Zitto Kabwe ahofia kukamatwa, kufunguliwa mashtaka na kufungwa pindi atakaporejea nchini

Mbunge wa kigoma mjini amefungua kuwa anaogopa kurudi nchii kwa sababu anahofia usalama wake baada ya kuikosesha tanzania mkopo mkubwa uliokuwa na thamani ya sh $500m katika sekta ya elimu.

Chanzo: VOA

. Zitto naogopa kurudi tz nimeambiw...tishiwa maisha. https://youtu.be/XjWtP1oD1wU

Sent using Jamii Forums mobile app
 
PavelJr,
Taarifa zilizopo ni kuwa anatafuta ukimbizi nchi ya Canada .Marekani aliogopa kwenda kuna vitu fulani wanamjua kwa undani sana.Mbowe pia alitaka kwenda akaombe hifadhi canada.Ila kuna kisiki Zitto na Mbowe hawawezi fanikiwa hata LIsu hawezi

WAlikanyaga maslahi ya marekani na canada kwa kupiga vita wasiuze ndege zao kwa Tanzania.Mnakumbuka Zitto alifikia hadi kutamka kuwa ndege tunazoletewa ni mitumba.Akadhalilisha kampuni kubwa inayoheshimiwa duniani na kuichafua jina kuwa inauza mitumba

Anatapa tapa tu hadhi ya ukimbizi hawezi pata Canada wala Marekani
 
Hii technic ya kuzurura huko nje ni fimbo nzuri sana ya kuichapa CCM!
 
huyo ZITO wenu ni ndumilakuwili na wala ajawa na ushawishi wowote katika nchi ( tishio
Kidogo tishio alikuwa Dr Slaa.

Lakini sio ZITO ni nyie tu ambao mpo twitter, Facebook, Instagram ndio mnaosoma habari za ZITO uko vijijini ccm itakuwa inazoa kula kwa tiba za mchanga sio tena sanduku.

Siasa za upinzani Tanzania zimeshakufa upinzani umebaki YouTube, Facebook, Instagram na Twitter

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Rais hayuko kwa ajili ya wapinzani, yeye kwake wapinzani ni kama watoto kwa kambo. Sasa pata picha mtoto wa kambo angoje maslahi yake yasemewe na mama wa kambo.
Wapinzani ndo watu gani? Au ndo mapandikizi ya mabeberu?
 
Passport hizo hutolewa kwa watu waungwana wasio wahalifu

Ndio maana Rais ndiye mdhamini wako kwenye Passport hiyo sasa kama kwenye Passport anayewaagiza watu wa nchi zingine mpaka wakulinde huyo huyo unamponda bila aibu mpaka unaingilia shughuli za utendaji wa Baraza la mawaziri
Maana mkopo huo umebarikiwa na baraza la mawaziri mwenyekiti ni Rais
 
Duu hii kali.
Hapana msifanye hivyo mtaonekana kweli mnaminya demokrasia, mtawapa sababu adui zenu.
 
Wenzenu wanasubiri mjichanganye mfanye mambo kwa papara na hasira wapate ushahidi wa wanayo watuhumu.
 
Passport hizo hutolewa kwa watu waungwana wasio wahalifu

Ndio maana Rais ndiye mdhamini wako kwenye Passport hiyo sasa kama kwenye Passport anayewaagiza watu wa nchi zingine mpaka wakulinde huyo huyo unamponda bila aibu mpaka unaingilia shughuli za utendaji wa Baraza la mawaziri
Maana mkopo huo umebarikiwa na baraza la mawaziri mwenyekiti ni Rais
Huna akili, badala ya kujibu hoja mnakimbilia kutafuta sababu za kimabavu za kijinga kabisa. Suala la udhamini wa passport upo kikatiba na wala sio fadhila, nchi ni yetu sote acha utoto.
 
PavelJr,
Taarifa zilizopo ni kuwa anatafuta ukimbizi nchi ya Canada .Marekani aliogopa kwenda kuna vitu fulani wanamjua kwa undani sana.Mbowe pia alitaka kwenda akaombe hifadhi canada.Ila kuna kisiki Zitto na Mbowe hawawezi fanikiwa hata LIsu hawezi

WAlikanyaga maslahi ya marekani na canada kwa kupiga vita wasiuze ndege zao kwa Tanzania.Mnakumbuka Zitto alifikia hadi kutamka kuwa ndege tunazoletewa ni mitumba.Akadhalilisha kampuni kubwa inayoheshimiwa duniani na kuichafua jina kuwa inauza mitumba

Anatapa tapa tu hadhi ya ukimbizi hawezi pata Canada wala Marekani
Bibi yako mzaa babu yako ndio alikusimilia haya mlipokuwa mmekaa mkiota huku mmeuzunguka moto nje kabla ya kulala?
 
Hofu hiyo inatokana na kile alichokiita mfululizo wa vitisho vilivyotolewa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hofu hiyo ya Zitto imeibuka baada ya Kiongozi Mkuu huyo ACT Wazalendo kuandika barua kwa Benki ya Dunia (WB) kuitaka kusitisha mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kwa Tanzania kutokana na kile alichodai kuna ubaguzi katika elimu kwa watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni.

Zitto alieleza hofu yake hiyo jana, akidai kuwa analichukulia kwa uzito suala hilo kwa kuwa upo mfano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kupigwa risasi mjini Dodoma na hadi sasa ameshindwa kurejea nchini kutokana na hofu ya usalama wake.

“Ninachukulia vitisho hivi kwa uzito kwa sababu tuna mfano wa mwenzetu Lissu, lakini usije kushangaa ukisikia nimekamatwa na kufungwa nitakaporejea Tanzania kwa sababu sasa hivi kesi za utakatishaji fedha zinatumika kuwanyamazisha wakosoaji kwa sababu mashtaka yake hayana dhamana," alisema.

Wiki iliyopita, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, kuchunguza kitendo cha Zitto kuiandikia barua WB kuzuia mkopo huo ili kuona kama kuna jinai au la na kumchukulia hatua mbunge huyo kufuatia hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Siha, DK. Godwin Mollel (CCM), kutaka kuchunguzwa kwa jambo hilo.

Zitto kwa sasa yuko Amerika ya Kaskazini kwa shughuli ambazo chama chake hakijaziweka wazi kwa umma.

IPP Media
Ooooh! Zitto! Njooo upambabe na dhambi ya usaliti kibaraka mkubwa wa mabeberu! Hivi mwenye akili timamu unaanzaje (kwa mfano) kutumia kofia ya ubunge (uliyopewa kuwatetea wananchi wa nchi yako) badala yake unaiandikia Benk ya Dunia (WB) isiipe nchi yako mkopo? Kwani wewe ni nani kati ya watanzania million 50? Kwavile unakula na kushiba kodi za watanzania masikini na wanyonge ndo unapata nguvu za kwenda juu kuzuia hela za kuwakomboa hao wanyonge ili watoke kwenye umasikini? Hakika Zitto ni Adui wa taifa (enemy of the state)
 
Hofu hiyo inatokana na kile alichokiita mfululizo wa vitisho vilivyotolewa na viongozi mbalimbali wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Hofu hiyo ya Zitto imeibuka baada ya Kiongozi Mkuu huyo ACT Wazalendo kuandika barua kwa Benki ya Dunia (WB) kuitaka kusitisha mkopo wa Dola za Marekani milioni 500 kwa Tanzania kutokana na kile alichodai kuna ubaguzi katika elimu kwa watoto wa kike waliopata ujauzito wakiwa shuleni.

Zitto alieleza hofu yake hiyo jana, akidai kuwa analichukulia kwa uzito suala hilo kwa kuwa upo mfano wa aliyekuwa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema), kupigwa risasi mjini Dodoma na hadi sasa ameshindwa kurejea nchini kutokana na hofu ya usalama wake.

“Ninachukulia vitisho hivi kwa uzito kwa sababu tuna mfano wa mwenzetu Lissu, lakini usije kushangaa ukisikia nimekamatwa na kufungwa nitakaporejea Tanzania kwa sababu sasa hivi kesi za utakatishaji fedha zinatumika kuwanyamazisha wakosoaji kwa sababu mashtaka yake hayana dhamana," alisema.

Wiki iliyopita, Spika wa Bunge, Job Ndugai, alimtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Profesa Adelardus Kilangi, kuchunguza kitendo cha Zitto kuiandikia barua WB kuzuia mkopo huo ili kuona kama kuna jinai au la na kumchukulia hatua mbunge huyo kufuatia hoja binafsi iliyowasilishwa bungeni na Mbunge wa Siha, DK. Godwin Mollel (CCM), kutaka kuchunguzwa kwa jambo hilo.

Zitto kwa sasa yuko Amerika ya Kaskazini kwa shughuli ambazo chama chake hakijaziweka wazi kwa umma.

IPP Media
Kwasababu hatukumtuma,apambane na hali yake hakuna huruma ya wananchi hapa. Labda ma-bwana zake aliowaandikia barua watamuhurumia,ila asisahau hao wazungu wakielewana na serikali yeye watamtelekeza kwa ndugu mwandishi.

macson
 
Back
Top Bottom