Mwanamwana
Platinum Member
- Aug 1, 2011
- 9,604
- 22,722
Mahakama Kuu ya Tanzania imetupilia mbali kesi ya madai ya matusi iliyokuwa ikimkabili Kiongozi wa Chama Mstaafu wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, iliyofunguliwa na Harbinder Singh Sethi wa kampuni ya Pan Africa Power Solutions Ltd (PAP).
Pia soma > Zitto Kabwe afunguliwa kesi na Harbinder Singh kisa sakata la IPTL
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa Desemba14, 2025 na Msemaji wa Ofisi binafsi ya Zitto Kabwe, Rahma Salum, hukumu hiyo ilitolewa Alhamisi Desemba 11, 2025, na Mheshimiwa Jaji Arnold Kirekiano ambaye alibaini kuwa mlalamikaji ameshindwa kuthibitisha madai yake kwa kiwango kinachohitajika kisheria.
Katika uamuzi wake, Jaji Kirekiano alisema mahakama imejiridhisha kuwa kauli za Zitto Kabwe alizotoa kupitia akaunti yake ya mtandao wa kijamii wa X (zamani Twitter) tarehe 5 Aprili 2025 hazikuwa za uongo wala za hila, bali zilihusu maslahi ya umma, hususan matumizi ya fedha za umma.
"Nabaini kuwa mlalamikaji hajathibitisha kwa kiwango kinachohitajika kisheria, kuwa chapisho hilo lilikuwa la uongo na la hila. Aidha nimebaini kuwa chapisho hilo lilihusu suala la maslahi ya umma, yaani fedha za umma." Alisema Jaji Kirekiano
Mahakama pia ilikataa hoja zote tatu zilizowasilishwa na Sethi, ambaye alikuwa akidai fidia ya jumla ya Shilingi bilioni 15, ikijumuisha Shilingi bilioni 10 kwa madai ya kuchafuliwa na Shilingi bilioni 5 kama fidia ya jumla. Kutokana na hilo, mahakama ilihitimisha kuwa hakuna fidia yoyote inayostahili kutolewa na hivyo kuitupilia mbali kesi hiyo kwa gharama za mlalamikaji.
Katika kesi hiyo, Sethi alidai kuwa chapisho la Zitto Kabwe lililomtaka Msajili wa Makampuni (BRELA) kufuta usajili wa kampuni ya Independent Power Tanzania Limited (IPTL) lilimchafua na kumwonesha kama tapeli, jambo alilodai liliharibu sifa yake mbele ya jamii, wawekezaji na jumuiya yake ya kidini.
Hata hivyo, kupitia mawakili wake, Moses Mgonja na Anitha Nyangahondi, Zitto Kabwe alikanusha madai hayo akisisitiza kuwa kauli zake zilikuwa za kweli, za nia njema na ni maoni halali kuhusu masuala yanayogusa maslahi ya umma.
Zitto alieleza kuwa uzoefu wake kama Mbunge wa zamani na Mwenyekiti wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali (PAC) na Mashirika ya Umma (POAC) ulimpa uelewa mpana wa sakata la IPTL, hususan katika muktadha wa ripoti za CAG.