Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Chadema inafeli sana,Leo mnaenda kuomba maridhiano wakati mlisusia uchaguzi Wa serikali za mitaa,maana yake ile migomo illikuwa ni mchezo Wa kuipa sisiem viti vyote,vipi kuhusu kina tundu lissu wameridhia hayo maridhiano chama kinaendeshwa na fikra za MTU mmoja hii ni aibu kwa upinzani.
 
Yaani mtu kakuibiwa mkeo kambaka na kila aina ya udhalilishaji, halafu wewe mwathirika unaomba maridhiano nae...

Ile gia ya anagani itawatesa miaka mingi sana ijayo.
 
Naona kuna watanzania wameshindwa kumsoma Mbowe kabisa. Hati kaomba poo. Usilolijua nikama usiku wa giza.
Sina chama lakini kati ya Mbowe na Zitto kwa hili ninamkubali Mbowe.
ha ha ha ''sina chama.....''
 
Hapo Zitto kakosea, kwa maana kila mtu yuko huru kusherehekea au kutosherehekea, na ndio uhuru tuliousherehekea jana: kuwa na mawazo, maoni na mitazamo huru kabisa! Kutofautiana ni jambo la asili na lina afya kwa jamii ilmradi hatuvunji sheria yoyote dhidi ya yeyote MsemajiUkweli,
 
MsemajiUkweli,
Zitto huyu huyu ndio alikuwa anabaki bungeni mara kwa mara wakati wenzie wanasusia kupitishwa kwa mambo ya ajabu.
Huyu huyu siku ya hotuba ya kwanza ya mkulu alibaki mjengoni, au sio yeye namfananisha tu?
 
Zitto anasahau mshirika wake Maalim Seif aliomba maridhiano kwa Karume?
Tofauti ilikuwa Mbowe kaomba hadharani kijasiri na yeye Maalim aliomba kimya kimya akapewa ulaji huku wenzie hawajui makubaliano ya siri ya Karume na Seif.

Siasa za Tanzania kichekesho sana, sishangai hata kule Kenya Raila Odinga alipokutana na Uhuru Kenyatta wenzie walimdhihaki kama hivi hivi.
 
Kwa mtazamo wako Paskali kipi bora Maridhiano ili amani itamalaki au mapambano ya jino kwa jino?
Mwenyekiti wa Chadema Mhe. Freeman Mbowe, aliwahasisha Chadema kususia uchaguzi wa serikali za mitaa, wakasusa, CCM wakatwaa ushindi wa mezani.

Katika bandiko hili nililaumiwa sana.

Jana pale Mwanza, Mhe. Mbowe kaomba maridhiano, swali ni jee Chadema waliposusa, walisusa ili wapate nini kama mwisho wa siku unakuja kubembeleza kuomba maridhiano?.

Siku zote haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, huwa inapiganiwa!.
P
 
Egnecious,
Kwahiyo wewe ukitoa maoni yako sawa , ila Zito akitoa maoni yake sio Mtanzania, hivi wewe unaelewa uhuru wa kutoa maoni kweli ???
 
Naunga mkono hoja, tupa kule zzk, twende na kina mbowe na lipumba. Kanaona wivu wenzake Jana wamepata coverage forums za kitaifa.
Mkuu hii ni vita ya kugombea wanachama ruzuku iongezeke.
Sasa naona safari hii Zitto kakanyaga button mbaya.

Hayo ya uraia ni mbwembwe tu za CCM.
 
Pascal Mayalla,
CCM ya sasa wako radical,wapinzani bado wapo siasa za enzi ya mzee Mwinyi.Ila kuna kitu kinanitatiza Paskali nisaidie kunijibu kama unaijua sababu.

Huyu Mbowe nimemfuatilia muda sana sasa kwa miaka mingi.Kila wakati kunapotokea events ambazo zinaibana sana serikali na kuupa nguvu upinzani,yeye ghafla hutustukiza na maamuzi ya ajabu ajabu yanayorudisha advantage kwa serikali ya ccm.Mfano ni hii ishu ya sasa,uchaguzi wa mitaa na kususa wapinzani kulishaiweka ccm kona mbaya.2015 upinzani ukiwa na Slaa ulikuwa tishio kubwa sana,ghafla bin vuu Lowasa huyu hapa,tena kwa Mbowe kushinikiza

wenzie!2010,Slaa alidai kumshinda JK,you all know what happened!Ndani ya Chadema,manguli wote wenye siasa kali mnaelewa kinachowakutaga,from Wangwe to Lissu.Mnyika alikuwa fire mno,muone hivi sasa alivyo.Mdee nae taratibu anasurrender to this kind of Mbowe diplomacy.Na hii siasa ya Mbowe imeifikisha wapi Chadema?Imeisaidia nini Tanzania mpaka sasa?Miaka mingapi imepita,makovu ya ccm yanaheal au yanazidi kuwa vidonda?huyu mbwa anayebweka anafanikiwa kumtiisha au walau kumtisha mwizi au kuzidi kumpa confidence ya kupanda ukuta baada ya kuona mbwa ni mbwekaji tu and nothing else?

Its time kumtazama Mbowe kwa jicho pevu.Simuamini tena.He might be something else!
 
Zitto kapanic kwa lile walilofanya CDM jana, kashtukizwa hakutegemea, anatamani ile nafasi ingekuwa yake kwa tabia zake za ki_opportunist, toka jana ni twitter, insta habanduki huko, eti leo Zitto anataka siasa za mapambano anawafundisha CDM!, wonders shall never end, wakati ule anaenda kukutana na JK watu wanamuuliza kulikoni anasema JK ni sawa na babake, vipi leo Magufuli sio sawa na babake pia?!
Mbowe ni mnafiki sana hili liko wazi, kasusia uchaguzi , CCM wakachukua ushindi wa 99% tena na vijembe juu vya Polepole , leo eti unaomba nao maridhiano huu ni ujinga mkubwa , yaani mtu akufanyie ubaya tena wala samahani asikuombe , wewe uliofanyiwa ubaya ndio utoke kuomba samahani , nakwambia chadema imekubali kuwa kibaraka wa CCM , huu ni ukweli mchungu kabisa
 
MsemajiUkweli,
Hivi kukaa unafuatilia sana mienendendo ya matukio ya kisiasa yanayohusiana na Rais wa Nchi na hatimaye kuanza kuyakosoa hata pasipokuwa na sababu yenye mantiki nayo pia inaweza kuwa ni kick kisiasa?

Nimesikia pia akimkosoa Mh. Kabudi kuwepo kwenye maridhiano ya wa-Kenya ya hivi karibuni kuwa anaingilia mambo ya nje ya nchi zingine, hapana siyo hivyo, Kabudi alikaribishwa, hakujipeleka mwenyewe. Pia mwka 2007 Rais mstaafu JK alikaribishwa huko huko Kenya na alienda akafanya kitu kikubwa cha kihistoria. Zaidi, kuondolewa vikwazo Zimbambwe, Mh.Kabudi hajaingilia chochote. Anatoa matamko ambayo ni ya SADC, kulingana na cheo alichonacho kwenye SADC, na si kama Waziri tu wa Serikali ya JMT.

Nashauri Mh. Zitto atafute ushauri mbadala kwa Serikali, kama anaona swala la Tanzania kujitoa kwenye mahakama husika kumefanywa katika namna ambayo anaona si sahihi.
 
Zitto Ni mwanasiasa zuzu kuwahi kutokea Tanzania.. tushamushitukia njama zake.

Mara aje na hoja za Uasi wa kijamii
Mara hoja za kutaka kumpa mchina bandari ya Bagamoyo.

Yani hiki kijamaa sasahivi hakina hoja madhubuti Zaidi ya kuhangaika tu.
 
Zitto Ni mwanasiasa zuzu kuwahi kutokea Tanzania.. tushamushitukia njama zake.

Mara aje na hoja za Uasi wa kijamii
Mara hoja za kutaka kumpa mchina bandari ya Bagamoyo.

Yani hiki kijamaa sasahivi hakina hoja madhubuti Zaidi ya kuhangaika tu.
Zuzu Mbowe anaejali maslahi yake binafsi ya ubunge 2020 na kuwatelekeza wagombea aerikali za mitaa.
 
Back
Top Bottom