Zitto Kabwe: Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2019

Zitto Kabwe: Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2019

Hivyo vitabu vyote Zitto vina page ngap ngap? mbona kama uko speed hivyo?

unavikumbuka vyote kweli? tuseme wakati umemaliza hiki chamwisho,kile chakwanza

unakumbuka hata kilihusu nini? uko race vibaya mno,sasa na wananchi unawatumikia saa ngapi?
Navikumbuka sana. Vile ambavyo vinavutia sana huwa narudia na kurudia. Ni kujipanga tu ndugu yangu. Kuna mwaka nilisoma zaidi ya hivi. Siku hizi uzee umeingia na majukumu pia mengi
 
Nadhani unajisemesha tu. Tumefanya kazi kubwa sana kuliko wakati wowote katika MANISPAA ya Kigoma Ujiji, I am proud of our work
Manispaa ujiji iko nyuma Sana kielimu Angalia matokeo ya shule za msingi na sekondari kipindi chako cha ubunge
 
Mm nikupongeze tu mh mbunge pamoja na majukumu ya kitaifa unatenga muda kulisha ubongo wako.

Tupe mbinu na ss tufanye nn tuweze kupenda kusoma vitabu au wewe ulianzaje kipenda kijisomea vitabu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hongera sana Kaka Zito Kabwe. Vijana wajifunze na kujizoesha kusoma vitabu. Sio kushinda kwenye pooltable na Draft. Mwaka huu nmesoma Vitabu viwili. Hakika kitabu ni mbolea ya Ubongo.

Kikubwa naona jiandae Uandike Kitabu kwa mkono wako. Achana na kile alichoandika Dada Asha kukuhusu. Natamani kusoma kitabu chako. Mungu akufanyie wepesi uweze kuandika

Najitahidi ndugu yangu
 
Kuna audio books mkuu, vitabu vya kusikiliza.
Hivyo vitabu vyote Zitto vina page ngap ngap? mbona kama uko speed hivyo?

unavikumbuka vyote kweli? tuseme wakati umemaliza hiki chamwisho,kile chakwanza

unakumbuka hata kilihusu nini? uko race vibaya mno,sasa na wananchi unawatumikia saa ngapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nadhani unajisemesha tu. Tumefanya kazi kubwa sana kuliko wakati wowote katika MANISPAA ya Kigoma Ujiji, I am proud of our work
Mkuu, wewe unajua zaidi kuliko mimi kuhusiana na hawa watu.

Baadhi ya watu wamekuwa wakikulaumu hujibu maswali humu jukwaani, binafsi nlishawahi kukushauri Bora huo upupu wanaouliza usiwe unajibu maana ni kheri nusu Sharif kuliko Sharif kamili.

Yapo maswali of course yanastahili kujibiwa, ila hebu angalia hiyo hoja ya yehodaya hapo juu uliyomjibu. Hata usingemjibu tungekuelewa tu
 
Mheshimiwa hongera sana! Labda kwa kuwa umekiri ulishindwa kusoma vitabu vingi zaidi kutokana na muda. Hata tuliowengi changamoto za muda ndio zinatukabili; kazi, familia, na masuala ya kijamii. Lakini nitajitahidi labda angalau nipate muda usiku na jumapili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Suala hilo mbona ndio kazi kubwa ya ACT Wazalendo. Ni kazi endelevu
Kwanza mkuu Zitto nikushukuru leo kwa kujibu hoja ya msingi humu kwa sababu kwa uzoefu kidogo nilio nao mara nyingi hujibu hoja ispokuwa pale unapochafuliwa ndio hujibu kujisafisha. Hata hapa nilitaraji kwamba angalau kwa 90% usingejibu ila naona angalau umejibu; ni jambo zuri.

Sasa turudi kwenye hoja yangu, kwanza nikupongeze kwa kukubali umuhimu vya vyama vya siasa kuendeleza rasilimali watu hasa kwenye leadrship skills.

Pili tukubaliane kwamba hata kama jambo hilo linafanyika huko ACT ni kwa kiwango kidogo mno ambacho kinasikitisha.

Mkuu Zitto wewe ni msomi ambaye ni rahisi sana kuelewa vitu. Sasa hivi kupitia mitandao ya kijamii tu, inaweza kusaidia kuleta mafanikio makubwa sana kwenye mambo mbalimbali au janga kubwa sana. Wewe kama kiongozi mkuu wa ACT, unatakiwa kujiuliza, maswali yafuatayo.

1. Ni kwa vipi unaweza kutumia maendeleo ya teknolojia kukifanya chama chenu kuwa cha kisasa (unatakiwa kuelewa kwa sasa ACT reputation yake iko chini sana)na hakuna kitu cha maana wanachoonekana kufanya Zaidi ya kukimbizana na matukio, na hili limekuwa ni tatizo kongwe sana.

2. Ni kwa vipi mnaweza kutengeneza chama kinachosimamia misingi na sio blaa blaa kama sasa (wakati hicho chama kinaanshiwa watu walikuwa na imani nacho sana ila sasa ndio hivyo tena)Ni kosa kubwa sana chama cha siasa kujishikiza kwa reputation ya mtu badala ya watu kujishikiza kwenye reputation ya chama.

3. Hicho chama ni kama wewe ndio chama na chama ndio wewe, hilo ni tatizo kubwa.

4. Hakuna namna mnaweza kuendeleza rasilimali watu kama hamna katibu mkuu ambaye ametulia akili na ana upeo mpana na 'ultitude' ya kuutazama ulimwengu kwa jicho la tofauti.

5. Delegate madaraka ili wengine wajifunze.

6. Acheni kujazana fikra za kwamba kazi yenu ni kuitoa ccm madarakani, mtakuwa hamna la kujifunza na kujifanyia self improvement na baadae mtapotea kabisa, (na hasa hili linahusu Zaidi wengine, wewe hili halikuhusu maana kama uwakujifunza ushapitia mengi)

7. Jifunzeni na kuwafunza viongozi na wanachama wenu kwamba hatima ya upinzani wa Tanzania ipo mikononi mwao wenyewe na sio CCM. Vinginevyo hakuna improvement itakayofanyika. na mwisho kwa leo;-

8.Eleweni kuwa tatizo la demokrasia Tanzania msingi wake ni tatizo la kijamii, kwa hiyo ili kulitatua 'focus' ni jamii na sio 'CCM' na suala hilo linahitaji muda mrefu. Vinginevyo ni sawa na kujenga ghorofa juu ya puto.

Nimeandika mengi lakini kwa kuwa unasoma vitabu, naamini haya ni machache sana kwako kusoma.Mengine yanaweza kukukera ila siku moja yanaweza kusaidia mahali.

Ijumaa njema,
 
Zitto ni 'mashine 'sasa Kama kasoma vitabu 34 kwa mwaka! Hapo unaweza kukuta kasoma magazeti 5000 kwa mwaka! ni nzuri sana
 
Kuna kitabu cha yerricko nyerere cha UJASUSI wa kidola na kiuchumi, Fanya nacho ukisome ni kizuri
 
Mkuu Zitto tunakushauri Kama walivyotangulia wenzangu uwe distinguished na wengine kwakuwa socially. Utakubaliana na Mimi kuwa hata kwa simu yako Ni kazi Sana kukupata especially kwa usiyemjua.

Although ni political life ila ungepunguza hii kadhia. Pia topic Kama hii ungetafuta siku unanafasi useme leo utazungumza na Wana JF ili kila anaye comment umjibu tuone faraja yako usiwe Kama Mnyika
 
Mkuu Zitto vipi huvutiwi na vitabu vya Falsafa? Naona kidogo kwenye List yako havipo, tuseme unavutiwa. Je, ni vitabu gani vya falsafa ungependa vijana wajikite katika kuvisoma?
 
Back
Top Bottom