Zitto Kabwe apendekeza TANESCO wauze hisa(20%) fedha itakayopatikana ilipe madeni, Waziri Makamba atoa maagizo

Aisee zito Hajui hata biashara zimaendaje huyu jamaa amewahi kuuza hata karanga kweli? Tanesco ikitoa hata robo ya hisa tu mzigo utamrudia mwananchi mana hakuna atakekubali shirika lijiendeshe kwa mauzo ya Luku tu, Yani muondoe connection fee, Monthly Service charge still pawe na faida???, Tanesco iendelee kuwa State owened Entity ni nzuri kiusalama pia, Nishati ni esential tool kwa Nchi tuzicheze na Nishati kabisa.

Afu kwa records za Tanesco nani aweke Mpunga wake Kununua share? Huku shirika halijawahi kutoa Dividend kwa Serikali ambaye ndio main financier

Tanesco iachwe iendelee kumilikiwa na Serikali ili wananchi wapate huduma kuna watu walidai Zitokee kampuni zingine mbadala zicompate na Tanesco kuondoa Monopoly nkawauliza nani anaweza kukufanyia haya kwa bei ya 27000

-Surveying Bure ambayo ina Labour charge na Transport
-Material Bure ambapo accessories kama wire tu ni zaidi 27k
- Connection ambayo ina involve labour charges na transport
Bado mteja huyo huyo awekwe D1 na kuuziwa umeme kwa 122 per unit seriously?
Mteja ashindwe Kuingiza umeme tanesco iwashe gari Km 60 kumfata Bure kabisa
 
Unanunua hisa kwenye shirika ambalo kila mwaka ni hasara ya Mabilioni lini shareholders watapata dividends? Ayatollah Zitto KAKURUPUKA!!!


Yaani tununue hisa ili zikalipe madeni?
Kwani sisi wanahisa tulikuwepo wakati shirika likikopa kwa hasara?
Nani atanunua hisa za shirika linaloendeshwa kwa hasara na siasa za CCM?
 
Hawa wangekubali ushandi tangu ile 2006 nchi ingepata heshima..

Haiwezekani nchi ina umri wa kikongwe kabisa inajadili kukatika umeme saa 10 nzima bila sababu ya msingi wala uwajibikaji kwa watu huku hizi hoja ndogo ndogo hazina nafasi tena
 
Wawekezaji wapo tayari kuzalisha na kusambaza umeme, kikwazo ni sheria iliyotungwa na wanasiasa, kwa sababu wanazojua wao.
Hawa wawekezaji Wakiruhusiwa na Tanesco ikafa kivyovyote basi Jua umeme utakuwa Anasa na sio Huduma kwa jamii, Wataumia wananchi wa chini hakuna investors atataka kuwaungia watu umeme kwa 27k afu awauzie unit 122 hayupo
 
Hivi mnaweza kutufafanulia ni kwa vipi Tanesco inapata hasara?

Kila kitu tunalipia, hii hasara inatokana na nini?
Kajifunze hesabu za kujumlisha na kutoa.
 
Ukishauza hisa 20%, then wahuni watakuja kutaka asilimia nyingine 20 ziuzwe, kisha watakuja tena na kutaka 20% nyingine ziuzwe. Hatimaye shirika lote liuzwe
 
Kiongozi wa Chama cha ACT wazalendo Zitto Kabwe amemshauri waziri wa nishati January Makamba apeleke DSE 20% ya hisa za Tanesco zikauzwe na fedha itakayopatikana itumike kulipa madeni ya Shirika.
Kama mwekezaji au Mlipa deni atafanikiwa kurudisha na kupata faida juu ya uwekezaji wake, kwanini Tanesco au serikali usifanye hivyo na kuondoa inefficiency? Au in efficiency inaondolea na uwekezaji na sio sisi wenyewe??
 
Watanzania hawajasahau Tanesco ilivyouzwa kwa South Africans na Serikali ya awamu ya 4 na kupata hasara kubwa. Wakati sasa Pesa za walipa kodi zimefanya kazi kubwa na JNHPP ipo karibu kwisha wameanza tena mbinu ile ile ili kuwakamua Watanzania.

Watanzania sio wajinga tena, hawa wote (Zito na January) wanaangalia matumbo yao - swala hili halitakubalika vyovyote vile. Kweli kuna watu wana tamaa kama fisi.
 
Waziri JANUARY MAKAMBA
Ndugu muheshimiwa waziri, nakupa pongezi kurudi ktk safu ya uongozi,

Pili, napenda kutoa maoni na ushauri wangu, imefika wakati shirika la umeme lijiendeshe kibishara na litengeneze faida, mfano soko la umeme liko wazi wateja wanahitaji huduma, lakini kupata huduma ya kuwekewa umeme utafatilia utadhani una kesi ya mauaji,kila siku jalada bado,
USHAURI.
Ktk kuchelewa kufungiwa umeme, Tanesco abaki mzalishaji wa umeme na mkusanya Kodi,msambazaji wapewe makampuni binafsi, hapo itasaidia ushindani, na huduma kufika kwa haraka, mfano unajenga nyumba Kuna wasambazaji 3 kila mmoja atakufata Mimi ntakufungia kwa mkopo, mwingine atasema Mimi ntakufungia nakupa na unit 100 bure, wew mteja utachagua uende kampuni gani,

Ndani ya muda mfupi umeme utaenea kote na suala la kucheleweshewa litakuwa historia,

Kwa Sasa mmeshusha Bei ya kuingiza umeme, lakini sio kwamba umepungua Bali itakuwa mmetengeneza mianya ya kuwaneemesha wafanyakazi wa Tanesco wasio waaminifu l guess.

BWAWA, la nyerere simamia liishe kwa wakati, watanzania wanakumbuka ulikuwa kinyume na mpango huo wakati ule, chonde chonde hutaeleweka, simama kidete utuachie alama sio lawama,,,
Peni imeisha wino, naingia kulea wazee
 

Tanesco haikukaguliwa na CAG
 
We kima nadhani huelewi hata maana ya soko la hisa ni nini
Watu wanakurupushwa brother, yaani kuiongoza hii nchi tabu sana; umaskini na ujinga vimetufanya tuwe watu wa wasiwasi tu muda wote. Hoja ya mtu (isitoshe ni pendekezo tu) kabla haijaeleweka tayari watu wamesharukia kwenye malalamiko. Hoja za waziri mwenyewe hata hawazizungumzii
 
Zitto ni familia ya kikwete wanajua wanachofanya hajaandika bahati mbaya
 
Nionavyo mimi, Tanesco imekosa management huru.
Sio Tanesco Tu
Mashirika yote ya umma yalirudushwa Utumishi..chini ya JPM..

Ilikuwa rasmi Utumishi ndo wanaajiri..
Makusanyo yote yanapelekwa hazina n.k
Centralisation ilikuwa policy rasmi
 
Duh watu wanahesabu kali nyie... apo wanaliwinda kudhibiti Bwawa la Nyerere ,Stieglers Gorge HEP ,kwishaaa !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…