Zitto Kabwe: Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2019

Zitto Kabwe: Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2019

Zitto,

Christine Berry + Joe Guinan - People Get Ready: Preparing for a Corbyn Government

ABOUT THE BOOK
Jeremy Corbyn’s Labour stands on the brink of power, promising a fundamental re-ordering of British politics. But what, in practice, will this entail? How can a radical government stand up to an establishment that is hostile to any significant redistribution of wealth and power? People Get Ready! dives into the nitty gritty of what’s needed to bring about transformative change.

Unlike a decade ago, the left’s problem is no longer a shortage of big ideas. Inside and outside the Labour Party, an agenda for new forms of public and community ownership is taking shape. Today the biggest danger facing the left is lack of preparedness—the absence of strategies that can make these ideas a reality.

People Get Ready! draws on previous attempts at radical change, from the election of Labour at the end of the Second World War and the progressive early days of Mitterrand’s presidency in France, to Tony Benn’s battles with Harold Wilson and Margaret Thatcher’s icy insistence that there was no alternative to free markets. These stories highlight the importance of knowing your allies and, even more, your enemies, of being ready to deal with sabotage and resistance from the highest levels, of being bold enough to transform the structures of government, and of having a mass movement that can both support the leadership and hold it to its radical programme when the going gets tough.

Remarkably, democratic socialism in Britain is closer to government than in any other European country. The responsibilities this brings for those supporting the Corbyn project are as great as the opportunities it presents. But there isn’t much time to get ready …
_________________________________________________________________________________

Hiki kitabu natamani nikipate na kukisoma hasa ikizingatia dhahama chama cha Corbyn (Labour) iliyokumbana nayo katika uchaguzi mkuu wa Uingereza uliofanyika 12/12/2019. Nitatamani kusoma mistari yote na kati ya mistari ya hiki kitabu ili nijue alau mchango wa machapisho kama hili ulivyochangia SUNAMI iliyokikumba chama cha Labour.

Hongera Mkuu Zitto kwa kutupatia hamasa ya kujisomea vitabu na machapisho mengine ili kujiongezea ufahamu wa mambo mbalimbali.

Ahsante
 
Wengine lugha inawakwamisha.

Nimewahi kwenda Tabora kikazi nikakutana na bwana mdogo yupo kidato cha 4 anasoma sana vitabu, na nikabaini yule mtoto anatumia mpaka pesa yake kununua vitabu.

Nilishangazwa sana! Umri wake plus na nature ya maisha aliyokua nayo - yalikua duni.

Ila sikumuona na kitabu cha kiingereza hata kimoja. Nikaja kubaini bwana mdogo lugha ni tatizo pia. Katika vitu daima nitamchukia Nyerere ni suala la mabadiliko ya ovyo kabisa ya lugha ya kufundishia anayokutaja nayo kijana wa kitanzania...kutoka kwenye circle ya Kiswahili ghafla anakua introduced kwenye lugha ya kigeni asiyoifahamu vema. Hii inawaumiza sana vijana wetu. By the way heko mheshimiwa Zitto.
 
Nimejiona mjinga sana, nina muda lakini nashindwa kusoma vitabu, sijui shetani huyu kanikamatia wapi, nilipo kuwa mdogo nilikuwa nasoma sana vitabu. Mwaka ujao nataka angalau nisome kitabu 1 kwa mwezi.

Sent from my SM-P585 using Tapatalk
 
Ila inawezekana maana anapokea zaidi ya milioni 10 kila mwezi huku anayemlipa anamzuia kufanya mikutano kwahiyo pesa yote anayoliwa anapiga mfukoni
Anayemlipa ni mimi, wewe na wananchi wengine huyo anayemzuia kufanya mikutano muda mwingine huwa nahisi anajikuta yeye ndo kila kitu kwenye maisha ya Watanzania jambo ambalo sio kweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hivyo vitabu vyote Zitto vina page ngap ngap? mbona kama uko speed hivyo?

unavikumbuka vyote kweli? tuseme wakati umemaliza hiki chamwisho,kile chakwanza

unakumbuka hata kilihusu nini? uko race vibaya mno,sasa na wananchi unawatumikia saa ngapi?
Acha Kutoa Boko Kila Muda, Kama Huna Desturi Ya Kusoma Vitabu. Ni Kawaida Sana Na Huwezi Kusahau Kitu Unachokipenda

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi mwaka wa tatu sasa bado nasoma kitabu kimoja....No easy Walk to Freedom by Nelson Mandela....
japo sijamaliza kukisoma but nimejifunza mambo mengi sana......
mojawapo watu hutoka mbali sana.....
real struggle huwadefine watu....
Oliva Tambo na Nelson Mandele....
laleni pema peponi.....
 
Habari zenu wakuu.

Mimi ni msomaji mzuri wa vitu hasa nonfiction book. Mwaka huu nimesoma vitabu vingi ila hii ni list ya vitabu vitano ambavyo nimevielewa sana.

1. The subtle art of not giving a https://jamii.app/JFUserGuide-Mark Mason

2. 12 rules for life- Jordan Peterson

3.The law of human nature -Robert Green

4. Imotionl Intelligence-Daniel Coleman

5. The way of the superior man-David deida.

Sent using my 6x6 bed.
 

Attachments

  • download.jpeg
    download.jpeg
    9.8 KB · Views: 4
  • download (2).png
    download (2).png
    8 KB · Views: 4
  • download.png
    download.png
    8.5 KB · Views: 4
  • download (2).jpeg
    download (2).jpeg
    7.9 KB · Views: 4
  • download (1).jpeg
    download (1).jpeg
    12.7 KB · Views: 4
Sawa umesoma.. umejifunza nini?
Habari zenu wakuu.
Mimi ni msomaji mzuri wa vitu hasa nonfiction book.
Mwaka huu nimesoma vitabu vingi ila hii ni list ya vitabu vitano ambavyo nimevielewa sana.
1.The subtle art of not giving a ****-Mark Mason

2.12 rules for life- Jordan Peterson

3.The law of human nature -Robert Green

4.Imotionl Intelligence-Daniel Coleman

5.The way of the superior man-David deida.



Sent using my 6x6 bed.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
List yangu ya vitabu ambavyo nimesoma mwaka 2019!

1. Animal farm by George Orwel

2. Art of War

3. Becoming by Michele Obama

4. Capitalist Nigger by Chika Onyeani

5. Criminal Psychology

6. Millionare success Habits by Dean Graziosi

7. Skin in the Game by Nassim

8. The rules of Work by Richard Templar

9. How to win an Election by Quintus Tullius Cicero

10. Permanent Record by Snowden

11. can, I must, I will - Dr. Reginald Abraham Mengi

12. A secret history - Donna Tartty

13.A set back is a setup for come back - Willie Jolley

14. Goals -Brian Tracy

15. How to win friends and influence people - Dale Carnegi

16. Truth Matters -Dr. Walter J. Veith

17. Start your own Business

18. Build a band in 30day

19. Bitter Haverst-Ian Smith

20. One menute Manager-Kenneth & Spancer Johnson

21. Life of Muhammad

22. Tanzania Industrialization Journey 2016-2056 -Ali Mufuruki and Others

23. The leader who had no title-Robin Sharma

24. Shake hands with a Devil-Romeo Dallaire

25. Parenting With Love And Logic-Foster Cline

26. The Purpose-Driven° Life-Rick Warren

27. Reflections Of A Man -Amari Soul

28. The Richest man Who ever lived-Scott

29. He came to set the captive free.Rebecca Brown

30. How the Mighty fall-Jim Collins

31. Lean Impact-ANN MEI CHANG

32. Unleash the Warrior within-Richard Machowiczp

Nawatakia sikukuu njema za mwisho wa mwaka! Mungu awabariki sana
 
Baadhi ya Vitabu nilivyosoma mwaka 2019 – Zitto Kabwe

Mwaka 2019 nimejaaliwa kusoma vitabu 34 (2018:49 na 2017:36+3). Ni sahihi kuwa idadi imepungua sana, hii ni kwa sababu shughuli nazo zimekuwa nyingi, haswa masuala ya ujenzi wa chama na kuhami demokrasia. Mwaka 2019 ndio mwaka nimekanyaga mahakamani mara nyingi zaidi kuliko wakati wowote wa maisha yangu. Majukumu yanapozidi, muda wa kujisomea unapungua. Hata hivyo nashukuru sana nimejikongoja mpaka kufikia vitabu 34.

Ingizo jipya ni riwaya za mwandishi wa Kituruki Orhan Pamuk ambaye nimesoma vitabu vyake 4 mwaka huu. Amenifanya kupenda kusoma kazi za waandishi wengine kutoka Uturuki kutokana na riwaya zake zenye mchanyato wa masuala ya Siasa za Uturuki, utamaduni, mapenzi na maisha ya watu kiujumla. A Strangeness in Mind ndio ilinivutia kuliko zote katika Riwaya za Pamuk nilizoorodhesha hapa. Hii ni riwaya inayoeleza maisha ya kijana Mevlut aliyetoka shamba na kuhamia mjini na namna maisha yalivyobadilika kwa kasi. Ni hadithi inayoonyesha tamaduni za kituruki kuhusu ndoa na mahusiano ya ndugu na familia. Kitabu hiki kitakufanya uione Uturuki na mapinduzi ya kijeshi yalivyoigubika mwaka hadi mwaka, pamoja na mtanziko wa Siasa zenye kuheshimu misingi ya Dini au kufuata umagharibi. Riwaya za Pamuk nilizosoma ni pamoja na;

1. Orhan Pamuk - Snow

2. Orhan Pamuk - Silent House

3. Orhan Pamuk - A Strangeness in Mind

4. Orhan Pamuk - Instanbull

Nilisoma pia Riwaya nyengine kadhaa zikiwemo kazi za watunzi mliozoea kuwaona kama Jefrey Archer na John Grisham katika orodha zangu za miaka ya hivi karibuni. Pia nilimsoma Mzee Makaidi, kazi yake aliyoandika mingi nyuma. Mwaka huu nimevutiwa sana na kazi za mtunzi wa kitanzania anayechipukia Bwana Lello Mmasy. Riwaya na Mimi na Rais ilinikosesha usingizi kwani sikutamani kuacha kuisoma. Ni Riwaya iliyosadifiwa vizuri na kwa ubunifu mkubwa huku ikichora picha halisi yenye kuvutia msomaji.

Riwaya hii naifananisha na ile ya A Man of The People ya Chinua Achebe (kwa ubunifu na labda utabiri). Nchi ya Stanza na Rais wake Bwana Costa aliyekuwa anaharibu Uchumi wa Taifa lake, katika riwaya hii, inaweza kuwa ni nchi yeyote ya Afrika katika hali ya sasa.

Nilifurahi pia kusoma kazi ya Mama Fatma Jinja iitwayo The Shirazi Enigma kwani ni hadithi yenye historia kubwa ya Zanzibar. Ukitaka kujua usasa na uchangamano wa watu wa mataifa mengi Zanzibar soma hadithi ya Salwa katika Riwaya hii. Bwana Abdulrazak Gurnah pia anasimulia hadithi katika historia ya Zanzibar pia. Kazi yake niliyoorodhesha hapa ni historia ya Siasa na familia za Zanzibar katika miaka ya Sabini na Themanini. Mtunzi wa Riwaya Helmut Zell kutoka Ujerumani pia alinivutia kazi yake ya Black Money in Dar. Ukisoma Riwaya hiyo unakumbuka mtifuano wa sakata la Escrow mwaka 2014. Kama kwa Mmasy, nilijisoma pia kwa Zell. Riwaya nilizosoma ni pamoja na;

5. Jeffrey Archer - Nothing Ventured

6. Abdulrazak Gurnah - Gravel Heart

7. Fatma Jinja - The Shirazi Enigma

8. E J E Makaidi - The Serpent: Hearted Politician

9. Helmut Zell - Black Money in Dar es Salaam

10. Lello Mmassy - Mimi na Rais

11. Jeniffer M Makumbi - Kintu

12. John Grisham - The Guardians

Kama kawaida, napenda historia. Hivyo mwaka huu nilisoma vitabu vya historia kadhaa ili kupata maarifa ya tulipotoka ili niweze kutafakari huko tunakokwenda. Vitabu vya historia nilivyosoma ni pamoja na;

13. W H Ingrams - Zanzibar: Its History and Its People

14. Judith Listowel - The Making of Tanganyika

15. Linda Pappas Funsch - Oman Reborn: Balancing Tradition and Modernisation

16. A Monument to China - Africa Friendship: Firsthand Account of the Building of The TAZARA

17. Amilcar Cabral - Unity and Struggle

18. Paul Kenyon - Dictatorland

19. Yuval Noah Harari - Sapiens: A Brief History of Humankind

Mwaka huu tumebahatika kupata vitabu vya baadhi ya Viongozi wetu nchini. Rais wa Awamu ya Tatu Mzee Benjamin Mkapa ameandika Wasifu wake. Amesimulia maisha yake. Kabla ya hapo Mzee Njelu Kasaka, aliyekuwa Mbunge na Katibu wa Kundi la G55 lililotaka Serikali ya Tanganyika alitoa kitabu chake pia. Vitabu muhimu sana katika kuifahamu Tanzania ilipotoka na ilipo kupitia maisha ya wanasiasa hawa. Nimefurahi sana kusoma vitabu vyao. Pamoja nao pia nilisoma vitabu vya watu wengine kama vile Hashil Seif ambaye alishiriki mapinduzi ya Zanzibar.

Kitabu cha Balozi Wilibrod Slaa kinaeleza maisha yake na pia nini kilitokea katika chama cha CHADEMA mwaka 2015. Sio kitabu cha kupuuza kwani kina mafunzo mengi kwa wanasiasa. Nasikitika kuwa Balozi Slaa alichagua ya kutoandika kwani labda kupitia kwake ningeweza kujua haswa ushiriki wake katika kufukuzwa kwangu kwenye chama ambacho yeye alikuwa Katibu Mkuu. Nilikinunua ili nisome suala hilo, bahati mbaya hakusimulia mkasa ule wa Zitto na Kitila.

A Son of Two Countries cha Casmir Rubagumya ni wasifu wa Mtanzania mwenye asili ya Rwanda ambaye aliishi maisha ya ukimbizi na wazazi wake, kusoma mpaka kuwa Mhadhiri wa Chuo Kikuu na hatimaye kustaafu. Alipata uraia wa kuandikisha na kuitumikia Tanzania kwa weledi wake wote. Licha ya kubembelezwa kurudi Rwanda baada ya mauaji ya kimbari, aligoma na kuendelea kuwa Mtanzania tofauti na wenzake wengi wa aina yake ambao waliamua kurudi Rwanda. Ni simulizi ya maisha yenye kusisimua na mafunzo. Ni Kitabu kimojawapo ambacho nilipokishika sikukiacha mpaka namaliza. Wasifu na Tawasifu nilizosoma ni pamoja na;

20. Benjamin W Mkapa - My Life, My Purpose

21. Njelu Kasaka - Maisha, Siasa and Hoja ya Tanganyika: G55

22. Hashil Seif Hashil - Mimi, Umma Party na Mapinduzi ya Zanzibar

23. Willibrod P Slaa - Nyuma ya Pazia: CHADEMA ilivyosalitiwa 2015

24. Casmir M Rubagumya - A Son of Two Countries

25. Sergey Plekhanov - Sultan Qaboos Bin Said A Said: A Reformer on the Throne

26. Ken Saro-Wiwa - A Month and a Day: A Detention Diary

Mchanganyiko wa vitabu mbalimbali kama kawaida. Ni katika kuongeza maarifa au kurutubisha itikadi ya Ujamaa. Pia katika kujifunza makosa ya wengine ili kutorudia makossa hayo. Vitabu mchanganyiko mwaka huu ni pamoja na;

27. James Brent Styan - The Bosasa Billions

28. Christine Berry + Joe Guinan - People Get Ready: Preparing for a Corbyn Government

29. P. Anyang’ Nyong’o - Presidential or Parliamentary Democracy in Kenya?

30. Greg Mills et al - Democracy works

31. Nick Robinson et al - The Power of Journalists

32. Douglas Rogers - Two Weeks in November: The Astonishing Inside Story of the Operation that Toppled Mugabe

33. Nanjala Nyabola - Digital Democracy, Analogue Politics

Zawadi kubwa niliyopata mwaka huu ni kitabu kinachoeleza Aya za Qur’an Tukufu na muktadha wa kila Aya katika kushuka kwake. Ni kitabu kinachokaa pembeni ya Kitanda changu kwa ajili ya marejeo ya mara kwa mara. Wanazuoni wa mirengo yote ya Dini ya Kiislam wameshiriki katika kuandika ‘comentaries’ za kitabu hiki.

34. Sayyed Hossein Nasir - The Study Quran

Mwaka huu ninatangaza kitabu changu cha Mwaka, yaani Kitabu kilichonivutia zaidi kuliko vyote nilivyosoma mwaka huu. Kitabu changu cha Mwaka 2019 ni Two Weeks in November cha Bwana Douglas Rogers. Kitabu hiki kinaeleza namna Watu mbalimbali waliokuwa maadui na marafiki, waliokuwa wakiviziana kuuana na wapinzani wakubwa, walivyoshirikiana kumwondoa madarakani Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe mwezi Novemba mwaka 2017.

Ni kitabu cha matukio ya kweli ambayo huwezi dhania ni kweli, unaweza kudhani ni hadithi tu. Licha ya kwamba kuondolewa kwa Mugabe madarakani hakujaleta ahueni kwa wananchi wa Zimbabwe, mbinu, mikakati na mafunzo ndani ya Kitabu hiki ni somo tosha kwa wapigania demokrasia kote Afrika. Hiki ni kitabu ambacho utakirudia hata mara 10 bila kuchoka.

Kila Rais wa Afrika, kila Mkuu wa Majeshi, kila Kiongozi wa Upinzani na kila mwanasiasa mwenye kujitambua asome kitabu hiki. Akifanye rejea yake ya mara kwa mara. Wiki 2 za Novemba 2017 zaweza kutokea katika nchi yeyote ambayo Viongozi wake hawazingatii demokrasia, utawala wa sheria, Utu na mshikamano katika kuendesha Taifa. Tafuta nakala yako.

Nawatakia kheri katika kumaliza mwaka 2019 na kila la kheri katika mwaka 2020. Nawashawishi kupata muda wa kujisomea japo kitabu kimoja kila mwezi. Kusoma ni kurutubisha ubongo.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Dar es Salaam
Disemba 20, 2019
Mkuu mbona umesahau vitabu vyangu?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom