Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

Zito Hana anachoweza kuzuia mkopo toka taasisi yeyeto duniani.Kuamini hivo ni kumsingizia wao ufanya tafiti kabla ya kujidhihirisha,hakuna yeyeto asiyejua kwamba tunatawaliwa na madhalimu yanayokandamiza haki za wengi.Wao wamechunguza wamethibitisha ya kwamba Pesa zao haziendi tumika kwenye malengo kusudio elimu ni kama chambo tu kupitishia.Zitto hana nguvu yeyeto ya kuzuia makubaliano ya nchi na taasisi yeyeto
 
Ukisikia kunyimwa kura unadhani ni lazima ukose hata kura moja? Kura za watu wa mjini sio kura? au kura za watu wa mjini zina thamani nusu? Zamani ndio kulikuwa na hiyo Hadaa eti ccm wanashinda vijijini ila sio sasa. Wanachokifanya ccm kwenye chaguzi kiko wazi usidhani hatuoni uhayawani wao. Wapinzani hawataki upendeleo wowote bali wanataka mshindi halali. Nipe tofauti ya upinzani kisha weka ubora wa ccm ili nione kweli kuna tofauti ya kuwafanya ccm washinde kwa 100%. Tunataka tume huru ya uchaguzi, hizi nyingine zote ni mbwembwe tu, wananchi ndio wataamua wanamtaka nani na sio rais anamtaka nani awe kiongozi.

sasa kama mnajua hamtashinda msanusumbua watu ya nn,? as i said early ccm ina mapungufu lakini kuna mstari haijavuka ambao wapinzai mmevuka. there is no reason to urge here , make politics nzuri then tutawachagua or muunde chama kingine chenye watu wenye akili timam, hata kama mtakua na mapungufu pia tuone haya yanaeleweka

mfano tunaweza sema ccm labda wanakula rushwa ama wanatumia dola, lakini hata ukiachana na hivi ni watu wanaojua kujenga hoja, sasa wapinzani bado hamna iki kitu mpaka tushawishike kweli mna msimamo
 
Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.”

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai
Hahahaaa tumewashika pabaya. Leo mmeanza kuamini ktk majadiliano?? Mangapi tumejafmdiriana mkayapitisha kimabavu??
 
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho.

Anasema Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge. Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.

=========
Leo Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wanamsubiri Zitto awaeleze kwa nini aliandika barua hiyo.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.”

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”

Hata hivyo hapo jana Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Joseph Kakunda alisema kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuandika barua ya kutaka kuzuia mkopo wa elimu unaotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni kituko nani aibu.

Kakunda aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za bajeti na Uwekezaji na Mitaji ya Umma.

“Naomba nizungumze masikitiko yangu dhidi ya barua moja ambayo mwenzetu mmoja (Zitto) ameiandika kutaka kuzuia fedha za miradi ya elimu ni kituko na ni aibu sana kwetu sisi wabunge kuona mwenzetu ameandika barua,” alisema Kakunda ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora

Alisema barua hiyo wangekuwa wameandika watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yeye asingestuka sana lakini kuandikwa na mbunge mwenzao wakati Serikali imepeleka Sh1 bilioni kwa ajili ya kukarabati Sekondari ya Kigoma iliyoko kwenye jimbo lake ni jambo la kusikitisha.

“Sasa hivi Sekondari ya Kigoma ni kama mpya. Na vilevile Serikali imepeleka zaidi ya Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha elimu. Sasa anazuia zisije kwa haraka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kitanzania nieleze masikitiko makubwa sana,”amesema.

“Nilitamani nipaze sauti huko aliko anisikie lakini kwa sababu yuko mbali naachia hapo lakini atasikia kutoka kwenye Hansard (kumbukumbu Rasmi za Bunge)" alisema Mh. Kakunda
Kumuhoji Zitto ni kumuongezea umaarufu zaidi mnatakiwa msome alama za nyakati

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nani angemsikiliza? Sana sana angezomewa na wagonga meza. Kwani ni mikataba mingapi ya hovyo imepitishwa pale bungeni? Wapinzani wakipinga na kutaka maboresho wanazomewa na kutolewa nje. Leo hii supika ndiyo anasema angemsilikiliza Zitto?

Sent using Jamii Forums mobile app
Nimemshangaa sana Ndugai alivyokuwa mnyonge kwa hili. Mbona sioni ule ukali wake?? Hahahhahaaaaa ndugayiiiiii
 
Soma threads zangu za nyuma. Sisimamii upande mmoja. Nasimamia ninachoona ni sahihi na sio lazima nitolee tamko kila kitu kwa uzuri au ubaya wake. Sio lazima.

Kuhusu haki na ukandamizwaji ni same old cry tangu dunia iumbwe. Malalamiko hayajawahi kuisha na hayataisha.

Isitoshe, huu ukandamizaji unaotajwa siku hizi umeegemea zaidi kwa wanasiasa na wanaharakati. Huko uchafu ni mwingi so mnajuana. Msiwagharimu wasiohusika kwenye maslahi yenu.

Sitashiriki.

Hao wanaokandamiza wengine ni wanasiasa, na wanaokandamizwa ni wanasiasa, hivyo kama hao wanaokandamiza wengine wanakaliwa kimya acha hao unaosema hawahusiki wakutane na hiyo hali.
 
Ndugai na wana -CCM wenzake a.k.a Watu wasiyojulikana ni vema waache harakati zao za kupotosha Umma, kama kweli kilichozungumzwa na Mh.Zitto ni uwongo iweje WB wakubaliane naye!? WB siyo mambululaz km wengi wa wana-siasa wa TZ walivyo!
 
Nani angemsikiliza? Sana sana angezomewa na wagonga meza. Kwani ni mikataba mingapi ya hovyo imepitishwa pale bungeni? Wapinzani wakipinga na kutaka maboresho wanazomewa na kutolewa nje. Leo hii supika ndiyo anasema angemsilikiliza Zitto?

Sent using Jamii Forums mobile app

Ndugai ni mnafiki anadhani hatujui kwamba hilo bunge hakuna nafasi ya mpinzani kuhoji jambo lolote la maana. Eti anasema lilikuwa ni jambo la kuzungumza, ni mara ngapi tunaona wapinzani wakidhalilishwa huko bungeni tena wakiwa na hoja za msingi. Zito akaze kamba hapo hapo.
 
sasa kama mnajua hamtashinda msanusumbua watu ya nn,? as i said early ccm ina mapungufu lakini kuna mstari haijavuka ambao wapinzai mmevuka. there is no reason to urge here , make politics nzuri then tutawachagua or muunde chama kingine chenye watu wenye akili timam, hata kama mtakua na mapungufu pia tuone haya yanaeleweka

mfano tunaweza sema ccm labda wanakula rushwa ama wanatumia dola, lakini hata ukiachana na hivi ni watu wanaojua kujenga hoja, sasa wapinzani bado hamna iki kitu mpaka tushawishike kweli mna msimamo

Unaongea utoto gani we dogo? Ccm wanajua kujenga hoja? Unadhani tumekuja hapa nchini juzi nini? Nimekuambia weka ubora wa ccm naona unazungusha tu skirt.
 
Unaongea utoto gani we dogo? Ccm wanajua kujenga hoja? Unadhani tumekuja hapa nchini juzi nini? Nimekuambia weka ubora wa ccm naona unazungusha tu skirt.

si ndo mfano kujenga hoja zenye mashiko , weka ubora sasa wa upinzani
 
Unaongea utoto gani we dogo? Ccm wanajua kujenga hoja? Unadhani tumekuja hapa nchini juzi nini? Nimekuambia weka ubora wa ccm naona unazungusha tu skirt.

na ninakubali kua ccm wana mpungufu , lakini hawajavuka mstari wa aibu kama upinzai, ccm wanajua kujenga hoja ata kama znaupigaji nyuma yake! mfano wanaweza kuomba mkopo wa elimu wakafanya kitu kinahusiana na elimu na bado wakakuonyesha kuna kitu kimefanyika na huo mkopo ingawa wamepiga, rushwa ipo duniani kote hakuna sehem hakuna rushwa

binadam kama binadam tuu wazuri sana kwenye rushwa mfano rushwa hospitali, rushwa ya ngono na rushwa za aina nyingi! ukiachana na mapungufu kama haya upande wa ccm wapo vizuri na chama kimesimama sku zote, aya taja ubora wa upinzani

tukianza na ilo la kuzia mkopo, huo unaitwa upunguani! endelea mengine ...
 
Kupata mimba shuleni ni gross misconduct na adhabu yake ni dismissal ...na sidhani kama Sheria zimebadirika..

kama anaona anataka kuendelea na shule akasome private schools sasa kwa kua ni zinalipiwa na kodi bure kelele ziishe
 
Nani angemsikiliza? Sana sana angezomewa na wagonga meza. Kwani ni mikataba mingapi ya hovyo imepitishwa pale bungeni? Wapinzani wakipinga na kutaka maboresho wanazomewa na kutolewa nje. Leo hii supika ndiyo anasema angemsilikiliza Zitto?

Sent using Jamii Forums mobile app
Angeweza kushika shilingi kukwamisha bajeti ya wizara ya elimu au jinsia na watoto hadi jambo alilo lalamikia World Bank litatuliwe na kanuni au sheria huko bungeni.

Alikuwa na nafasi ya kufanya hivyo yeye au kumuomba mbunge yeyote afanye kwa niaba yake kama yeye hakuwepo bungeni wakati wa kujadili bajeti ya wizara husika.
Zitto alikuwa anajua hili lakini amefanya alichofanya kwa malengo binafsi na ya hatari.
 
Naonelea ugike wakati Zito ulihamshe bungeni kuhusu matumizi ya pesa za bunge.
Posho ifutwe,mshahara upunguzwe.
Yani pajengwe apartment za bunge huko,wabunge wale canten,mpaka pale bunge litakapoisha.
 
Kupata mimba shuleni ni gross misconduct na adhabu yake ni dismissal ...na sidhani kama Sheria zimebadirika..
Sijasema kuwa sheria zimebadilika, lkn pia dismisal ya mmoja haizuwii mwengine kubeba mimba.
 
na ninakubali kua ccm wana mpungufu , lakini hawajavuka mstari wa aibu kama upinzai, ccm wanajua kujenga hoja ata kama znaupigaji nyuma yake! mfano wanaweza kuomba mkopo wa elimu wakafanya kitu kinahusiana na elimu na bado wakakuonyesha kuna kitu kimefanyika na huo mkopo ingawa wamepiga, rushwa ipo duniani kote hakuna sehem hakuna rushwa

binadam kama binadam tuu wazuri sana kwenye rushwa mfano rushwa hospitali, rushwa ya ngono na rushwa za aina nyingi! ukiachana na mapungufu kama haya upande wa ccm wapo vizuri na chama kimesimama sku zote, aya taja ubora wa upinzani

tukianza na ilo la kuzia mkopo, huo unaitwa upunguani! endelea mengine ...

Kapimwe Corona virus.
 
Back
Top Bottom