Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Zitto Kabwe awa mbogo, awashukia vikali wanaodai Makamu wa Rais, Dkt. Mpango ni Mrundi

Ila hizi propaganda kwamba Dr. Mpango ni Mrundi kwa kuwa tu ameonekana akicheza wimbo wa kiha ni utoto na kukosa hoja.

Kigogo sometimes anakuwa na mambo ya kipuuzi sana. These days yupo off target kwa kila jambo na frustrations zake zinamfunua na kuonyesha ni mtu wa aina gani
Kweli kabisa

Umakamu wa rais umemuuma sana, hili jambo halina mantiki kabisa. Kama kuna mtu anashida na uraia, alete ushahidi. Sio ngoma au mavazi.
 
Kumbe homeboy ni homeboy tu. Kiongozi wa ACT-Wazalendo amefura na amekuwa kama mbogo. Hii ni baada ya video iliyosambaa mitandoni ikimuonyesha Makamu wa Rais wa sasa akicheza ngoma inayofanana na ya Kirundi.

View attachment 1742127
Mwambie zitto asifoke kiasi hicho.
Pia mwambie ruksa kwenda kuchukua kadi pale CCM
 
Akiwa VP hili ni muhimu sana ! umeelewa


Umuhimu wake ni upi???

Sana sana inaleta matabaka (classes) ya uraia, kwamba raia wa class fulani hatakiwi kupata haki na wadhifa fulani na fulani no matter how brilliant he is to serve the country!!, huu ni aina fulani ya ubaguzi wa ukabila unaoshadidishwa na Wapuuzi na Wajinga wachache, Dr J k Nyerere alipata kusema; "sumu ya ukabila ni mbaya sana ukishaanza kuinywa itakutafuna tu na haiishii hapo tu--"-"

Nami nasema sumu ya ukabila wa Dr Mpango haitaishia hapo itawatafuna wengi sana. Na wameanza kuuliza Samia naye ni Muomani kwani ndugu zake wengi ni raia wa huko.

Mpango ni Muha halisi, kuna tofauti kati ya Muha na Muhutu.
 
Kauli kama hizo ndizo zinatia shaka sana

Hoja ni moja, je uraia wake ni wa kuzaliwa au wa kupewa?

Kadri watu anavyopandisha povu na kukimbia hoja ndivyo shaka ilipo

Kuna umuhimu wa kuhoji hili. Ni Raia wa Tanzania, je uraia wake upoje kama VP?
Kwanza una fahamu sheria ipi ina regulate mambo ya uhamiaji hapa Tanzania???? Umeshaipitia ukaifaham vizuri au kupitia tu key provision zake. Mambo mengi nchini yanaendeshwa kisiasa tu. Yaani kama VP akijibu hii hoja, atakua amenikosea san maana anawapa nguvu watu mitandaoni. Mwisho wa siku hii nchi itakua inaendeshwa na watu mitandaoni. Mimi nachoona tuwaachie uhamiaji wafanye kazi yao tu, kama wakiona kuna haja watamuoji.
 
Anasubiri mtu atweet “tuhuma” then apate hoja. Kuna ujinga mwingi sana huko Twitter these days. Mtu anajipostia uzushi tu then activists wanapick na kuanza kupropagate

Na wengine eti ni wanasheria. Elimu bila kuelimika!
Halafu, hivi wanaopost huko Twitter nao ni Watanzania? Wasije wakawa Wamanga wa Oman na Wanyasa wa Malawi.

Kila mtu ahojiwe uraia wake....

So stupid!

Hawakuhoji kote huko alikowahi kutumikia.
 
Hivi hii issue kwanini ni kwa watu wa Kigoma sana?
Kwa sisi wengine tuliobahatika kutembea mikoa ya pembezoni mwa Tanzania hasa ukizingatia desturi na hulka ya watanzania kwa majirani kumekuwa na mwingiliano mkubwa wa jamii na koo mbalimbali.
Nenda kule Kilimanjaro,Nenda Mbeya,Nenda Mara ,Nenda Mtwara ,Nenda Tanga ,Nenda Arusha ,Nenda Katavi na hata Kagera ni jambo la kawaida koo moja kuwa na nasaba pande zote mbili .

Sasa kwanini kwa upande wa Kigoma inakuwa ni “Issue” kuna agenda gani ya siri ?
 
Kumbe homeboy ni homeboy tu. Kiongozi wa ACT-Wazalendo amefura na amekuwa kama mbogo. Hii ni baada ya video iliyosambaa mitandoni ikimuonyesha Makamu wa Rais wa sasa akicheza ngoma inayofanana na ya Kirundi.

View attachment 1742127
The whole issue started with this person
Screenshot_20210403-224056.png
 
Kigogo angekuwa known ingependeza zaidi ili awe liable anapothibitika kumchafua mtu, lakini kujificha kwa fake ID halafu unaropoka ropoka sio fair, Dr. Mpango himself alishasema yeye ni Muha, Kigogo kwa kujaribu ku prove wrong kaweka video Dr. Mpango akicheza ngoma ya "kirundi" na anaowaita ni "warundi", hili peke yake kwangu halitoshi kuthibitisha bila shaka kwamba Dr. Mpango ni Mrundi, kwani kwa kawaida maeneo ya mipakani mara nyingi tamaduni zao hufanana kati ya nchi moja na nyingine, mbaya zaidi Kigogo nae anatumia taarifa za mtu mwingine kutoa hizo shutuma ambapo mtu huyo nae anatumia fake ID.

Kwani kuna tatizo kwa yeye mwenyewe Dr Philip Isdor Nzebayannga Mpango kutoka hadharani na ku prove uhalali wa Uraia wake?

Katiba inatambua aina tatu za Uraia. Lakini ili mtu awe kiongozi ktk serikali hususani ktk nafasi ya Urais, VP na PM ni sharti awe raia by natural birth i.e wazazi wake wote lazima wawe Watanzania by birth...

Hii ndiyo status ya uraia wa Dr Mpango?
Screenshot_20210403-224056.png
 
Acha niachangie kdg na mm siku alvyo tangazwa kuwa Ni yey ndie makamu wa rais mawazo yangu yaliamia burund tu bila kujuA na alivyo anza kuhutubia bunge ndio akanichanganya kabsa
Mosi nilishangaa Sana mpngo huyu kuamishwa amishwa shule za msingi na sekondar ovyo na kuhama eneo moja kwenda jingine na kurudi Tena palepale pa mwazo .. cajelewa kulikuwa na adha gani hadi kufanya hvyo ...mtoto wa mkulima anaamaje aamje hovyo

Mfno alisema alisoma darasa la Kwanza na kuamishwa tabora na kusoma darasa la. Pili na kurudi tena kgoma kuendelea na darasa la tatu

Aidha alisema hata sekondar alisoma Mara kigoma Mara tabora madarasa togauti tofauti ...cjamuelea kbsa mm hapo

Ingawa nisema tabora Ni sehemu ambayo ktk nnch hii watu wengi Ni wanatoka kigoma kunzia urambo hadi uyuhi watu wakigoma Ni wengi snaa humo na warundi pia Ni wengi snaa. Ktk maashamba Yale ya. Tumbaku what is so special there .

Lingine linalotia doa urai wake Ni pale alivyo chukuwa likozo ya sabatical leave kwenda marekano bank ya dunia Kama mchumi mwaandamizi hapo pia kuna


Mwisho nisema Tu kuwa kigogo anasumbua mbna hakuona hili. Mtu kawa Hadi naibu katibu mkuu wa ps na pia mkuu wa tra makao makuu pale ilala
Sas najiuliza mbma hakushtukiwa muda wote huo
 
Huyo huwa anapenda udini na ukabila. Yupo vizuri huko
Lisemwalo lipo kama halipo laja.Zitto kujiunga na CCM Jumanne hii.Sababu VP ni wa kwao.Hawa akina Zitto ndio wanafiki namba moja.
 
Kwanza una fahamu sherehe ipi ina regulate mambo ya uhamiaji hapa Tanzania???? Umeshaipitia ukaifaham vizuri au kupitia tu key provision zake. Mambo mengi nchini yanaendshwa kisiasa tu. Yaani kama VP akijibu hii hoja, atakua amenikosea san maana anawapa nguvu watu mitandaoni. Mwisho wa siku hii nchi itakua inaendeshwa na watu mitandaoni. Mimi nachona tuwaachie uhamiaji wafanye kazi yao tu, kama wakiona kuna haja watamuoji.
Mbona hujibu hoja yangu kwa kutumia '' key provision' unazosema ambazo pengine sizijui!

Uhamiaji walipoteza credibility baada ya kutumika katika mambo hovyo hata ya Abdul Nondo
Yaani uhamiaji walitumia rasilimali kuchunguza uraia wa Nondo , hawa wana credibility gani?

Muhimu , Dr Mpango aeleze yeye au kupitia uhamiaji au popote kuhusu aina ya uraia wake kama VP
Hili halikwepeki kwasababu hadi sasa hivi hakuna anayeweza kueleza ni raia wa kuzaliwa au kupewa
 
Umuhimu wake ni upi???

Sana sana inaleta matabaka (classes) ya uraia, kwamba raia wa class fulani hatakiwi kupata haki na wadhifa fulani na fulani no matter how brilliant he is to serve the country!!, huu ni aina fulani ya ubaguzi wa ukabila unaoshadidishwa na Wapuuzi na Wajinga wachache, Dr J k Nyerere alipata kusema; "sumu ya ukabila ni mbaya sana ukishaanza kuinywa itakutafuna tu na haiishii hapo tu--"-"
Katiba imeanisha aina ya uraia na ikatoa mashrti kwa viongozi yakiambatana na uraia wao

Nimesema mara nyingi sana katika bandiko hili, kwa mtu wa kawaida hili si tatizo
Kwa VP ni tatizo kwasababu huyu anaweza kuwa Rais
Katiba inasemaje kuhusu Uraia wa Rais wa Tanznia? Hapo ndipo hamtaki kwenda mnajificha kwa vioja na si hoja

Kuna shaka kubwa kila dakika kwamba uraia wa Dr Mpango una walakini, hivyo lazima kuwepo na taarifa ima kutoka kwakwe au popote zikithibitisha aina ya Uraia wake. Hapa narudia aina ndiyo key word.
Nami nasema sumu ya ukabila wa Dr Mpango haitaishia hapo itawatafuna wengi sana. Na wameanza kuuliza Samia naye ni Muomani kwani ndugu zake wengi ni raia wa huko.

Mpango ni Muha halisi, kuna tofauti kati ya Muha na Muhutu.
Hakuna ukabila, walioleta ukabila ni wale wanaosema Ukigoma ndio tatizo

Wengine sisi tunasema, hapa, si tatizo Dr Mpango ana passport ya Tanzania ni Raia
Je, uraia wake ni wa kuzaliwa ? Je, ni wa kupewa?
Mbona ni swali rahisi tu !

Bila kujua aina ya Uraia wake, basi wale wanaosema tofauti watapata uhalali hata kama si kweli.
 
Hakuna hoja. Hatuwezi kupoteza muda kupropagate uzushi kwa kuwa kuna mtu mmoja katweet (below)

Wewe unayesema eti kuna habari huyu ni Mrundi nani kakwambia? Umbea na uzushi tu bila evidence.

Hii tweet eti ndio chanzo chenu cha habari. Are we serious?

Heshima yako mkuu.

SIKUJUA KAMA NAWE UNAPENDA USHADADU WA VIHOJA.
Hapana ! wala si hivyo

Dr Mpango ni Raia wa Tanzania.
Je, uraia wake ni wa kuzaliwa au ni wa kupewa? Kwanini watu hawajibu hili tukamaliza ?

Kuna mtu alisemwa na Raia wa kigeni, watu wakabisha . Uchunguzi ukabaini ni kiongozi zanzibar na ni Raia wa kigeni. Si uhamiaji wala chombo chochote kile kilichobaini. Ni udaku tu

Hata kuugua kwa Magufuli ni udaku tu mwisho ikawa kweli. Kifo chake kilisemwa ni udaku tu anachapa kazi.

RC Mbeya akasema ameongea naye leo unajua alikuwa mahututi
PM akasema Raia anachapa kazi kumbe alikuwa mahututi
 
Watu wa mikoa ya pembezoni huwa wananyanyapaliwa sana kwa kubambikiwa uraia wa nchi jirani.

Zitto yuko sahihi kukasirika
Tatizo letu hasa upinzani ni kuchafuana. Mtu yeyote mwenye kujuwa historia ya TZ pamoja na makabila yake anatakiwa kujuwa kuwa watu wa mipakana wana makabila yanayoshahibiana. Waha kwa kifupi wana uhusiano na Warundi. Nafikiri siku hizi hata historia ya makabila hatujifunzi. Wale tuliyokuwa shule miaka ya 1950 tulijifunza juu ya makabila na asili zao. Ndiyo maana ukinitajia Mwami Ntare ninajuwa ni nani na alitawala wapi. Sasa hivi watu wanasikia Wahutu na Watusi, wakidhani hayo ni makabila kumbe siyo. Hata Waha, Wanyamwezi, na Wasukuma wana wahutu wao na watusi wao.

Hao wanamuita Mpango Mrundi ni CHADEMA waliokosa sera wamebaki kuchafuana. Hata kama angekuwa Mrundi, kwani Warundi wangapi wamechukuwa utaia wa TZ kutokana na migogoro yao. Je, akiwa na asili ya Kirundi lakimi ni Mtanzania utamnyima hiyo nafasi kwa sababu asili yake ni Burundi. TZ haibagui wananchi wao kwa dini, kabila, wala asili yao. Ukishakuwa Mtanzania ni Mtanzania tu, hata kama wewe ni mzungu. Hivi mliwa kuwaona mawaziri wa Nyerere ambapo kulikuwa na wazungu, waafrika, na wahindi. Hivi leo hii ikitokea hivyo, kelele za CHADEMA zitafika wapi? Au watanyamaza kwa sababu huko Ulaya ndipo alipo prpogandist wao mkubwa anti-pus Lissu.
 
Back
Top Bottom