Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Mimi binafsi hadi sasa bado sijaelewa maridhiano aliyoyaomba Mbowe mbele ya JPM ni yapi kati ya haya

Chadema wafutiwe kesi zao?
Uchaguzi serikali za mitaa urudiwe?
Ccm waache kuchukua wabunge na madiwani wa chadema?

Yani kwa kweli sijaelewa siku Chadema wakikutana na serikali wataongelea nini kuhusiana na hayo maridhiano

Ndio mda mwingine namuona Zitto yupo sasa maana sioni chochote cha muhimu
 
Namshauri Zitto kabwe asibeze hatua ambayo Chadema wameamua kuchukua.Badala yake kupitia chama chake cha ACT MAENDELEO nao Wachukue Hatua waitakayo.Chadema kutaka maridhiano hakumzui Zitto na Chama chake kuingia Barabarani.

MARIDHIANO KUHUSU NINI?

CDM wanataka "MARIDHIANO" kuhusu kitu gani?

Mwenyekiti wa CDM aliwahi kutangazia umma wa Watanzania kwamba anayoyahubiri Tundu Lissu katika majukwaa ya kimataifa ndiyo msimamo wa CDM. Mahubiri hayo yanamchafua Rais na hata kuitaka Jumuiya ya Kimataifa kutokuunga mkono juhudi za ujenzi wa Nchi na Taifa kwa ujumla! CDM imekuwa ikipinga kila linalofanywa na Serikali, iwe ujenzi wa Mradi wa Umeme wa maji "Stiggler's Gorge, SGR, Miradi ya barabara (fly-overs), ufufuaji wa ATCL, n.k. CDM inapinga kila kitu ili mradi ipinge tu!

Hii ndiyo CDM inayotafuta "MARIDHIANO"!

Sifahamu Hadidu za Rejea za "MARIDHIANO" zitakuwa zipi kabla kwanza CDM hawajakana kwa kutangaza hadharani kwamba si uungwana na si haki kuitendea Tanzania madhira kwa hatua ambazo CDM imezibuni na kuzitekeleza kupitia majukwaa ya kimataifa; pia CDM itangaze wazi kuunga mkono juhudi za makusudi zinazochukuliwa na Serikali kujenga Nchi na Taifa kwa ujumla.

Madhira yanayofanywa na CDM kwa Nchi na Taifa kwa ujumla hayaendani na nia njema ya kuomba "MARIDHIANO". Ni unafiki mtupu.
 
Mimi binafsi hadi sasa bado sijaelewa maridhiano aliyoyaomba Mbowe mbele ya JPM ni yapi kati ya haya

Chadema wafutiwe kesi zao?
Uchaguzi serikali za mitaa urudiwe?
Ccm waache kuchukua wabunge na madiwani wa chadema?

Yani kwa kweli sijaelewa siku Chadema wakikutana na serikali wataongelea nini kuhusiana na hayo maridhiano

Ndio mda mwingine namuona Zitto yupo sasa maana sioni chochote cha muhimu
Kama hujaelewa subiri kwani Mbowe alichokisema pale UWANJANI ndio hicho wote tulichokisikia
 
Namshauri Zitto kabwe asibeze hatua ambayo Chadema wameamua kuchukua.Badala yake kupitia chama chake cha ACT MAENDELEO nao Wachukue Hatua waitakayo.Chadema kutaka maridhiano hakumzui Zitto na Chama chake kuingia Barabarani.
Kwa hiyo mnatambua kuwa JPM ndiye Rais
 
Kamati kuu ilikaa na kuamua kuwepo na maridhiano kwa hiyo maridhiano ni msimamo wa chama tofauti na Zitto ambaye matamko yake ya Instagram ndio (ninavyofikiria mimi) msimamo rasmi wa ACTwazalendo.
Hebu angalia tofauti kati ya Chadema na Actwazalendo
Kamati kuu=Mbowe
 
Taifa zima liungane bila ya kujali tofauti zetu zote za dini,Siasa, Elimu, kabila kunusuru Taifa kurudi utumwani

Hongera sana Chadema kwa hatua yenu ya kumuunga mkono Rais Magufuli

Wabembe na Mabaki ya Sultan yamejipanga ipasavyo kurudisha Utumwani Visiwa vya Znz 2020!

Heshima kwako Comrade Freeman Aikael Mbowe, Prof Bingwa bobezi Lipumba na wengineo

Tanzania sio kitalu cha Kujifunzia kutawala
 
Wanataka maridhiano kwani kuna mafarakano?

wasimpotezee focus Rais
 
Cuf ile ya Prof Lipumba na maalimu Seif ilitumia hii kitu Jino kwa Jino lakini haikuwafikisha popote zaidi ya kutulizwa na IGP Mahita.
Hii approach haifai na imepitwa na wakati..... inaashiria vurugu badala ya amani na mshikamano.

Maridhiano anayoyaomba mh Mbowe walau yanaweza kuleta matumaini kama kweli kuna tatizo linalohitaji pande fulani kukaa mezani na kucompromise.

Cha muhimu kufahamu hapa ni kuwa siyo maridhiano yote hutoa option ya Nipe Nikupe.....maridhiano mengine yana option moja tu ya " Nibebe"

Kama ambavyo Rose Muhando alivyoimba katika wimbo wake wa Nibebe.

Maendeleo hayana vyama!
 
Tatizo Zito anajiona yeye anajua na anaweza kila kitu...na hicho ndio kilifanya akashindwa kuishi chadema....hapo alipo akili na Nguvu yake yote ni kuhakikisha Chadema inaanguka ili chama chake kiwe chama kikuu...kipindi kile cha JK chadema walifanya siasa za kiharakati
kwa wingi ambazo zilipelekea mauaji na majeruhi wengi tu yakiwemo Yakina Mwangosi...zito na baadhi ya watu walipinga na kudai chadema waache siasa za kiharakati za kudai haki...na wafanye siasa za kistaarabu...hata kipindi wenzie wanatoka bungeni kudai haki yeye alikuwa hatoki...leo itakuaje tena anageuka!....kwa kifupi a
Chadema ni adui wa Zito kuliko hata CCM.
 
Back
Top Bottom