Zitto Kabwe ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha
ACT- Wazalendo aliyehudumu nafasi hiyo kwa muongo mmoja. Zitto alihamia ACT- Wazalendo mwaka 2015 baada ya
kuvuliwa uanachama ndani ya CHADEMA kutokana na kukiuka katiba ya chama hicho kwa kupeleka mahakamani migogoro ambayo ilitakiwa kushughulikiwa ndani ya chama kwa mujibu wa katiba.
Katika mtandao wa Facebook ilichapishwa
taarifa iliyotumia grafiki yenye utambulisho wa Jambo TV ikinukuu andiko linaloonekana kuchapishwa na Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa X, likisema 'CHADEMA waache siasa za hofu na uzushi, kauli za sumu ni propaganda isiyo na msingi'
Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa Kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa andiko lililonukuliwa katika taarifa hiyo si la kweli ni la kutengenezwa na wapotoshaji kwani halikuchapishwa na
Zitto Kabwe kwenye ukurasa wake wa X.
Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya Kughushi kwani
Jambo TV haikuchapisha kabisa katika kurasa zake rasmi za mitandao ya kijamii, bali Wapotoshaji walitumia Utambulisho huo ili kusambaza Taarifa Potoshi.