Zitto Kabwe ahofia kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kufungwa pindi atakaporejea nchini

Zitto Kabwe ahofia kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kufungwa pindi atakaporejea nchini

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
1581055384551.png

Hofu hiyo inatokana na kile alichokiita mfululizo wa vitisho vilivyotolewa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hofu hiyo ya Zitto imeibuka baada ya Kiongozi Mkuu huyo ACT Wazalendo kuandika barua kwa Benki ya Dunia (WB) kuitaka kusitisha mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kwa Tanzania kutokana na kile alichodai kuna ubaguzi katika elimu kwa watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni.

Zitto alieleza hofu yake hiyo jana, akidai kuwa analichukulia kwa uzito suala hilo kwa kuwa upo mfano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kupigwa risasi mjini Dodoma na hadi sasa ameshindwa kurejea nchini kutokana na hofu ya usalama wake.

“Ninachukulia vitisho hivi kwa uzito kwa sababu tuna mfano wa mwenzetu Lissu, lakini usije kushangaa ukisikia nimekamatwa na kufungwa nitakaporejea Tanzania kwa sababu sasa hivi kesi za utakatishaji fedha zinatumika kuwanyamazisha wakosoaji kwa sababu mashtaka yake hayana dhamana," alisema.

Wiki iliyopita, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, kuchunguza kitendo cha Zitto kuiandikia barua WB kuzuia mkopo huo ili kuona kama kuna jinai au la na kumchukulia hatua mbunge huyo kufuatia hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Siha, DK. Godwin Mollel (CCM), kutaka kuchunguzwa kwa jambo hilo.

Zitto kwa sasa yuko Amerika ya Kaskazini kwa shughuli ambazo chama chake hakijaziweka wazi kwa umma.


IPP Media
 
Dawa ni kuuondoa utawala wa kimabavu mwezi October.
 
Hii hapa chini ni Tweet ya Zitto na ambayo nimeitumia kumtahadharisha:

"Tunamaliza ziara yetu ya nchi za nje kwa awamu ya kwanza hapa Marekani kwa kukutana na Watanzania wanaoishi hapa. Jumapili nitakuwa Dar es Salaam kwa ajili ya Kesi Kisutu, Shughuli kadhaa za chama na kisha kuendelea na ziara Afrika. Shabaha yetu kubwa ni UCHAGUZI HURU na HAKI"
 
Hii hapa chini ni tweet ya Zitto na ambayo nimeitumia kumtahadharisha:

Tunamaliza ziara yetu ya nchi za nje kwa awamu ya kwanza hapa Marekani kwa kukutana na Watanzania wanaoishi hapa. Jumapili nitakuwa Dar es Salaam kwa ajili ya Kesi Kisutu, Shughuli kadhaa za chama na kisha kuendelea na ziara Afrika. Shabaha yetu kubwa ni UCHAGUZI HURU na HAKI
Kwa sababu Mbowe kakataliwa kwenda Marekani au?!!
 
Serikali na Bunge wanasaidia sana wapinzani ku balance story. Ziara ya Zitto imefanikiwa sana Bunge nililitoa ushahidi muhimu kwa mjadala.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kitendawili, "Rais wa ajabu haijui Marekani.….…
 
Hii nchi imejaa kambare watupu na kila mtu ana sharubu! Kila mtu anaongelea masuala ya kitaifa kana kwamba hatuna mkuu wa nchi!

Rais hayuko kwa ajili ya wapinzani, yeye kwake wapinzani ni kama watoto kwa kambo. Sasa pata picha mtoto wa kambo angoje maslahi yake yasemewe na mama wa kambo.
 
Hii hapa chini ni Tweet ya Zitto na ambayo nimeitumia kumtahadharisha:

"Tunamaliza ziara yetu ya nchi za nje kwa awamu ya kwanza hapa Marekani kwa kukutana na Watanzania wanaoishi hapa. Jumapili nitakuwa Dar es Salaam kwa ajili ya Kesi Kisutu, Shughuli kadhaa za chama na kisha kuendelea na ziara Afrika. Shabaha yetu kubwa ni UCHAGUZI HURU na HAKI"
Zitto go go go Zitto usiangalie. Tumebaguliwa Sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom