Pre GE2025 Zitto Kabwe kugombea Urais wa Tanzania 2025, Jimbo la Ubunge Kigoma mjini anawaachia Vijana wa ACT Wazalendo

Pre GE2025 Zitto Kabwe kugombea Urais wa Tanzania 2025, Jimbo la Ubunge Kigoma mjini anawaachia Vijana wa ACT Wazalendo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
KC Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekubali ombi la mh Ismail Jussa wa Zanzibar aliyemtaka agombee Urais wa JMT 2025 badala ya kurejea bungeni kama ilivyopangwa

Zitto Kabwe amekubaliana na ombi hilo na kusema Sasa yuko tayari kuwa Rais wa JMT mnamo Uchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba Ubunge anawaachia Vijana kutoka Ngome ya ACT Wazalendo

Source: Mwananchi

My take; Lisu sasa arudi NCCR tu
Atapata kura za Mwandiga na Chakechake
 
CHADEMA nayo ina tofauti gani na ACT kwenye mchakato wa kumpata mgombea urais kama sasa hivi Mbowe na Lissu wanataka kushikana mashati?
Na safari hii vita ni Kali Mbowe hataki Lisu agombee ,Lisu anataka kugombea uraisi
 
Bora agombee ili tupunguze kelele za kinafiki. Maana tangu yupo CHADEMA anataka Urais.

Chama chake hakina huo ubavu. Tuliona jinsi Membe alivyopata shida kukampeni. Anapoteza muda tu, ajikite kwenye ubunge tu. Otherwise, anajimaliza kisiasa.
 
wameweza kujijenga kitaasisi na hivyo wako tayari kuchukua mamlaka ya Nchi Zanzibar na Tanzania bara k
Bara ACT haina kitu , ni mfu tu. Visiwani ni nguzo ya Maalim Seif na si ACT as ACT. Kuna siku wataanzsha chama lao ku reflect majina nan imani za wazazibari
 
Bara ACT haina kitu , ni mfu tu. Visiwani ni nguzo ya Maalim Seif na si ACT as ACT. Kuna siku wataanzsha chama lao ku reflect majina nan imani za wazazibari
ACT Kwa Hilo wako vizuri wamepiga hesabu vizuri sana.Bara ACT wazalendo Ina Waislamu wengi na wazazibari wengi wanaofanya shughuli zao Tanzania Bara ambao ni wanachama wa ACT wazalendo na Jamii zao

Zanzibar Hana shida atapata kura nyingi sana kuliko chama chochote Cha upinzani
Wazazibari hawana mtu wa awezaye Pata kura upande wa Tanzania Bara ndio maana wamempa yeye
 
Zitto acha utani!
Jielekeze kwenye ubunge kumbuka hata umaarufu huo huna tena ulishapotea muda mrefu!
 
Bara ACT wazalendo Ina Waislamu wengi na wazazibari wengi wanaofanya shughuli zao Tanzania Bara ambao ni wanachama wa ACT wazalendo na Jamii zao
waislamu wamegawanyika ccm chadema, act...........
 
Zito akagombee urais wa MWANDIGA atapita Kwa kishindo
 
Kampeni zao huwa za ajabu sana, wanatembelea makao makuu ya mikoa tu na zile wilaya zinazopitiwa na barabara kuu inatosha, wanaishia kupata kura chache. Walau chadema wanaweza kuvuna kura nyingi nyuma ya ccm. Act bado sana, labda kwa zanzibar hasa pemba
Kila kitu kina mwanzo, hata kwenye uchaguzi wa kwanza wa vyama vingi 1995 Chadema haikusimamisha mgombea urais na imesimamisha wagombea ubunge kwenye baadhi ya majimbo tu.
Haikufika nchi nzima.
Kazi ya chama cha siasa ni kufanya siasa, kama huwezi kufanya siasa kwenye eneo kubwa fanya kwenye eneo dogo.
 
waislamu wamegawanyika ccm chadema, act...........
Chadema Waislamu wa kumulika na torch wachache mno ndio maana hata maandamano ya chadema Dar es salaam yalianzia wilaya zote za Dar kasoro temeke kwenye Waislamu wengi Dar Walijua Temeke hawatapata watu

Lakini ingekuwa CCM au ACT wazalendo wangekuwa kibao
 
Chadema Waislamu wa kumulika na torch wachache mno ndio maana hata maandamano ya chadema Dar es salaam yalianzia wilaya zote za Dar kasoro temeke kwenye Waislamu wengi Dar Walijua Temeke hawatapata watu

Lakini ingekuwa CCM au ACT wazalendo wangekuwa kibao
Acha udini ndugu.
Vyama vyote ni mali ya watanzania bila kujali dini wala makabila yao.
Ulitumia chombo gani kufanya utafiti kupata idadi ya dini za wanachama wa Chadema?
Chadema hawaamini kwenye dini yoyote, usiwaharibie mbele ya jamii
 
KC Mstaafu wa ACT Wazalendo Zitto Kabwe amekubali ombi la Mh. Ismail Jussa wa Zanzibar aliyemtaka agombee Urais wa JMT 2025 badala ya kurejea bungeni kama ilivyopangwa.

Zitto Kabwe amekubaliana na ombi hilo na kusema Sasa yuko tayari kuwa Rais wa JMT mnamo Uchaguzi mkuu wa 2025 na kwamba Ubunge anawaachia Vijana kutoka Ngome ya ACT Wazalendo.

My take; Lissu sasa arudi NCCR tu.

=====

Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Zanzibar, Ismail Jussa Ladhu amesema kuwa wao kama Chama katika miaka yao 10 kama Chama chenye usajili wa kudumu, wameweza kujijenga kitaasisi na hivyo wako tayari kuchukua mamlaka ya Nchi Zanzibar na Tanzania bara kwa kumsimamisha Kiongozi wao Mstaafu wa Chama Zitto Kabwe kuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Jussa ameyasema hayo jana katika sherehe za kitaifa za maadhimisho ya miaka 10 ya ACT yaliyofanyika mkoani Kigoma ambapo amebainisha kuwa Zitto anayo nafasi kubwa ya kukivusha chama hicho na kuchukua uongozi wa Nchi.

“Tunajua Mnamtaka Zitto kuwa Mbunge wenu hapa mjini kwenye uchaguzi ujao lakini sisi kama chama tunataka atuvushe kwenye nafasi ya uraisi wa Tanzania kutokana na uwezo na nafasi aliyonayo na tunaomba mtoe baraka zenu kufanikisha hilo” — Jussa.

Kwa upaande wake kiongozi wa Chama Mstaafu, Zitto Kabwe amesema kuwa “Niko tayari na nimejianda kimaarifa na kusaikolojia kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na wakati wowote mkinihitaji niko tayari, kuhusu ubunge hakuna shida wakina Nondo wapo na Vijana wengine wakati wowote tupo tayari kuleta mabadiliko ya ya Nchi yetu, mimi ni mstaafu napokea amri kutoka nyie Viongozi wangu”.

Zitto kabwe mbali na hayo amesema miaka 10 ya kuanzishwa kwa Chama hicho inatosha kukifanya kuwa Chama kikubwa Nchini na cha Watu hivyo mpango wa miaka 10 ijayo ni mkakati wa kuhakikisha Chama kinashika dola.

Kuhusu mpango wa Chama kumtaka kugombea Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa 2025, Zitto alisema kuwa alijipanga kugombea Ubunge jimbo la Kigoma Mjini lakini Chama kinayo maamuzi na kama kitaamua hivyo basi hatokuwa na kipingamizi.

Millard Ayo
this is bad news to chadema and to the puppet politically speaking 🐒
 
Hata John M-nyika anaipenda Tanganyika yetu. Tukutane Nyikani .
 
Back
Top Bottom