Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Paragraph yako ya mwisho umeandika;
''Ndiyo maana Mimi naamini kuwa uamuzi wa Freeman Mbowe wa kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ulikuwa sahihi kabisa na wanaoupinga hawaitakii mema nchi hii na wana nia nchi yetu iingie kwenye machafuko makubwa yanayofanana na mauajI ya kimbali''

Imenibidi nicheke baada ya kusoma paragraph yako ya mwisho!

Yaani nchi iingie kwenye machafuko kwa sababu zipi? Kama watanzania hawakupigana na mkoloni wa mwisho ambaye alikuwa mgeni, unadhani wanaweza kupigana wao kwa wao? Forget it!

Halafu Mbowe anataka maridhiano gani kwa manufaa ya nani? Naomba unisaidie kunielimisha!

Kwani CHADEMA na vyama vya upinzani walipokataa kutambua ushindi wa Rais Mkapa na Kikwete yalifanyika maridhiano? Mbona Tanzania iliendelea kusonga mbele kama kawaida.

Ni kitu gani kwa sasa kimebadilika mpaka yawepo maridhiano wakati watanzania ni hao hao ambao walipuuza kelele za kuwashawishi kutawatambua Marais Mkapa na Kikwete.
 
Hakuna mwanaume wa kuleta vita nchi hii ,mbowe na chadema hawana mvuto wa kuingiza nchi kwenye machafuko

Yeye ameomba msamaha sio kwamba anawaonea huruma watanzania Bali anaona amrchuja na kesi ya akwilina inamtupa jela


State agent

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unataka Mbowe na CDM wafanye maandamano?ili wapigwe mabomu?tactiful Mbowe aliongea maneno mazito juzi na usifikiri hawajui kama jamaa ana ego.
Sent using Jamii Forums mobile app
 

Naona hata hujui unachokiongelea hapo.

Tume ya Ukweli na Maridhiano ya Afrika Kusini iliundwa mwaka 1995 na ilianza kazi mwaka 1996.

Hapo ndipo maridhiano yalipoanza. Na tayari Mandela alikuwa keshaachiwa na tayari alikuwa keshachaguliwa kuwa rais.

Kilichokuwepo kabla ya hapo, na ambacho ndicho nadhani unachokiongelea wewe, ni yale majadiliano na maafikiano yaliyopelekea Mandela kuachiwa na baadaye sera ya ubaguzi wa rangi kumalizwa.

Na usisahau kuwa moja ya mambo yaliyopelekea mpaka Makaburu wakakubali kufanya majadiliano na hatimaye kumwachia Mandela, ni pamoja na mapambano ya silaha.

 
Imebidi ucheke kwa vile wewe ni mmoja wa wanufaika wa tension iliyopo na watu wa sampuli yako ndiyo mnamjaza upepo Rais kwani unapata mkate wako kwa kuandika tungo za kuchochea usiwepo utengemano katika Taifa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hebu wewe kada wa Lumumba nieleweshe hiki kifuatacho, hivi ni kwanini Rais wa nchi kabla hajakabidhiwa madaraka ya kuongoza nchi, anaapa kuitetea na kuilinda Katiba ya nchi??

Hivi wewe unavyoona anavyofanya Rais ndicho kiapo chake cha kuitii na kuiheshimu Katiba ya nchi??

Hivi inakuwaje kwa mfano Rais wa nchi anatamka hadharani kuwa ni marufuku viongozi wa upinzani kufanya mikutano ya kisiasa hadi mwaka 2020, wakati yeye na chama chake, kila kukicha tunawaona wanazunguka nchi nzima kufanya kampeni??

Hivi huoni ubaguzi huu ambao unavunja Katiba ya nchi waziwazi, kuwa inaweza kupekekea nchi yetu ikaingia kwenye machafuko ya umwagaji damu nchini??
 
Hayo aliyokuwa anafanya Zitto kipindi cha Kikwete na haya wanayofanya wakina Mbowe yakuomba waonewe huruma yanatofauti gani mkuu?.

Yaani siasa alizofanya Zitto tukaziona zakijinga ndio hizohizo wanakujanazo wakina Mbowe.
Hakuna mahali Mbowe amesema waonewe huruma bali ametoa angalizo kwa Rais kutenda haki.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Zitto bado tu ujawajua chadema ndio hao hao waliotaka kukupoteza kwa ulimwengu wa siasa ukaamua kuanzisha chama chako
 
Jambo Hili Kule Ccm Kirumba Lilitamkwa Likiwa Sawa Sawa
Na Pale Yametazamwa Maslahi Ya Nchi Siyo Vyama Hivi Viwili Vya Ccm & Chadema


Tatizo Inaonekana Tayari Tumeyageuza Na Tunaelekeza Kulaumu Kuwa Upo Upande Ulioshindwa Labda Unaomba Huruma Kwa Huo Mwingine


Ni Nani Kati Yetu Hapendi Kuona Siasa Zikistawi Tanzania Pamoja Na Watu Wake Wakiwa Kwenye Ushirikiano Muda Wote Na Nchi Ikapiga Hatua

Maridhiano Ni Faida Kwa Tanzania Yote Bila Kujari Chama Wala Mtu Mmoja Mmoja
 
Imebidi ucheke kwa vile wewe ni mmoja wa wanufaika wa tension iliyopo na watu wa sampuli yako ndiyo mnamjaza upepo Rais kwani unapata mkate wako kwa kuandika tungo za kuchochea usiwepo utengemano katika Taifa hili.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu DOUGLAS SALLU usishangae huyo kada wa Lumumba namna anavyotetea vitu vya kipuuzi namna hiyo, kwa kuwa ndiyo namna yeye na familia yake wanavyotumika na ndiyo "means" ya kwenda "maliwatoni"
 

Freeman Mbowe is right. Muhimu kuwa na maridhiriano.
 

Unakosea, Mbowe is right
 
Mkuu Kennedy upo sahihi kwa asilimia 100

Wengi wa wachangiaji wanauchukulia ule kuwa ni mpambano mathalani wa watani wa jadi kati ya Yanga na Simba, wakati kiuhalisia alichofanya Mbowe, ni kuiepusha nchi yetu isiingie kwenye machafuko ya kupigana sisi wenyewe kwa wenyewe
 
Nijuavyo mimi aombaye maridhiano ni aliyeshindwa/aliyekosa namna. Kwa maana hiyo Mbowe anaomba maridhiano kwa kutomtambua Magufuli kama Rais pamoja na serikali yake? Kwa kususia chaguzi za serikali za mitaa zilizofanyika hivi karibuni?Kwa kuzuiwa kufanya mikutano hata ya ndani ya chama? Kwa kesi zinazowakabili mahakamani?n.k
Ni kipi hasa kilichompelekea yeye kuomba maridhiano baada ya madhila yote waliyofanyiwa ikiwemo Mwanasheria wake mkuu wa chama anayeishi uhamishoni mpaka sasa baada ya shambulizi la kikatili?
Sawa,baada ya kuomba maridhiano wamefikia makubaliano yepi?

Mbowe katuvunja sana moyo tuliowaamini, ilikuwa move ya hovyo kabisa kufanywa na tuliyemuamini kama kiongozi shupavu kwenda kupiga goti kuomba poo kwa waliyetuaminisha ni mtesi wao.
Unless atuambie waliyokubaliana katika maridhiano hayo na tuone kwa vitendo vinginevyo tutachukulia kama maridhiano yatakayomnufaisha yeye binafsi na viongozi wenzie chamani mwake.
 
Nini kifanyike sasa. Inaonekana unamwona mbowe kama kiongozi dhaifu sana.
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe hivi hujaona tatizo linaanzia wapi??

Ni kutokana na kitendo cha "kujimwambafai" kwa mkuu wetu, kwa kuamini kuwa yeye ndiye anayelimiliki Jeshi la Polisi nchini na kwa yeyote anayempinga yeye, hata kama ni kwa "constructive criticism" basi ataliamrisha Jeshi *lake" limshughulikie mtu huyo!

Na kwa namna Jeshi letu lilivyopoteza kufanya kazi yake kwa weledi, litatii amri hiyo Ingawa linajua kuwa siyo amri halali!
 
Hayo aliyokuwa anafanya Zitto kipindi cha Kikwete na haya wanayofanya wakina Mbowe yakuomba waonewe huruma yanatofauti gani mkuu?.

Yaani siasa alizofanya Zitto tukaziona zakijinga ndio hizohizo wanakujanazo wakina Mbowe.
Chama nimeamua kufanya siasa za kistaarabu.
 
Iko wazi Mbowe anajaribu kuukwepa mlango wa kuingia jela kupitia kesi ya akwilina ikiwa ni pamoja na kukilindaa kibarua chake.
Iweje Leo aombe maridhiano kwa mtu asiyemtambua kama Rais wa Nchi hii?

Kama walisusia Uchaguzi Serikali za mitaa halafu Leo hii anataka yeye awepo bungeni term ijayo? Je huo sio ubinafsi? Je shutuma zilizokuwa zikitolewa kwa muda mrefu kwamba Serikali inatesa na kuau watu Leo kumebadilika nini? Nimekuwa shabiki na kupigia kura wapinzani kwa term nne tofauti lakini kwa kitendo cha Mbowe kuomba poo nimemshusha vyeo vyote.

Kwangu Mbowe namuona kama wasaliti wengine tu, iweje aombe poo kwa mtu aliyemshtumu kumdhuru Lisu? Sio Mbowe aliyebariki safari za Lisu nje ya Nchi kuipaka matope Tanzania na Serikali yake?

Mwisho kabisa swala la watazania kupigana vita kwasababu ya Siasa zisizo na kichwa wala miguu liondoe kichwani kwako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…