Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

CHADEMA na CCM kama Simba na Yanga.

ACT WAZALENDO ni Azam Fc.
 
Nakubaliana na KC wa ACT wazalendo mh Zitto kwamba maridhiano yalipaswa kufanyika " kabla" ya uchaguzi wa serikali za mitaa na si sasa.

Na kwa bahati nzuri waziri wa Tamisemi alitoa hiyo fursa baada ya baadhi ya vyama vya upinzani kutishia kujitoa lakini akapuuzwa.

Leo hii kwa sababu wakubwa wanataka kutetea viti vyao bungeni ndio kamati kuu yote ya Chadema iliyosheheni wabunge wote inaona umuhimu wa kwenda Mwanza kuomba maridhiano kwa Mwenyekiti wa CCM.
Maridhiano ni jambo jema lakini mbona hamuwazungumzii kabisa wagombea wenu mliowaondolea udhamini kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa?

Kama Chadema wangekubaliana na agizo la Jaffo la kuwarejesha wagombea wote walioondolewa na watendaji leo Chadema ingekuwa na viongozi wa kutosha katika serikali za mitaa ambako ndipo penye " msingi" wa siasa.

Sikubaliani na Zitto katika approach yake ya kutumia nguvu lakini hili la kuwadharau wagombea wa serikali za mitaa Chadema mlichemka.

Maendeleo hayana vyama!
 
Mimi nafikiria Chadema wanaona mbali maana tunaambiwa na wazee kwamba "mtaka cha mvunguni shurti ainame" kaw hivyo Chadema lazima wainame ndio wakioate hicho cha mvunguni bila ya kuonama Hataweza kukipata.

Turufu au uti wa mgongo kwa Chama hicho ipo mikononi mwa Tundu Lissu. Kama hawakunyenyekea kwa Rais Magufuli na kutafuta maelewano na maridhiano bali Turufu hiyo itakuwa haina kazi ya maana. Kwa hivyo piga uwa ya kisiasa kwa Chadema ni Lissu lazima arudi nchini. Na natumai kubembeleza kote huko ni kumuingiza paka chumbani ili apambane na panya.

Nafikiri wapo sahihi maana ccm imekwisha kuonesha kwamba Lissu ni tishio kwa uhai wa Chama chao na wanamuogopa hasa. Sasa kama watafuzu jambo hilo na natumai watafuzu maana Makanisa yameshaingia ndani ya upatanisho na kwenda mbio kuleta maridhiano.

Lakini kwanini viongizi wa Makanisa wajitie ndani ya mizozo ya kisiasa?. Makanisa ya Turufu ya Veto hapa Tanzania na hasa Wakatoliki maana wao ndio wapiga debe wa Chama Cha Mapinduzi. Mkapa ndie mtu wa kati baina ya Kanisa Katoliki na Serikali walioikubali na kuridhia Wakatoliki.

Hawa Makanisa wa mashirika yao ya Kijasusi humu nchini tena yananguvu kubwa mfano wa shirika la JEISUIT la Wakatoliki au la FEBIAN Society nguvu za Vatican katika kudhibiti Ulimwengu.

Basi madhal mkono wa Kanisa upo ndani ya maridhiano Lissu atarudi na hataguswa hata kidole. Mimi nawaambia maneno hayo ambayo Lema alimwambia Zitto asubiri na ayatazame.
 
Kigogo 2014 tulishampuuza siku nyingi ndiyo maana tulimtimua huku Chadema
 
Zitto huyu ninayemfahamu awe tayari kwa mapambano ya "jino kwa jino"?
 
Kama kuna nafasi (room) ya political peace reconciliation ningeshangaa mno kama Mh. Mbowe na wanasiasa wenzake wangeigomea kuketi kisa eti wameonewa na kuumizwa sana..na wanaendelea kuumizwa na kusota magelezani na mahakamani kila kuchwao.

Kiongozi bora ni yule aliye dynamic....unabadilika kutokana na mazingira yaliyopo.... Mbowe ni dynamic ..kama fursa ya maridhiano ipo mezani why don't you grab it?

Kwenye Sayansi wanasema " If variable "A" doesn't work why don't you try using variable "B" ?.

Hongera Rais wetu na Hongera Mh Mbowe na timu yako kwa kuitikia wito, vitu kama hivi ndiyo vinavyotakiwa kufanyika hasa kwa wanasiasa vijana...mambo ya kuwindana kama wanyama wa mwitu kw eli tulifikia pabaya mno!!
 
Yale Yale ya UKUTA yamejirudia Kwenye Maridhiano ya kitaifa

Kwa hili nipo pamoja na Mh ZITTO,

Upinzani Kwa Tanzania bado Sana.
Ungeshauri nini ili upinzani uwe sana Tanzania?

Watanzania hawajui wanataka nini!

Kuna muda wanaonesha wanachukizwa na matendo ya CCM na serikali na kwamba wanatamani CHADEMA/Upinzani uongoze serikali!

Kuna kipindi wanataka CCM iendelee kushika dola na Wapinzani waendelee kuwa wapinzani maisha yao yote!

Kuna kipindi wanataka maridhiano na kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa!

Kuna kipindi HAWATAKI lolote. Wapo wapo tu!

CHADEMA wakisusia wanalaumiwa, wakikomaa wanalaumiwa!

Wakipambana barabarani wanalaumiwa, wakitaka maridhiano wanalaaniwa!

Mtanzania halisi si ndege wala mnyama. Ni Popo!
 
 
Hivi mnataka kusiwe Na maridhiano ili kuwe Na nn? Nimeamini watanzania wengi sio wazalendo
Alipaswa aombwe msamaha , sio yeye aliekosewa ndio ajipeleke kuomba msamaha , huo ni ujinga mkubwa alioufanya Mbowe , ameomba poo
 
Mapovu mpaka dawa iwaingie kisawasawa
 
Hayo aliyokuwa anafanya Zitto kipindi cha Kikwete na haya wanayofanya wakina Mbowe yakuomba waonewe huruma yanatofauti gani mkuu?.

Yaani siasa alizofanya Zitto tukaziona zakijinga ndio hizohizo wanakujanazo wakina Mbowe.
 
Wewe endelea kuumia tu as an individual, lakini umma unaweza Taifa kwanza. Lakini pia usisahau usemi kwamba if you can't beat them join them.
 
Waliosema if you can't beat them join them ain't that much stupid. Mtanzania gani mwenye akili timamu asiyejua kwamba JPM is due for re-election come next year!
 
Kumekuwa na mjadala mpana, kuhusiana na kitendo alichofanya kiongozi wa upinzani Bungeni (KUB) Mheshimiwa Freeman Mbowe, kuomba maridhiano ya kitaifa baina ya vyama vya upinzani kwa upande mmoja na watawala wa CCM

Kumekuwa na mawazo tofauti yanayotolewa kwenye mjadala huo, wengine wakisema, Freeman Mbowe, hakustahili kuomba maridhiano hayo na kundi jingine ni lile linalosema alikuwa sahihi kabisa kuomba maridhiano hayo kwa wakati huu

Mimi nami ningependa kutoa maoni yangu kama ninavyoruhusiwa kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 18(1) inayotamks hivi nanukuu " Kila mwananchi yuko huru kutoa maoni yake na kupokea maoni hayo bila ya kujali mipaka ya nchi na mawasiliano hayo hayapaswi kuingiliwa na chombo kingine chochote" mwisho wa kunukuu

Hebu sasa tuone mantiki ya Mheshimiwa Mbowe kuomba maridhiano hayo

Kwa mujibu ya nilivyosikia Maelezo yake aliyoyatoa siku ile ya kilele cha sherehe za Uhuru, pale Mwanza, tarehe 9/12/2019 ni kuwa wapo watu wengi sana wameumizwa na utawala huu wa awamu ya tano wengine wanahangaika sana kwenda mahakamani baada ya kubambikiwa kesi na Jeshi la Polisi nchini kwetu na wengine wamejeruhiwa na wengine kuuawa, wakati wakitekeleza kihalali shughuli zao za kisiasa, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ya mwaka 1977, ibara ya 3(1) ambayo nainukuu "Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendeshwa katika mfumo wa kidemokasia na ni ya mfumo wa vyama vingi" mwisho wa kunukuu

Hebu tuangalie kiuhalisia, hivi nchi yetu inaendeshwa katika mfumo wa kidemokrasia na ni mfumo wa vyama vingi??

Jibu hapa ni HAPANA kubwa kabisa, na Rais anafanya hivyo wakati anajua fika kuwa Katiba hiyo imempa kinga ya kutoshtakiwa akiwa hivi sasa yupo madarakani na hata baadaye atakapondoka madarakani!

Mfano halisi ni kile kilichotokea katika kile ambacho watawala wetu wanakiita kuwa wameendesha uchaguzi wa serikali za mitaa, ambapo wananchi wengi tumeuona kama ulikuwa UCHAFUZI wa serikali za mitaa, ambapo vyama vya upinzani walisusia baada ya wasimamizi wa uchaguzi, kuyakata majina ya wagombea wa vyama vya upinzani zaidi ya asilimia 95, ambapo majina ya wagombea wa CCM, yalionekana kama ya "malaika" ambapo asilimia 100 walionekana wamejaza kwa usahihi kabisa kwa asilimia 100 na hivyo kupita bila kupingwa!

Hivi katika mazingira hayo ya namna uchaguzi wa serikali za mitaa ulivyoendeshwa nchini na kwa namna utawala huu ulivyopiga marufuku kwa wapinzani kufanya mikutano yoyote ya kisiasa/kinyume cha Katiba ya nchi, wakati huo huo akiruhusu wenzao wa CCM kuendelea kufanya kampeni nchi nzima bila kubughuziwa na Polisi, hivi mnategemea Mbowe angeweza kufuata njia ipi kama siyo hiyo ya kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli??

Hebu nikumbushe kidogo historia, wakati ule wa enzi za utawala wa ubaguzi wa rangi kule Afrika Kusini, ambapo waafrika weusi waliteseka sana, hadi shujaa wetu, marehemu Nelson Mandela, kuhukumiwa kufungwa kifungo cha maisha, katika kesi ya kubambika alipoitwa mhaini, hivi kama isingekuwa kwa waafrika wa nchini humo kuomba maridhiano na makaburu wa nchini humo, huyo Mzee Mandela si angefia jela??

Ndiyo maana Mimi naamini kuwa uamuzi wa Freeman Mbowe wa kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ulikuwa sahihi kabisa na wanaoupinga hawaitakii mema nchi hii na wana nia nchi yetu iingie kwenye machafuko makubwa yanayofanana na mauajI ya kimbali

Mungu ibariki Tanzania
 
Kwa maana hii Wote wako sawa kila MTU afuate approach inayomfaaa......Hapa utuuzima unadawa Zito sio mgeni wa siasa za Bongo kuna kitu anakitafuta
 
Lazima ifahamike kuwa kuna kiwango cha uvumilivu ambapo mtu ana uwezo wa kuhimili na kiwango hicho kikipitiliza, basi maamuzi ya mtu huyo huwa yanakuwa ya hatari sana na hasa mtu huyo anappona anaonewa na vyombo vya dola, kama vile Jeshi la Polisi, mbavyo wajibu wao mkubwa vinapaswa kumlinda yeye na mali zake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…