SI KWELI Zitto Kabwe asema 'Hatutakubali kuvurugwa na kelele za wanaharakati nje'

SI KWELI Zitto Kabwe asema 'Hatutakubali kuvurugwa na kelele za wanaharakati nje'

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
photo_2025-10-10_09-21-11.jpg
 
Tunachokijua
Zitto Kabwe ni mwenyekiti mstaafu wa chama cha ACT- Wazalendo aliyehudumu nafasi hiyo kwa muongo mmoja. Zitto alihamia ACT- Wazalendo mwaka 2015 baada ya kuvuliwa uanachama ndani ya CHADEMA kutokana na kukiuka katiba ya chama hicho kwa kupeleka mahakamani migogoro ambayo ilitakiwa kushughulikiwa ndani ya chama kwa mujibu wa katiba. Kupitia tiketi ya CHADEMA Zitto aliwahi kuwa mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini mwaka 2005 mpaka 2015.

Katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 Zitto ni mgombea wa ubunge katika jimbo la Kigoma mjini ambaye amekuwa mstari wa mbele na chama chake kuhamasisha wananchi kushiriki uchaguzi kupitia agenda ya 'Linda kura'

Madai
Kumekuwepo na taarifa inayosambazwa mtandaoni ikitumia utambulisho wa grafiki za Mwanahalisi kuwa Zitto Kabwe asema 'Hatutakubali kuvurugwa na kelele za wanaharakati nje'

Je, ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu umejiridhisha kuwa taarifa hiyo si ya kweli kwani ujumbe ulionukuliwa ni wa kughushi kwani haujachapishwa na Zitto kwenye ukurasa wake rasmi wa mtandao wa X.

Vilevile grafiki iliyotumika kusambaza taarifa hiyo ni ya kughushi kwani haijachapishwa na Mwananchi kama inavyoonekana.​
Back
Top Bottom