Zitto Kabwe atoa hoja nzito juu ya uwekezaji wa DP World Tanzania

Tulilijua hili... atafuatia Lipumba kisha sheikh Kishki!! Tunajua mpambano umehamia misikitini!
 
kwanini serikali inataka kuingia mkataba na kampuni yenye tuhuma kwenye nchi mbalimbali ilizowai kufanya kazi za bandari?
DP World ni kampuni kubwa sana na inawashindani wengi sana, inafanya kazi na zaidi na ya nchi 60, ni kawaida kuwa shutuma na shutuma sio tuhuma. Hebu onesha kesi moja tu, ambayo DP World ilishindwa na kutozwa faini. Kampuni kubwa na shutuma sio kigezo cha kutofanya biashara, sio jambo baya, ni kawaida, hata wewe kesho unaweza kupewa shutuma, ila haina maana una makosa, ni shutuma tu.
 
Zitto huyu huyu anayetaka tusiwaguse Wazanzibar kwenye jambo ili tusionekane Wabaguzi ? Wadanganye Wajinga sana .
 
Kama kawaida ya watanzania hakuna wasichokijua, Kkla kitu wanajua. Unaeza mkuta mtu anashabikia kuwa katiba ibadilishwe (of course ni kweli) lakin ukimuuliza kuhusu katiba iliyopo hajui kifungu chochote, watu wanatumia hisia badala la logic, Mtu kaleta Mada badala ya watu kutoa hoja, wanatoa kashfa. Yaan watanzania ni wepesi wa kukosoa sana lakini hawawezi toa njia mbadala. Sijui ni Ujuaji ulokithiri, uvivu kutafuta maarifa au mtu asionekane yuko nyuma.

Ni rahisi Tanzania mtu kupinga kitu, kama tu yeye hakifahamu bila kujitathimin kuwa yapo mengi hayafahamu na anapaswa kujifunza.

Kama Taifa tunasafari ndefu ya kwenda.


Ni vyema kujibu hoja kwa hoja.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…