Zitto Kabwe ameonya vikali dhidi ya yeyote atakayethubutu kubebeshwa kura ya ziada, akisisitiza kwamba matokeo ya kitendo hicho hayapaswi kulaumiwa kwa mtu mwingine, kwani tayari dua imesomwa na wazee wa mji, na kinachotakiwa ni haki pekee.
"Msikubali kudanganywa na CCM kubeba kura ya ziada hata moja. Yatakayokukuta, usitulaumu. Wananchi wote wa Manispaa ya Kigoma Ujiji, nendeni mkapige kura zenu moja kwa moja, mchague mnayemtaka. Msithubutu kuingia na kura ya ziada, kwa sababu yatakayokukuta tusilaumiane," alisisitiza Zitto.
Kwa wasimamizi wa uchaguzi, Zitto aliwataka kutekeleza wajibu wao kwa haki, akiongeza kuwa ACT Wazalendo ni chama cha amani kinachotafuta haki, lakini hawatakubali kuchokozwa. Aliwaonya wanaopokea maagizo ya kubadilisha matokeo au kutangaza washindi wasio halali, akisisitiza kuwa viongozi hao wanaowadanganya wana mahali pa kukimbilia, lakini wao watabaki wakikumbana na matokeo ya vitendo hivyo.
"Wazee wa mji wameomba dua na Mungu amesikia. Tunahitaji haki, siyo kuomba radhi baadaye. Tendeni haki sasa," alihitimisha.
Bwashe imagine ngamia aliwe na waha tuu afu impact iwe nchi nzima? Nani kasema?. Wao wafaidi nyama sisi wengine tufaidi laana?! Hakuna kitu kama hiyo. Zito hayupo seriou kabisa🤣🤣🤣🤣