Kuna pande mbili za suala hili
1. Upande wa kwanza umeonyesha hata kwa jina la 'Dr..' ambalo linaonekana kuwa la Burundi
2. Upande wa Pili ni ule unaotumia Ukigoma kama kinga ya kutohojiwa
Ikumbukwe, Uraia una maeneo mawili, kwanza wa kuzaliwa na pili wa kufikia au kupewa
Dr Mpango ni Raia wa Tanzania iwe alizaliwa au alipewa, hilo halina mjadala
Pamoja na yote , Dr Mpango ana wajibu wa kueleza nature ya Uraia wake ili kuondoa mashaka kwamba hana uraia wa kuzaliwa au kupewa. Bila kufanya hivyo itakuwa ni halali kusema Dr Mpango si Raia
Hivyo basi Dr Mpango anapaswa ajitokeze kama kiongozi wa umma kuthibitisha aina ya Uraia wake.
Haitoshi kusema katoka Kigoma basi ni Raia, inatakiwa kwenda mbali zaidi ya hapo.
Abdul Nondo ambae sote tunajua ni kijana au mtoto alituhumiwa si Raia.
Tulijua ni uongo lakini Nondo alikwenda mbali na kuonyesha Babu yake alimpokea Nyerere, hilo tu lilimaliza ubishi kuwa kwavyovyote iwavyo wazazi wa Abdul wamezaliwa Tanzania na yeye pia na ni raia wa kuzaliwa na mjadala ulifungwa daima milele
Dr Mpango ajitokeze kama Askofu aliyetuhumiwa na ambaye alitoa uthibitisho wake.
Hii system iliundwa na akina Mpango wakiwa Baraza la Mawaziri la Magufuli kwa chuki, dhulma na ukatili
Wazungu wanasema '' Chicken are coming home to roost''
Dr Mpango anawajibika kuondoa shaka kwa vithibitisho vinginevyo hoja kwamba si Raia inamuondolewa nguvu ya kutumikia Taifa , inamuondolewa uadilifu na itia mashaka kama kweli ni Mtanzania anayepaswa kupewa dhamana na usalama wa Taifa letu.
JokaKuu Mag3 tindo The Boss Zitto