Zitto Kabwe: Haikubaliki , Haivumiliki na Haitakubalika Watu kuendelea Kupotea/Kutekwa na Kuuawa!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Zitto Kabwe amesema Haikubaliki Haivumiliki na Haitakubalika Watu kuendelea Kupotea Kutekwa na Kuuawa

Jukumu la msingi la Dola lolote Duniani ni Kulinda Uhai wa Watu wake

Hakuna Taifa Bila Watu

Zitto Kabwe amehuzunika ukurasani X Baada ya taarifa za msaidizi wa Mnyika
Nafikiri kuna haja Kinana,Nape na January wakamatwe,haya mambo huwa yanakuwepo wakiwa tu hawapo kwenye uongozi....Mama Samia chukua huu ushauri na uufanyie kazi...Zitto kama mpambe wao hapa anatumika kuchochea mambo
 
Nadhani na mtoto wake Abdul naye akamatwe. CDM na ACT Wazalendo wajiunge na kumgomea huyu mama. Inakera sana.
 
Nafikiri kuna haja Kinana,Nape na January wakamatwe,haya mambo huwa yanakuwepo wakiwa tu hawapo kwenye uongozi....Mama Samia chukua huu ushauri na uufanyie kazi...Zitto kama mpambe wao hapa anatumika kuchochea mambo
Watakamatwa bila sababu, lazima wawe connected. Lakin hata hivyo situpilii mbali huenda kuwa yanafanyika ili kumuondolea credibility kwenye jamii
 
Mnafiki mkubwa huyu
Unafiki wake upo wapi? Kuweni na hekima. Zito amezungumza kauli ya msingi kabisa, halafu wewe unakuja na kauli za kipuuzi.

Tuheshimu, tulinde na kuthamini uhai wa wenzetu kama ulivyo wa kwetu.

Hata kama watu watatofautiana katika itikadi lakini linapokuja suala la uhai wa binadamu, ni lazima tuangana, kuyaacha mashetani mauaji pekee yao, na ndiyo yageuke kuwa maadui yetu sote.

Tunataka kusikia kauli ya Rais Samia, maana yeye alisema kuwa watu hawatekwi, atuambie marehemu alitekwa au alijiteka?
 
Utekaji ni njia zilizoshindwa awamu iliyopita sijui kwanini tena watu wameamua kurudi kule kule tulipotoka
Shetani hawezi kuacha uovu. Kwake uovu ndiyo imani yake. Utekaji na uuaji ni uovu. CCM ni shetani. Huu uovu hautaisha mpaka siku CCM itakapoondolewa na kufutika kabisa, na wana wa nchi kuamua kuotengeneza nchi upya kwa namna itakayoupa utu thamani.
 
Unafiki wake upo wapi? Kuweni na hekima. Zito amezungumza kauli ya msingi kabisa, halafu wewe unakuja na kauli za kipuuzi.

Tuheshimu, tulinde na kuthamini uhai wa wenzetu kama ulivyo wa kwetu.

Hata kama watu watatofautiana katika itikadi lakini linapokuja suala la uhai wa binadamu, ni lazima tuangana, kuyaacha mashetani mauaji pekee yao, na ndiyo yageuke kuwa maadui yetu sote.

Tunataka kusikia kauli ya Rais Samia, maana yeye alisema kuwa watu hawatekwi, atuambie marehemu alitekwa au alijiteka?
Kuna siku utaelewa unafiki wa Zitto..

NB; napinga mauaji bila kujali yanafanywa na nani.
 
Back
Top Bottom