi 'huru' wa Oktoba 2025
 
Ukome kabisa Zito Kabwe ulishangilia sana kufa cha Magufuli hadi ukasema anayempenda Magufuli akazikwe nae, kumbe hukujua kuwa mbaya wako Seth ametulizwa na Magufuli. 😄.
Ipo siku mtanikumbuka kwa mazuri na si kwa mabaya ~~~ Magufuli
 
Kiongozi Mkuu mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa zamani Zitto Kabwe amefunguliwa Kesi na Harbinder Singh Seth akidaiwa kumkashifu mfanyabiashara huyo na kumvunjia heshima mbele ya jamii

Akizungumza na wanahabari leo Zitto Kabwe amesema kuwa kesi hiyo imetokana na yeye kuzungumzia sakata la IPTL (Kampuni ya kufua umeme) ambapo Seth ameomba kulipwa ‘mabilioni’ ya fedha

"Nimewaita hivi leo kwasababu ya kesi ambayo nimefunguliwa na mtu anayeitwa bwana Harbinder Singh Seth kuwa nimemkashifu na kumshushia heshima mbele ya jamii kwa vile eti nimezungumzia sakata la IPTL (Kampuni ya kufua umeme), na ameomba mahakama mbali na mambo mengine nimlipe ‘mabilioni’ ya fedha"

"Tuhuma hizo za bwana Seth kwanza si za kweli, kwasababu sijamkashifu na wala kumshushia heshima, lakini ninampongeza sana na kumshukuru kwa ujasiri wake wa kunishitaki kwasababu kesi hii itatoa fursa ya kumaliza jambo hili linaloweka wingu kwa muda mrefu sana katika taifa letu, lakini pia kesi hii itanipa nafasi ya kuweka ukweli wote wazi na mwisho kuufukia kabisa huu mzoga unaoitwa sakata la IPTL"

"Binafsi sikatai kuandika maneno ambayo bwana Seth (Harbinder Seth- Mmiliki wa kampuni ya IPTL ya ufuaji wa umeme) ananituhumu nayo kwamba nimemkashifu , maneno hayo niliyaandika na kuyachapisha katika akaunti yangu ya X zamani Twitter, na maneno yale yanaakisi picha halisi na yenye ukweli wa jambo zima hili la IPTL"

"Pili maneno haya mimi niliyaongea kwa nia njema kabisa, ya kutaka kupata ufumbuzi wa sakata hili, na tatu, maneno yale niliyasema kwavile mimi nilibahatika kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyoshughulikia sakata la IPTL"

"Kama unakumbuka wakati ule maarufu lilivyojulikana kama sakata la Escrow, hivyo nilitumia fursa hiyo kuwaeleza Watanzania wenzangu ukweli wa jambo hili, kwasababu ninafahamu ukweli wa jambo hilo, na ni wajibu wangu kama raia kulinda rasilimali za taifa dhidi ya njama zozote zile za kupora rasilimali hizo kwa kisingizio cha uwekezaji".

Harbinder Sing anaenda kuibua sintofahamu mpya katika tasnia ya siasa.
 
Harbinder, Rostam, Jakaya, Kinana, the stiff necks.

Seems they haven't learned their lesson.​
 
Huyu singasinga atapata aibu.
Hawa akina Kabwe wanajua kila kitu
Ngoja tuone.
 
Huyu singasinga atapata aibu.
Hawa akina Kabwe wanajua kila kitu
Ngoja tuone.
 
Amfungulie na Kafulila, aliyepigania hizo pesa mpaka akaitwa tumbili.
Tumbili analamba asali kwa sasa anaweza kabisa kusema Singh alionewa na alipwe mabilione mengine kama fidia
 
Back
Top Bottom