Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Tatizo lako la ufahamu ni kubwa kuliko! Wewe unadhani nimeomba watu wa Kigoma wajitambulishe? Kwa nini unajitambulisha hapa?
 
Hili ni suala la public interest, ikiwa kuna haja uhamiaji watalizungumzia
Muhimu hapa ni 'public interest' hasa kwa nafasi yake.
Ni kazi ya uhamiaji kuchunguza na kutoa majibu. Mengine ni siasa tu.
 
Ni kweli unalosema

Tatizo ni kwamba hili ni suala la public interest. Kubwa zaidi ni pale ambapo limeingiza ukabila kwamba kwa kuwa ni wa Kigoma basi kuhoji suala hilo si sahihi.

Ninaseam hivi kwa vile ana passport ya Tanzania huyo ni Mtanzania.

Hoja iliyopo ni kuwa je , ni raia wa kuzaliwa au wa kupewa?

Akiwa VP wakati wowote anaweza kuwa Rais, sasa kama ni Raia wa kupewa tutaishia kuwa na mgogoro wa kikatiba. Hapa ndipo ima yeye au vyombo husika viweke wazi kuhusu uraia wake
 
Unauliza majibu ndugu yangu, labda nikutajie na kijiji alichozaliwa ukawatembelee wakuinyeshe kwao na ndugu zake.


Na wewe ni Mrundi, umejuaje hadi kijiji anachotoka??!!
 
Tatizo lako la ufahamu ni kubwa kuliko! Wewe unadhani nimeomba watu wa Kigoma wajitambulishe? Kwa nini unajitambulisha hapa?


Wewe akili yako ni kubwa kama jiwe, huijui Kigoma na watu wanaoishi huko, hivyo kwa huruma na upendo wangu kwako nikaona ni muhimu upate darsa ili usirejee makosa tena.
 
Na wewe ni Mrundi, umejuaje hadi kijiji anachotoka??!!
Hapana mimi sio mrundi, nilienda Burundi, wenyeji kule wakafunguka. Warundi wanatushangaa sana kuwa tunawapa mpaka Urais watu wa kwao.
 
Wewe akili yako ni kubwa kama jiwe, huijui Kigoma na watu wanaoishi huko, hivyo kwa huruma na upendo wangu kwako nikaona ni muhimu upate darsa ili usirejee makosa tena.
Nimekuuliza hujajibu. Nimeomba ujitambulishe kwamba wewe unatoka kigoma? Nani aliomba ujitambulishe?
 
Mkuu nashukuru kwamba kuna watu wanaoelewa hoja yangu

Mpango alikuwa senior minister na passport ya Tanzania tena ya kidiploamasi! Ni Raia hadi hapo

Tunachohoji ni je, uraia wake ni wa kuzaliwa au kupewa?
Hili si tatizo kwa mtu wa kawaida, ni tatizo kwa VP ambaye anytime anakuwa Rais wa JMT

Ikiwa hana uraia wa kuzaliwa basi nafasi hiyo ina matatizo kwasababu likitokea lisilotarajiwa tutakuwa na mgogoro wa kikatiba. Kumbuka wakati huo

Trump na wafuasi wake walimwandama Obama kwa hoja kwamba si Raia wa kuzaliwa . Jambo hilo lingemuondolea sifa ya kuwa Rais.
Rais Obama aligundua ni jambo lenye public interest na akaruhusu nyaraka zake zote z kuzaliwa, Hopsitali na magazeti ziwekwe wazi

Kwa hili la Mpango, utetezi hauwezi kuwa eti ni kwasababu ni mtu kutoka Kigoma.
Hii ni hoja isiyo na mashiko kwasababu hakuna anayehoji kabila lake, wanaohoji nature ya uraia wake

Kadiri watu wanavyokuwa mbogo ndivyo hofu inaongezeka na bila Mpango kusafisha hali watu watamtazama si kama VP bali Mrundi aliyevamia na hana uhalali. Hatutaki hilo, ajitokeze na kuondoa shaka.
 
Unasema Dkt. Mpango ni raia. Halafu bado unamtaka athibitishe kuwa yeye ni raia?

Sijaelewa.

Ni raia au si raia?

Kama ni raia [kama ulivyosema wewe], athibitishe nini tena?
Yes ni Raia wa Tanzania. Dr Mpango anamiliki passport ya Tanzania inayompa uraia

Hoja si kama ni Raia au la. Hoja ni nature ya uraia wake
Je, ni raia wa kuzaliwa ?
Je, ni raia wa kufikia au kupewa?

Hapo ndipo panahitajika ufafanunuzi kwa kuzingatia ni VP na anaweza kuwa President at anytime
 
Akiwa VP wakati wowote anaweza kuwa Rais, sasa kama ni Raia wa kupewa tutaishia kuwa na mgogoro wa kikatiba. Hapa ndipo ima yeye au vyombo husika viweke wazi kuhusu uraia wake
Unajuaje kama vyombo husika havikujilisha kwamba ni Mtanzania halali bila chenga kabla hajautwaa huo uVP?

Kitu hakiwi “public interest” baada tu ya watu flani huko Twitter kuanza kuhoji uraia baada ya kuona akicheza wimbo wa Kiha.
 


Uhamiaji ipi?
Wewe unajua aliwahi kamatwa Mkurugenzi wa uhamiaji ambae sio raia??Alikuwa Mmalawi na akashitakiwa mahakamani...

Uhamiaji wangekuwa makini basi Warundi wengi wanaouza machungwa dar wangekamatwa
 
Kwa hili la Mpango, utetezi hauwezi kuwa eti ni kwasababu ni mtu kutoka Kigoma.


Mtu kutoka Kigoma ndiye Mwana Kigoma kwa maneno mengine, sasa Mwana Kigoma siyo raia wa Tz ???--- isitoshe yeye ni Muha kwa kabila, Waha ni Wenyeji wa asili ya Kigoma, Waha hawana asili ya Burundi,Kongo au Rwanda, Kagera, Katavi, Tabora wala Shinyanga na ukimuona Muha nje ya Kigoma basi huyo alitoka Kigoma kama si yeye basi ni wazazi wake au hata mababu zake.

Wakoloni waliweka mipaka ya majimbo kulingana na makabila ya asili ya mahali hapo, Jimbo la magharibi wakati wa Ukoloni lilibeba mikoa ya Kagera (wahaya nk), Kigoma (Waha nk), Tabora (Wanyamwezi nk).
 
Unajuaje kama vyombo husika havikujilisha kwamba ni Mtanzania halali bila chenga kabla hajautwaa huo uVP?

Kitu hakiwi “public interest” baada tu ya watu flani huko Twitter kuanza kuhoji uraia baada ya kuona akicheza wimbo wa Kiha.
Kule Zanzibar yalitokea makubwa ndani ya Ofisi ya Rais kwa kuwa na raia wa kigeni hasa.
Vyombo husika vilikuwepo

Kama una uhakika na vyombo husika, iweje wahoji uraia wa Askofu ambaye alithibitika kuwa Raia?
Vyombo husika vilipoteza maana wakati wa utawala uliopita ambapo vilitumika hovyo kuadhibu watu

Jambo lolote huanza sehemu fulani. Aliyewashtua Zanzibar kuwa ndani ya Ofisi ya Rais kuna raia wa kigeni ni mitandao iliyoweka wazi nyaka za mhusika

Hatuna sababu ya kuhoji Uraia wake, tunasababu za kuhoji aina ya uraia wake! hapo ndipo hoja ilipo

Na kwavile tayari kuna kila sababu zinazotia shaka, ni kwa public interest na interest yake kusafisha hali ya hewa

Nadhani anapaswa kuitwa Vice president Dr Philip Mpango.
Bila kusafisha hali ataiwa Mrundi Dr Mpango na hilo litamsononesha sana na kumfanya dhalili bila sababu

Yeye ni raia, kuna tabu gani kueleza nature ya uraia wake? Kwanini Ukigoma unatumika badala ya majibu halisi
 
Weakness ya Kigogo ni hapendi mtu aende against his views.
 
Wanaohoji uraia wake hawahoji kabila, dini, kijiji au mtaa alipotoka

Wanakubali kuwa ni Raia wa Tanzania kwasababu hadi sasa anamiliki passport ya Tanzania. Ni raia

Hoja iliyopo ambayo wengi hawataki kukabiliana nayo ni hii
Je, ni raia wa kuzaliwa ndani ya ardhi ya Tanzania?
Je, ni raia aliyepewa uraia na kuwa raia wa Tanzania?

Haya ndiyo yanatakiwa kujibiwa na yana public interest kwasababu ni VP

Akiwa VP halafu akaitwa VP mrundi siku tutakapomhitaji kwa dharura yoyote kutakuwa na tatizo
Itabidi athibitishe uraia wake atake asitake. Kabla ya kufika huko Dr Mpango ana nafasi ya ku clear air.

Watu waelezwe nature ya uraia wake! si kumtetea kwa ukigoma! hapana!
 
Ifike mahali hii nchi tuwe na viongozi wanaotokea Zanzibar mana ndio watanzania halisi isije ikawa hawa wanao tokea huu ukanda wamepandikizwa na aliyetangulia ,


Sent using Jamii Forums mobile app
Zanzibar ni kisiwa ambacho wakazi wake wana asili ya nchi za Oman, Yemen, UAE, Tanganyika, Malawi, Uganda na nyingine nyingi. Iweje viongozi wa Tanzania watoke huko wakati Tanganyika pia ina mkusanyiko wa wabantu, wahameti,na waniloti, wazulu? .... kuna kundi la wanasiasa wenye wivu wa kisiasa, tusiwaruhusu kuigawa nchi.
 
Hizo “sababu zinazotia shaka” ni zipi mkuu? Ni kwa sababu anatokea Kigoma? Ni kwasababu ule wimbo wa Kiha kwa mbaali una rafudhi ya Kirundi!?😅

Anapaswa kusafisha hali gani? Hakuna hoja. Wanaozusha basi waje na credible evidence. Otherwise hii ni wivu wa kike tu
 
Tatizo hawa watutsi wanaamini nchi yao ni Rwanda hata kama wanajulikana kama watanzania.

Ni bora umkubali muhindi,Msomali au Mwarabu mzawa kuliko hawa watutsi.Wanafanya mambo mengi ya upendeleo wa kikabila na kwenda kujenga kwao Rwanda
Hivi kwanini Watusi wa Tanzania huwa wanaonekana sio raia ukilinganisha na Wahutu au Waha wa kirundi?

Wote hawa si victims wa mipaka ya mzungu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…