Zitto Kabwe: Kuomba maridhiano kwa Rais Magufuli ni kujipendekeza na unafiki

Mbowe amekosea kuomba maridhiano na shetani. Ukatili ambao wamefanyiwa wapinzani haujawahi kuonekana tangu siasa za vyama vingi ziruhusiwe.
 
Wewe unayejiita State Agent unaleta kufuru!

Wewe unajua wazi kabisa kuwa huyo Rais wako, nguvu anazipata wapi.....

Anatumaini vyombo vya dola ndiyo vimbebe na mbeleko......

Siku vyombo vya dola vitakapoamua kuwa "fair" kwa vyama vyote, ndiyo siku hiyo watakuwa wanafunga virago pale mitaa wa Lumumba
 
"JokaKuu, post: 33754592, member: 221"]
..Mzee mwenzangu umesahau kwamba TANGANYIKA ilipata UHURU bila kumwaga damu, kupitia MARIDHIANO
.Mkubwa, Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini, Mwingereza alikabidhiwa tu na si chake.

Hakuwa na jinsi, walipaswa kukaa na Watanganyika ili kurefu muda.
Alikuwa tayari kwa maridhiano

Katika Tanzania huru tunahitaji maridhiano yapi kukidhi katiba na sheria zetu wenyewe?
..binafsi kuomba maridhiano siyo unyonge bali ni ishara ya kukataa kulipa unyama kwa unyama, ukatili kwa ukatili, na dhuluma kwa dhuluma.
Ni unyonge wa hali ya juu sana

Baada ya Wapinzani kuteseka na kuteswa leo Mbowe ndio anaona haja ya maridhiano?

Ndiyo maana nimeuliza swali ambalo halijibiwi hapa jamvini.
Kwamba, kuna tatizo gani hadi kuomba maridhiano?

Maridhiano ni mashauri baina ya pande zinazokinzana
Katika maingira yetu maridhiano ni kutokana na nini? Kwamba, katiba haina majibu ?
..alternative ya maridhiano ni CDM / wapinzani kulipa kisasi, na wakifanya hivyo hawatakuwa na tofauti na CCM.
Altenative haikuwa kisasi bali kusimamia haki
Kudai haki hakuna alternative, haki ikiwepo inatakiwa itolewe. Mbowe anadai nini?
..Nchi hii tuliaminishwa kuwa wapinzani wana vurugu na watasababisha vita, lakini utawala wa awamu ya 5 umedhihirisha kwamba watawala / CCM ndiyo wapenda shari, na wavunja amani na wenye kutishia mshikamano wa waTz.
Uhuni wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni kielelezo CCM inaweza kufanya chochote 'with impunity'

Hawa ndio wa kukaa nao kuomba maridhiano?

Kuna maridhiano ya kitu gani ambayo pengine hatuyajui?
Ninachokiona ni upande mmoja kupora haki.Lini haki ikaombwa kwa maridhiano?

Mbali na kosa la maridhiano ambalo halina justifications ya aina yoyote, kitendo cha kuwaacha Wapinzani wengine nje ni kuua united front !

Katika hilo Mbowe ameangalia impact yake siku za usoni?

Hayo yanatuacha na majibu mawili.

Kikao cha kamati kuu CDM na Mbowe hawakuwa makini.
Na kama walikuwa makini waliongozwa na agenda nje ya masilahi mapana ya chama chao

1. Maridhiano yanayohusu nini. Kuna ugomvi gani unaohitaji maridhiano.
2. Kutowashirikisha Wapinzani wengi ni upofu kwa kuangalia mambo kimkakati na kitalaam

Upofu huo unatokana na ''fatique'' ya kuongoza
kwamba Mbowe na kamati kuu CDM hawana mbinu mpya, mkakati wala hawana maono.

Njia rahisi na ya mkato dhidi ya changamoto zao ni kukumbatia Unyonge
 
Tushawastukia ACT kuwa chama chenu mnahitaji vurugu hapa nchini Nguruvi3,
Ndhani ACT watakuwa wanaangua kicheko kwa hoja hii

Ukitaka kuyaona mambo katika mtazamo mpana lazima uwe na fikra huru

Muhimu zaidi ni kusoma maoni yako na nakuhakikishia kuwa nina yaheshimu. Ni maoni yako
 
"Mmawia, post: 33752803, member: 165175"]
Mkuu maisha ya siasa hayaishii tu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tu.
Wala hiyo haikuwa hoja yangu ya msingi.

Huo ulikuwa mfano tu katika kujenga hoja zangu.

Hoja zangu za msingi na ambazo ningependa ikikupendeza uzijibu ni hizi
1. Maridhiano kutokana na tatizo gani?
2. Kutowashikisha Wapinzani kama ACT, je huko kukuui ''united front'' mbele ya safari?
3. Mbowe aliomba maridhiano kama kiongozi wa CDM au Upinzani?
Bado tunahitaji kupatiwa uwanja safi na huru wa kufanya siasa kwa kukutana na wananchi ili kusikikiza kero zao.
''Kupatiwa uwanja'' na nani?
Sheria za Msajili wa vyama na Katiba imekupa uwanja safi na huru.
Uwanja upi tena unaouomba?
Tunahitaji kuimarisha vyama vyetu kwa kufungua matawi na kuongeza wanachama.
Sheria inakuruhusu, ya Msajili wa vyama na Katiba ya nchi. Ukinyimwa sheria hivi unaidai au unaiomba?

Kwenda mahakamani kwa shauri lolote si kuomba sheria, ni kudai sheria ikupe haki

Sheria zimewekwa kukulinda na kukuhukumu ndio maana sheria haiombwi, inafuatwa

Unaposhindwa kusimamia sheria na haki yako ni tatizo lako, si la sheria au anayekunyima
Tunahitaji kujinadi kwa wapiga kura wetu kabla ya uchaguzi mkuu unao kuja kuliko kubakia sandukuni kama ilivyo sasa.
Unaweza kujinadi kila dakika, 24/7/365 na bado ukashindwa.

Uchaguzi wa serikali za mitaa unakupa jibu bila shaka.

Huhitaji kujinadi, unahitaji uwanja sawa wa mashindano.

Hapa huoni kudai katiba na tume huru ni muhimu kuliko kujinadi. Kamuulize Maalim
Tunahitaji taifa lenye upendo na umoja na mshikamano bila kubaguana kama ilivyo sasa.
Upendo na mshakamano ni suala la Watanzania wote.

Hakuna mwenye Upendo zaidi au anayepaswa kukumbatiwa ili upendo na mshikamano uwepo.

Upendo na Mshikamano ni ''two way street''
Tunahitaji kuheshimika kwa jamii na kupewa nafasi ya kushiriki kwenye mambo ya kitaifa kama ilivyo tokea juzi kwenye maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa nchi yetu maana sote ni wana tanzania.
Mbona katiba ya nchi imeshatoa?
Wewe unafarijika kitu gani ukiwaona viongozi wa vyama vya upinzani nchini wakishinda mahakamani kila wiki?
Je, wanashinda huko kwa dhulma au Haki?Je, jibu la tatizo hilo ni Unyonge!
Unapataje huo ujasili wa kupinga hatua angalau ya mh Mbowe kupata nafasi ya kumuelezea mh rais wa nchi na taifa kwa ujumla juu ya jambo hili muhimu kwa mustakabali mwema wa taifa letu?
Kwani imeanza leo, wakati wa Kikwete si walienda kunywa juisi ya maembe.

Walisikilizwa , je, outcome yake ilikuwa ni nini?

Kwa hili Mbowe na CDM hawana utetezi, ni fyongo tu pengine kwa masilahi yao binafsi

Kama si masilahi binafsi, watakuwa wamechoka kifikra, wanahitaji msaada au mapumziko
 
Zitto ni mnafiki tu
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ok: kwa mtazamo wako hakuna haja ya maridhiano, kwamba wapinzani hawana haja ya kukaa meza moja na ccm kwamba haki haiombwi, sasa hebu niambie; kwenye mazingira tuliyonayo Tz, ccm ndio chama dola na madhila yote wanayofanyiwa wapinzani, unasema haki haiombwi, unataka CDM wafanye nini? waendelee kugomea chaguzi ccm iendelee kujiokotea tu viti, CDM waandae vijana waingie msituni?, au waendelee tu kuwanunia ccm mpk mwisho wa dunia huku haki zao zikiendelea kukandamizwa?!

Napenda nijue solution ya kudumu toka kwako, sio solution feki itakayowafanya ccm waendelee kufanya wanayofanya kwa wapinzani, coz unaona walichofanya CDM wamekosea, naamini unapinga tu CDM walichofanya, but hujui action gani ya kufanya kumaliza tatizo, hebu tuwekee hapa hiyo solution tuione.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wa
 
Mkuu leo umerudi kwenye form,kweli there is no gambling like politics
 
Lakini hata hivyo Zito alikuwa karibu mno na Utawala wa awamu ya NNe, ndio tuseme naye alikuwa anajipendekeza kulinda nafasi yake ya Ubunge??
 
Huu mjadala ni mpana sana........
 



Wewe uliyeandika habari hii ni mbaguzi mkubwa wa ukabila, ilikupasa ueleze tu juu ya mambo ya kisiasa anayofanya Zitto bila kuingiza ukabila wa wazazi wake.

Kumbuka Tanzania haikuwepo kabla ya kuja kwa wakoloni, ni hao wakoloni ndio walioweka mipaka ya leo inayotufanya kwa upumbavu na ujinga wetu leo waafrika tuitane Wakongo, Warundi, Waha, wakurya nk, tumesahau kabisa katika mikoa ya mipakani kama Kigoma nk, Watu hawakuwa na mipaka ya kuchangamana kwani Warundi, Waha, Wakongo (wamanyema) nk, waliingia pande zote bila vizuizi kwa ajili ya biashara nk, hali kama hiyo ipo katika mikoa yote ya mipakani, makabila yapo pande zote za nchi tunazopakana, sasa ikitokea Mrundi na Mkongo wakazaa mtoto naye mtoto akawa Mtanzania hapo kunashida gani??--- ila, mkurya, mjaluo, mnyakyusa, mmakonde,mmasai, myao nk, ambao ni makabila yaliyopo ndani na nje ya Tz wao wakifanya siasa za kuwaudhi watu fulani kamwe huwezi kusikia wakiitwa "sio raia" !!!, ndiyo maana nasema ni upumbavu kunathibisha matukio ya kisiasa na ukabila na huko ni kufilisika kwa hoja

Sehemu kubwa ya Wenyeji wa manispaa ya Ujiji wanayo asili ya watu kutoka Kongo (Wamanyema) na wazazi wao walikuwepo kabla wakoloni hawajatugawa.

Tuache kasumba ya kikoloni ya divide and rule kupitia UKABILA.

Yawezekana hata wewe tukichimba asili yako yawezekana Babu yako alitoka Kongo au Rwanda.
 
Nashukuru kaka umempa ngumi za chembe jamaa haeleweki kipindi kile yeye anakutana na JK kasahau? Kapaniki kweli hjadi yericko nae kamchana kwenyr Instagram.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…