SI KWELI PreGE2025 Zitto Kabwe ameandika 'CHADEMA na wanaharakati sasa wamekuwa mashabiki wa CCM'

SI KWELI PreGE2025 Zitto Kabwe ameandika 'CHADEMA na wanaharakati sasa wamekuwa mashabiki wa CCM'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Source #1
View Source #1
photo_2025-07-23_15-35-36.jpg
 
Tunachokijua
Zitto Kabwe ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT- Wazalendo aliyehudumu nafasi hiyo kwa muongo mmoja. Zitto alihamia ACT- Wazalendo mwaka 2015 baada ya kuvuliwa uanachama ndani ya CHADEMA kutokana na kilichoelezwa kukiuka katiba ya chama hicho kwa kupeleka mahakamani migogoro ambayo ilitakiwa kushughulikiwa ndani ya chama kwa mujibu wa katiba.

Kupitia tiketi ya CHADEMA Zitto aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini mwaka 2005 mpaka 2015. Akiwa kiongozi mstaafu ndani ya ACT- Wazalendo ameendelea kuwa mwanachama muhimu ndani ya chama hicho kutokana na uzoefu wake wa muda mrefu katika siasa za Tanzania.

Lipo andiko linalosambazwa mtandaoni likonekana kuchapishwa na Zitto Kabwe kwenye mtandao wa X kuwa "CHADEMA na wanaharakati sasa wamekuwa mashabiki wa CCM badala ya kuwa wapinzani.

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key word search) umejiridhisha kuwa andiko hilo si la kweli bali ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halijachapishwa na Zitto Kabwe kupitia Kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii.

Kumbuka wapotoshaji wanaweza kutengeneza machapisho kwa kutumia utambulisho wa watu maarufu kama wanasiasa, viongozi wa serikali, wasanii na kadhalika, ili kusambaza taarifa zisizo za kweli. Rejea hapa, hapa na hapa.​
Hata kama imetengenezwa, lakini ujumbe ulioandikwa ndio hali halisi. CHADEMA wamesahau ajenda zao katika wiki hii na kushadadia ajenda ya mgombea urais kwa tiketi ya CCM. Kufanya hivyo ni ukilema wa focus.
Rudini kwenye ajenda zenu.
 
Acha wajadili madudu yenu huko fisiem. Kwani mlitaka wafanyeje baada ya kuwazuia wasifanye siasa kwa muda usiojulikana, kuwabambikia mashtaka viongozi wao na kufungia ofisi zao?
 
Acha wajadili madudu yenu huko fisiem. Kwani mlitaka wafanyeje baada ya kuwazuia wasifanye siasa kwa muda usiojulikana, kuwabambikia mashtaka viongozi wao na kufungia ofisi zao?
Kama ni hivyo, nyie wote karibuni CCM. Mkachukue kadi za CCM. Ili mkashiriki kumchagua mgombea Urais.
 
Back
Top Bottom