Zitto Kabwe asubiriwa na Bunge kueleza lengo la barua yake Benki ya Dunia kuzuia mkopo wa kuboresha Elimu (SEQUIP)

"Hii nchi ni tajiri sana ndugu watanzania tutembee vifua mbele" in Magufuli voice
 
Je ni kwa nini Spika na yeye asiandike waraka kwa WB????
 
Ukiona mji wako una shida kubwa sasa kuwahabarisha majirani zako ni kosa?

Nchi yetu tumerithi hii demokrasia ya Mabeberu wa Magharibi lakini inaonekana bado viongozi na wananchi wetu wengi hawajui vizuri majukumu yao kwa nchi yao na Serikali yao. Baada ya uchaguzi mkuu serikali inayoshinda ni Serikali ya wote, walioshinda na walioshindwa. Wenzetu wenye demokrasia yao huwezi kusikia mambo haya ya ajabu ya Mbunge kuandika barua nje ya nchi ili Serikali ishindwe kutekeleza sera yake. Ni jambo la kusikitisha sana na kwa kweli Mhe. Zitto kakosea sana kutumia nembo ya Bunge kwenye barua yake. Sera za vyama hushindanishwa Bungeni na kwenye uchaguzi, siyo kwa kutafuta msaada wa mataifa au mashirika ya nje. Mhe. Zitto kachanganya ubunge na uanaharakati na hili litamtokea puani. Tatizo kama la yule CAG wa zamani aliyekwenda kumwaga shutuma kwa serikali na bunge wakati yuko nje ya nchi. Kuna watu walimuunga mkono na Mhe. Zitto akiwa mmojawapo. Tatizo halikuwa shutuma alizosema lakini ni ule ukiukaji wa maadili ya uongozi wa nchi. Kama kiongozi asiyekuwa mwanasiasa, CAG huyo hakupaswa kusema hayo aliyosema wakati yeye akiwa humohumo serikalini. Huwezi kusikia viongozi wa nchi zenye demokrasia iliyokomaa, wawe kutoka Serikalini au wa upinzani, “wakiimwagia radhi” nchi yao kama ambavyo kina Mhe. Zitto na CAG mstaafu wamefanya, huku Mhe. Zitto akidai kufanya hivyo ni ‘kutetea nchi yake’!! Ni wakati muafaka sasa viongozi wote wa juu wa serikali, bunge na mahakama zetu wawe wanakwenda kupata mafunzo ya kidiplomasia kwenye chuo chetu ili kuepuka makosa haya ya maadili ya uongozi wa nchi.
 
Hili nalo linataka kuongeza tatizo, kwani limemaliza uzinduzi wa Tawi la mikia bungeni!
 
Binafsi hata kama serikali ina madhaifu hakuwa sawa Zitto Kabwe kuandika barua ya namna ile,huku Zitto akijua kabisa hizo fedha zingelisaidia akina nan?Kwanza kihalisi hakuna mtoto wa Bunge anayesoma kwenye hizi hizi shule zetu za serikali ambazo kwa ujumla ndizo mnufaika mkubwa wa fedha hizi.
Kwa matinki hiyo basi Zitto amewakosesha watanzania huduma muhimu katika nyanja ya elimu.Hivyo uzalendo wake uko wapi kwa watanzania au hizo hela Rais Magufuli angelizipeleka nyumbani kwake?Zitto tambua Baba /mama anunuwi nilitamani yaliyompata Lisu yangelikuwa yako kuliko wewe binafsi na mwenye uchu na madaraka.
 
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho.

Anasema Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge. Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.

=========
Leo Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wanamsubiri Zitto awaeleze kwa nini aliandika barua hiyo.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.”

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”

Hata hivyo hapo jana Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Joseph Kakunda alisema kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuandika barua ya kutaka kuzuia mkopo wa elimu unaotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni kituko nani aibu.

Kakunda aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za bajeti na Uwekezaji na Mitaji ya Umma.

“Naomba nizungumze masikitiko yangu dhidi ya barua moja ambayo mwenzetu mmoja (Zitto) ameiandika kutaka kuzuia fedha za miradi ya elimu ni kituko na ni aibu sana kwetu sisi wabunge kuona mwenzetu ameandika barua,” alisema Kakunda ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora

Alisema barua hiyo wangekuwa wameandika watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yeye asingestuka sana lakini kuandikwa na mbunge mwenzao wakati Serikali imepeleka Sh1 bilioni kwa ajili ya kukarabati Sekondari ya Kigoma iliyoko kwenye jimbo lake ni jambo la kusikitisha.

“Sasa hivi Sekondari ya Kigoma ni kama mpya. Na vilevile Serikali imepeleka zaidi ya Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha elimu. Sasa anazuia zisije kwa haraka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kitanzania nieleze masikitiko makubwa sana,”amesema.

“Nilitamani nipaze sauti huko aliko anisikie lakini kwa sababu yuko mbali naachia hapo lakini atasikia kutoka kwenye Hansard (kumbukumbu Rasmi za Bunge)" alisema Mh. Kakunda
Baada ya Tundu Lissu kujeruhiwa kwa risasi 16 na timu aliyoongiza BASHITE, tumebakia na Mwanamume mmoja tu aliyesimama naye ni Zitto Kabwe.

Usiogope Zitto Kabwe Mungu yu pamoja nawe kwa ajili ya kuwakomboa Watanzania. Soma Isaya 41:10
 
1. Tafakuri tafakuri, ni tafakuri jadidi
Fikira zenye urari, siyo tambo za Kabudi
Hili jambo ni dhahiri, kulisema imebidi
Zitto ni mwamba mgumu, Dikteta kaa chonjo

2. Zitto ni mwamba mgumu, Dikteta kaa chonjo
Haliwezi kusalimu, kwa vitisho na manjonjo
Ni jabari lenye sumu, kijikwaa hakuna chanjo
Zitto ni mwamba mgumu, dikteta kaa chonjo.

3. Hupendi haki kwa nini, nakuuliza sizonje?
Mimba zimekosa nini, ghadhabu yako zionje?
 
Wanataka kulifanya suala la kisiasa. Warejee kuangalia tatizo ni nini hasa. Kwa nini wasiwahurumie hata hao watoto wa kike waliopata mimba ambao wanataka kubaguliwa katika mfumo wa elimu kwa fedha ya mkopo ambayo hata wao wataeajibika kuilipa. Wanafsnya kana kwamba wote wamejirakia au wsnajipa hizo mimba wrnyewe!

Suala ni kuwa kulishakuwa na makubaliano ya kisera kuhusu suala hili. Tatizo lilitokea tu pale mtu mmoja alipozuia utekelezaji na kupinga kauli ya waziri. Turejee kujadili ili tupate mwafaka. Lakini kubwa tusiwabague watoto wetu. Tuwape elimu iliyo sawa.
 
Spika wa Bunge Mh. Job Ndugai amesema kama kulikuwa na tatizo la kisera, ni mambo ya kujadiliwa bungeni. Sio mara ya kwanza kutokea sera zikawa na udhaifu au zinahitaji maboresho.

Anasema Zitto alipaswa awasilishe maoni yake na mapendekezo kuhusu ubovu wa sera ya elimu kisha litazamwe. Ndio kazi za bunge. Sasa yeye anaenda kupiga kelele nje ya nchi kwa sababu hakubaliani na sera kweli?

Awajibishwe.

=========
Leo Ijumaa Januari 31, 2020 bungeni jijini Dodoma, Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema wanamsubiri Zitto awaeleze kwa nini aliandika barua hiyo.

“Mtu unaweza kuwa na tofauti na sera au mtazamo kati ya wewe mbunge au upande wa Serikali na kadhalika, lakini kufikia mahali pa ‘kublock’ Tanzania isipate fursa fulani nadhani ni kwenda mbali mno.”

“Kwa sababu watoto watakaokosa fursa hiyo ni watoto wa Tanzania ni walimu wa Tanzania ni miundombinu ya elimu ya Tanzania, sijui katika hilo kama mbunge unanufaika nini maana kama ni suala la utofauti la kisera haya ni mambo ya kujadiliana tu,” amesema Spika Ndugai.

Katika kusisitiza hilo, Spika Ndugai amesema, “ningependa kutoa ushauri wa ujumla tu kwamba ni vema kutumia fursa yetu kama wawakilishi wa wananchi tukaelimishana tukaelezana kuliko kuwakosesha Watanzania fursa wakati baadhi yetu watoto wetu wapo Feza Boys, wapo Marian Girls halafu unablock msaada kwa watoto walio wengi wa wapiga kura wetu jambo ambalo halifai kabisa.”

Hata hivyo hapo jana Waziri wa zamani wa Viwanda na Biashara nchini Tanzania, Joseph Kakunda alisema kitendo cha Mbunge wa Kigoma Mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe kuandika barua ya kutaka kuzuia mkopo wa elimu unaotolewa na Benki ya Dunia (WB) ni kituko nani aibu.

Kakunda aliyasema hayo bungeni jijini Dodoma wakati akichangia taarifa za kamati za Bunge za bajeti na Uwekezaji na Mitaji ya Umma.

“Naomba nizungumze masikitiko yangu dhidi ya barua moja ambayo mwenzetu mmoja (Zitto) ameiandika kutaka kuzuia fedha za miradi ya elimu ni kituko na ni aibu sana kwetu sisi wabunge kuona mwenzetu ameandika barua,” alisema Kakunda ambaye pia ni Mbunge wa Sikonge (CCM) mkoani Tabora

Alisema barua hiyo wangekuwa wameandika watu wa mashirika yasiyo ya kiserikali yeye asingestuka sana lakini kuandikwa na mbunge mwenzao wakati Serikali imepeleka Sh1 bilioni kwa ajili ya kukarabati Sekondari ya Kigoma iliyoko kwenye jimbo lake ni jambo la kusikitisha.

“Sasa hivi Sekondari ya Kigoma ni kama mpya. Na vilevile Serikali imepeleka zaidi ya Sh4 bilioni kwa ajili ya kuboresha elimu. Sasa anazuia zisije kwa haraka kwa ajili ya kuwasaidia watoto wa kitanzania nieleze masikitiko makubwa sana,”amesema.

“Nilitamani nipaze sauti huko aliko anisikie lakini kwa sababu yuko mbali naachia hapo lakini atasikia kutoka kwenye Hansard (kumbukumbu Rasmi za Bunge)" alisema Mh. Kakunda
kati ya wanasiasa ninaowaamini kwenye hii nchi ni Zitto, Mboye, Tundu lissu, Mnyika na Lema...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Binafsi hata kama serikali ina madhaifu hakuwa sawa Zitto Kabwe kuandika barua ya namna ile,huku Zitto akijua kabisa hizo fedha zingelisaidia akina nan?Kwanza kihalisi hakuna mtoto wa Bunge anayesoma kwenye hizi hizi shule zetu za serikali ambazo kwa ujumla ndizo mnufaika mkubwa wa fedha hizi.
Kwa matinki hiyo basi Zitto amewakosesha watanzania huduma muhimu katika nyanja ya elimu.Hivyo uzalendo wake uko wapi kwa watanzania au hizo hela Rais Magufuli angelizipeleka nyumbani kwake?Zitto tambua Baba /mama anunuwi nilitamani yaliyompata Lisu yangelikuwa yako kuliko wewe binafsi na mwenye uchu na madaraka.
Shirikisha ubongo wako kwanza kabla hujakurupuka kumpinga Zitto. Nenda kasome vizuri Sera ya Elimu iliyoandikwa mwaka 2014 uone inasema nini juu ya watoto wanaopata mimba shuleni.

Pili huu ni mkopo wa Benki ya Dunia, ina maana kila Mtanzania atalipa kupitia kodi yake inayokusanywa na Serikali. Sasa kwa nini umbague kwenye fedha inayokopwa kwa ajili ya elimu yake?
Tatu, unapombagua huyu aliyepata mimba shuleni ni hatua gani unayoichukua dhidi ya aliyempa mimba? Ni hatua gani una chukua dhidi ya yule aliyefanya ngono ila hakubeba mimba?

Wengine wanashangilia tu matamko ya Jiwe wakati wao wenyewe ni mama zao waliwazaa wakiwa shule na mama hao wakaendelea kusoma mpaka kuhitimu na kisha kuwasomesha watoto wao ambao ni Mawaziri wa sasa kama Ndalichako.
 
Interest,
Ndugai ameacha kuwa spika wa bunge la wananchi badala yake amekuwa mtetez wa central gvt

Too pathetic fella
 
Wao kila siku wanajimbwambafai kwamba wana fedha nyingi ,sasa wanalia lia nini?
 
Back
Top Bottom