Zitto Kabwe aitaka CHADEMA iweke hadharani Mapendekezo waliyompelekea Rais Samia kwani kufichaficha kunatia shaka

Zitto Kabwe aitaka CHADEMA iweke hadharani Mapendekezo waliyompelekea Rais Samia kwani kufichaficha kunatia shaka

Kiongozi mkuu wa ACT wazalendo mh Zitto Kabwe amekitaka chama kikuu cha Upinzani CHADEMA kuweka hadharani Mapendekezo waliyompelekea Rais Samia Ikulu ya Chamwino

Zitto Kabwe ambaye ni mjumbe wa Kikosi kazi cha Profesa Mkandala amedai mambo ya kufichaficha hayaleti taswira njema kwa wananchi.

Katika tweet yake Zitto Kabwe amesema kwa kutambua umuhimu wa uwazi ACT wazalendo kilielezea yale waliyopendekeza kwenye Kikosi kazi cha Prof Mkandalla.
Awaulize kwanza CCM waeleze mapendekezo yao waliyotoa kwenye kikosikazi maalum.

Sent from my TECNO LC6a using JamiiForums mobile app
 
Kiongozi mkuu wa ACT wazalendo mh Zitto Kabwe amekitaka chama kikuu cha Upinzani CHADEMA kuweka hadharani Mapendekezo waliyompelekea Rais Samia Ikulu ya Chamwino

Zitto Kabwe ambaye ni mjumbe wa Kikosi kazi cha Profesa Mkandala amedai mambo ya kufichaficha hayaleti taswira njema kwa wananchi.

Katika tweet yake Zitto Kabwe amesema kwa kutambua umuhimu wa uwazi ACT wazalendo kilielezea yale waliyopendekeza kwenye Kikosi kazi cha Prof Mkandalla.

Kutoka kumuombea Mbowe msamaha mpaka kutaka kujua chadema wanazungukana Nini na CCM
 
Huko ikulu ni kwa raisi wa wapi? Ye afahamu matatizo ya watanzania
Sasa kama Raisi anafahamu wao wanaenda kufanya nini? Nawao niwatanzania so Raisi atakuwa anayafahamu matatizo yao.
 
Hivi hawa jamaa wakiendaga uko Ikulu wanakumbuka kweli kuzungumzia hali ya maisha ya watanzania Au wanajali tu biashara yao inayobatizwa jina la siasa

Kila mazungumzo Yana context yake na hadidu rejea. Halafu unataka kura uipe CCM kuanzia Mwenyekiti wa Kijiji mpaka mbunge lakini shida za wananchi uwatupie chadema. Tuache ubinafsi.
 
Chadema wamepeleka mapendekezo ya Mbowe arudishiwe bilicanas yake, Lissu alipwe mafao yake, Wenje na Lema warudi Tanzania.

Hayo yakwako kujifurahisha. Kwenye siasa za Tanzania huwezi kuiweka pembeni. Serikali ilitaka kuifuta chadema bungeni, lakini mwishoni wa siku ilibidi wakawaonge akina Halima Mdee waje bungeni.
 
Biashara tunajua ilifanyika akiwa jela ili kunusurika lakini chadema nayo igeuzwe kuwa TLP na sasa mnashinda Ikulu muda wote kwisha habar yenu., wananchi watapambana wenyewe kivyao kudai katiba, watanganyika hawana dhamana

CHADEMA walikataa kuonana na kikosi kazi au kushiriki mikutano ya TCD. Msimamo wao ndio unefanya waonane na Rais.
 
Kila mazungumzo Yana context yake na hadidu rejea. Halafu unataka kura uipe CCM kuanzia Mwenyekiti wa Kijiji mpaka mbunge lakini shida za wananchi uwatupie chadema. Tuache ubinafsi.
Wao wanaenda kufanya nini Ikulu kama wanachoenda kukizungumza hakihusu wananchi na ni chama cha siasa ambacho kina malengo ya kuongoza nchi.

Wanaenda kufanya baishara na Raisi?
 
Kabissa tena waweke wazi sasa, mashaka kwa chadema yameanza tokea mbowe alipotolewa jela baada ya miezi 8 pamoja na kuwa na kesi ya kujibu lakin gafla akafutiwa kesi lakini break ya kwanza akatia maguu Ikulu ya Samia lakini sio hapo tu sasa ni kawaida yake kwenda Ikulu lakini hofu zaidi Tundu Lissu pia ambaye ni msemaji kwa kila kinachotokea hili hajaweza kulitolea fatwaa. giza ni nene
Mwenyekiti humjulisha lissu kila hatua kwa uwazi ili kulinda maslahi na siri za chama, chama chochote kina siri za chama na agenda zake
 
Mbona kama ana tetemeka?

Zitto ni sehemu ya serikali, namshauri awapigie washirika wake wamwambie hayo mapendekezo ya Chadema.
Nilimuona juzi yupo na wasira live TBC hadi aibu sijui zitto kapatwa na nini??
 
Hivi hawa jamaa wakiendaga uko Ikulu wanakumbuka kweli kuzungumzia hali ya maisha ya watanzania Au wanajali tu biashara yao inayobatizwa jina la siasa
Wewe ni ccm,kweli na wewe unawategemea Chadema!!! Bunge lote almost 99% ni ccm, hawakutoshi kweli???
 
Kiongozi mkuu wa ACT wazalendo mh Zitto Kabwe amekitaka chama kikuu cha Upinzani CHADEMA kuweka hadharani Mapendekezo waliyompelekea Rais Samia Ikulu ya Chamwino

Zitto Kabwe ambaye ni mjumbe wa Kikosi kazi cha Profesa Mkandala amedai mambo ya kufichaficha hayaleti taswira njema kwa wananchi.

Katika tweet yake Zitto Kabwe amesema kwa kutambua umuhimu wa uwazi ACT wazalendo kilielezea yale waliyopendekeza kwenye Kikosi kazi cha Prof Mkandalla.
Muda mwingne zitto Yuko Sawa Kabsa, Safari za chadema ikulu lazma iwe na maswali mengi lazma watoe mrejesho wanaenda kufanya Nini Kwa wanachama wao na wwtanzania Kwa ujumla. Leo unakutana na Samia kësho wanagoma kukutana na Kikosi Kazi kilichoundwa na huyo huyo wanayekutana nae. Kinadharia wanaonesha wao washatoa mapendekezo Yao Kwa RAIS.
 
Zitto anaiagiza Chadema akiwa na wadhifa gani Chadema? Awaagize Ccm wanao mtumia.
 
Back
Top Bottom