Zitto Kabwe: Hadi sasa wafuasi 13 wa ACT-Wazalendo wamepoteza maisha kwa vurugu za uchaguzi

Zitto Kabwe: Hadi sasa wafuasi 13 wa ACT-Wazalendo wamepoteza maisha kwa vurugu za uchaguzi

Quinine

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2010
Posts
22,227
Reaction score
49,628
Kwa upande wetu @ACTwazalendo na kutokana na Taarifa tulizokusanya mpaka sasa: Wananchi 13 wameuawa kwa kupigwa risasi na mabomu katika maeneo mbalimbali ya Zanzibar, Watu 130 Wamejeruhiwa, Watu 120 Wamekamatwa na Polisi, mtu Mmoja Amebakwa na Watu 14 Wametekwa Akiwemo Naibu Katibu Mkuu wa Chama Nassor Mazrui. -: Zitto Kabwe.

"Kati ya watu waliouawa mwanamke ni mmoja na wanaume ni 12. Mkubwa zaidi kati ya hawa waliouawa ni ndugu Chumu Kombo Saidi, mwenye umri wa miaka 45. Wanne kati ya waliouawa ni vijana chini ya miaka 20." @zittokabwe.

"Unyama zaidi umefanyika kwa wanawake, nitatoa ushuhuda wa matukio machache kwa sababu ya muda. Makamu Mwenyekiti wa Vijana Taifa, Khadija Anuar, alikamatwa Pemba Oktoba 27, akapigwa mno, kisha akaachiwa. Akakamatwa tena Oktoba 29, akapigwa zaidi na kuachiwa." @zittokabwe

"Watu 68 hata sasa wana majeraha ya vipigo vya nyaya za umeme, marungu, magongo, shoka na fimbo za Polisi." @zittokabwe.

"Tumeziomba Jumuiya za Kikanda na Kimataifa kutokutoa ushirikiano kwa Serikali zote mbili, za Muungano na ile ya Zanzibar, kwa sababu hazina uhalali." @zittokabwe

"Tumeandika Barua kwa Taasisi zinahusika na Masuala ya Haki za Binaadam kuwajulisha Madhila ambayo tunapitia na kuomba washirikiane nasi katika kulinda uhai wa watu wetu na kudai haki zetu.Taasisi hizo ni Amnesty International, Human Rights Watch pamoja na ICC." @zittokabwe

### Jambo la kusikitisha wakati haya yakitolea tayari kuna wabunge wa upinzani wanakimbilia bungeni kusaini posho, hawajali hata kutoa pole kwa wahanga####AIBU.
 
Halafu wanasema uchaguzi umemalizika kwa amani, na hao wanafiki viongozi wa dini eti wakaandaa kongamano kumshukuru Mungu uchaguzi kumalizika kwa amani! Amani wakati watu wamekufa.
 
Halafu wanasema uchaguzi umemalizika kwa amani,na hao wanafiki viongozi wa dini eti wakaandaa kongamano kumshukuru Mungu uchaguzi kumalizika kwa amani!Amani wakati watu wamekufa,pumbav kabisa!
Hakuna kiongozi wa dini apo wote ni freemasonry.
 
Marais waliotangazwa katika hotuba zao baada kiapo si wa Bara wala visiwani alitamka neno pole na faraja wahanga uchanguzi,Mbali ya pongezi nyingi kwa NEC,ZEC na ccm!
 
Acheni kuwalumu Wabunge kwenda kujiandikisha.

Mwaka 2015 aliuwawa Alphonce Mawazo lakini Wabunge wa Upinzani walienda Bungeni.
Tunaangalia msimamo wa chama na sio msimamo wa mtu, aliyejipeka bungeni akihitaji msaada wa chama atapata wapi au atakwenda kwa Polepole.
 
Sioni sababu ya kujadili mtu mmoja aliyepatikana kwa muujiza wa kuwatoa wasiowataka huyo mwacheni atimize azma ya waliomteua sisi tuelekeze mashambulizi kudai Katiba mpya na Tume huru ya uchaguzi.
 
Tunaangalia msimamo wa chama na sio msimamo wa mtu, aliyejipeka bungeni akihitaji msaada wa chama atapata wapi au atakwenda kwa Polepole.

Anajivua tu anakuwa CCM anagombea Tena na anapata

Then chama kinakuwa kimepata faida gani?

Au Ndugai anaamua tu kumtambua kama wakina Mwambe
 
Anajivua tu anakuwa ccm anagombea Tena na anapata

Then chama kinakuwa kimepata faida gani?

Au ndugai anaamua tu kumtambua kama wakina mwambe
Ni bora chama kukosa ruzuku kuliko kufuga msaliti mmoja ndani ya chama anayetoa siri.
 
Halafu wanasema uchaguzi umemalizika kwa amani, na hao wanafiki viongozi wa dini eti wakaandaa kongamano kumshukuru Mungu uchaguzi kumalizika kwa amani!Amani wakati watu wamekufa.
Una ushahidi?
 
Acheni kuwalumu Wabunge kwenda kujiandikisha.

Mwaka 2015 aliuwawa Alphonce Mawazo lakini Wabunge wa Upinzani walienda Bungeni.
Yeye anaona wabunge wanakimbilia posho kwa sababu hajapata ubunge mara ngapi alitofautiana na wenzake kimsimamo kisa apate uenyekiti wa kamati ya a bunge.
 
Ni bora chama kukosa ruzuku kuliko kufuga msaliti mmoja ndani ya chama anayetoa siri.
Halafu kinaishije?
Mbona unaongea kama mtu ambae unashabikia kitu ambacho hukijui?

Ukiambiwa toa ela uchangie chama utatoa?

Mwisho wa siku mtawakosa watu wote muhimu kwenye chama just because mnataka kushindana na Serikali Tena serikali yenyewe ya JPM
 
Alafu kinaishije?

Mtu anayejiunga chama kwa ajili ya ruzuku hafai.
 
Utawala wa dhuruma ni mgumu mno, atacheka machoni, lkn atalia moyoni katika miaka miatno yote!!!
 
Halafu wanasema uchaguzi umemalizika kwa amani, na hao wanafiki viongozi wa dini eti wakaandaa kongamano kumshukuru Mungu uchaguzi kumalizika kwa amani! Amani wakati watu wamekufa.
Unamuamini saana Zitto!

Hujiulizi, kwa nini alizuia ela za kuja kusomesha watoto wetu wakati wa kwake hawajulikani wapo "International skuli ipi" Bahati nzuri serikali ikafanikiwa kuzipata!
 
Back
Top Bottom