LGE2024 Zitto Kabwe aonya watakao bebeshwa kura ya ziada, asema yatakayowakuta wasilaumiane "Dua imesomwa, tendeni haki"

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
2,060
Reaction score
5,648
Zitto Kabwe ameonya vikali dhidi ya yeyote atakayethubutu kubebeshwa kura ya ziada, akisisitiza kwamba matokeo ya kitendo hicho hayapaswi kulaumiwa kwa mtu mwingine, kwani tayari dua imesomwa na wazee wa mji, na kinachotakiwa ni haki pekee.

"Msikubali kudanganywa na CCM kubeba kura ya ziada hata moja. Yatakayokukuta, usitulaumu. Wananchi wote wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, nendeni mkapige kura zenu moja kwa moja, mchague mnayemtaka. Msithubutu kuingia na kura ya ziada, kwa sababu yatakayokukuta tusilaumiane," alisisitiza Zitto.

Kwa wasimamizi wa uchaguzi, Zitto aliwataka kutekeleza wajibu wao kwa haki, akiongeza kuwa ACT Wazalendo ni chama cha amani kinachotafuta haki, lakini hawatakubali kuchokozwa. Aliwaonya wanaopokea maagizo ya kubadilisha matokeo au kutangaza washindi wasio halali, akisisitiza kuwa viongozi hao wanaowadanganya wana mahali pa kukimbilia, lakini wao watabaki wakikumbana na matokeo ya vitendo hivyo.

"Wazee wa mji wameomba dua na Mungu amesikia. Tunahitaji haki, siyo kuomba radhi baadaye. Tendeni haki sasa," alihitimisha.

Mwizi wa kura ni mwizi kama wezi wengine. Hata kama amevaa suti ni mwizi wachukuliwe hatua kali za kisheria kama wezi wengine.
 
Back
Top Bottom