Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Wewe unayejiita State Agent unaleta kufuru!Hakuna mwanaume wa kuleta vita nchi hii ,mbowe na chadema hawana mvuto wa kuingiza nchi kwenye machafuko
Yeye ameomba msamaha sio kwamba anawaonea huruma watanzania Bali anaona amrchuja na kesi ya akwilina inamtupa jela
State agent
Sent using Jamii Forums mobile app
Kigogo 2014 ni mnafiki na mbinafsi mnoZitto huyuhuyu kwenye uzinduzi wa bunge aliamua kubaki na kusikiliza hotuba ya Magufuli akitofautiana na wabunge wengine wa upinzani walioamua kususia na hakuna aliyemehutumu. Katika siasa watu hutumia mbinu tofauti kufanikisha malengo yao.
Sent using Jamii Forums mobile app
.Mkubwa, Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini, Mwingereza alikabidhiwa tu na si chake."JokaKuu, post: 33754592, member: 221"]
..Mzee mwenzangu umesahau kwamba TANGANYIKA ilipata UHURU bila kumwaga damu, kupitia MARIDHIANO
Ni unyonge wa hali ya juu sana..binafsi kuomba maridhiano siyo unyonge bali ni ishara ya kukataa kulipa unyama kwa unyama, ukatili kwa ukatili, na dhuluma kwa dhuluma.
Altenative haikuwa kisasi bali kusimamia haki..alternative ya maridhiano ni CDM / wapinzani kulipa kisasi, na wakifanya hivyo hawatakuwa na tofauti na CCM.
Uhuni wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni kielelezo CCM inaweza kufanya chochote 'with impunity'..Nchi hii tuliaminishwa kuwa wapinzani wana vurugu na watasababisha vita, lakini utawala wa awamu ya 5 umedhihirisha kwamba watawala / CCM ndiyo wapenda shari, na wavunja amani na wenye kutishia mshikamano wa waTz.
Ndhani ACT watakuwa wanaangua kicheko kwa hoja hiiTushawastukia ACT kuwa chama chenu mnahitaji vurugu hapa nchini Nguruvi3,
Wala hiyo haikuwa hoja yangu ya msingi."Mmawia, post: 33752803, member: 165175"]
Mkuu maisha ya siasa hayaishii tu kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa tu.
''Kupatiwa uwanja'' na nani?Bado tunahitaji kupatiwa uwanja safi na huru wa kufanya siasa kwa kukutana na wananchi ili kusikikiza kero zao.
Sheria inakuruhusu, ya Msajili wa vyama na Katiba ya nchi. Ukinyimwa sheria hivi unaidai au unaiomba?Tunahitaji kuimarisha vyama vyetu kwa kufungua matawi na kuongeza wanachama.
Unaweza kujinadi kila dakika, 24/7/365 na bado ukashindwa.Tunahitaji kujinadi kwa wapiga kura wetu kabla ya uchaguzi mkuu unao kuja kuliko kubakia sandukuni kama ilivyo sasa.
Upendo na mshakamano ni suala la Watanzania wote.Tunahitaji taifa lenye upendo na umoja na mshikamano bila kubaguana kama ilivyo sasa.
Mbona katiba ya nchi imeshatoa?Tunahitaji kuheshimika kwa jamii na kupewa nafasi ya kushiriki kwenye mambo ya kitaifa kama ilivyo tokea juzi kwenye maadhimisho ya miaka 58 ya uhuru wa nchi yetu maana sote ni wana tanzania.
Je, wanashinda huko kwa dhulma au Haki?Je, jibu la tatizo hilo ni Unyonge!Wewe unafarijika kitu gani ukiwaona viongozi wa vyama vya upinzani nchini wakishinda mahakamani kila wiki?
Kwani imeanza leo, wakati wa Kikwete si walienda kunywa juisi ya maembe.Unapataje huo ujasili wa kupinga hatua angalau ya mh Mbowe kupata nafasi ya kumuelezea mh rais wa nchi na taifa kwa ujumla juu ya jambo hili muhimu kwa mustakabali mwema wa taifa letu?
Kila mtu na chama chake na sera zake,Zotto aliambiwa waungane akawa mkaidiiii sasa anajali nini mipango ya wenzie?.
Sent using Jamii Forums mobile app
Wala hiyo haikuwa hoja yangu ya msingi.
Huo ulikuwa mfano tu katika kujenga hoja zangu.
Hoja zangu za msingi na ambazo ningependa ikikupendeza uzijibu ni hizi
1. Maridhiano kutokana na tatizo gani?
2. Kutowashikisha Wapinzani kama ACT, je huko kukuui ''united front'' mbele ya safari?
3. Mbowe aliomba maridhiano kama kiongozi wa CDM au Upinzani? ''Kupatiwa uwanja'' na nani?
Sheria za Msajili wa vyama na Katiba imekupa uwanja safi na huru.
Uwanja upi tena unaouomba?Sheria inakuruhusu, ya Msajili wa vyama na Katiba ya nchi. Ukinyimwa sheria hivi unaidai au unaiomba?
Kwenda mahakamani kwa shauri lolote si kuomba sheria, ni kudai sheria ikupe haki
Sheria zimewekwa kukulinda na kukuhukumu ndio maana sheria haiombwi, inafuatwa
Unaposhindwa kusimamia sheria na haki yako ni tatizo lako, si la sheria au anayekunyima
Unaweza kujinadi kila dakika, 24/7/365 na bado ukashindwa.
Uchaguzi wa serikali za mitaa unakupa jibu bila shaka.
Huhitaji kujinadi, unahitaji uwanja sawa wa mashindano.
Hapa huoni kudai katiba na tume huru ni muhimu kuliko kujinadi. Kamuulize Maalim Upendo na mshakamano ni suala la Watanzania wote.
Hakuna mwenye Upendo zaidi au anayepaswa kukumbatiwa ili upendo na mshikamano uwepo.
Upendo na Mshikamano ni ''two way street''Mbona katiba ya nchi imeshatoa? Je, wanashinda huko kwa dhulma au Haki?Je, jibu la tatizo hilo ni Unyonge!Kwani imeanza leo, wakati wa Kikwete si walienda kunywa juisi ya maembe.
Walisikilizwa , je, outcome yake ilikuwa ni nini?
Kwa hili Mbowe na CDM hawana utetezi, ni fyongo tu pengine kwa masilahi yao binafsi
Kama si masilahi binafsi, watakuwa wamechoka kifikra, wanahitaji msaada au mapumziko
Ok: kwa mtazamo wako hakuna haja ya maridhiano, kwamba wapinzani hawana haja ya kukaa meza moja na ccm kwamba haki haiombwi, sasa hebu niambie; kwenye mazingira tuliyonayo Tz, ccm ndio chama dola na madhila yote wanayofanyiwa wapinzani, unasema haki haiombwi, unataka CDM wafanye nini? waendelee kugomea chaguzi ccm iendelee kujiokotea tu viti, CDM waandae vijana waingie msituni?, au waendelee tu kuwanunia ccm mpk mwisho wa dunia huku haki zao zikiendelea kukandamizwa?!.Mkubwa, Tanganyika ilikuwa chini ya udhamini, Mwingereza alikabidhiwa tu na si chake.
Hakuwa na jinsi, walipaswa kukaa na Watanganyika ili kurefu muda.
Alikuwa tayari kwa maridhiano
Katika Tanzania huru tunahitaji maridhiano yapi kukidhi katiba na sheria zetu wenyewe?
Ni unyonge wa hali ya juu sana
Baada ya Wapinzani kuteseka na kuteswa leo Mbowe ndio anaona haja ya maridhiano?
Ndiyo maana nimeuliza swali ambalo halijibiwi hapa jamvini.
Kwamba, kuna tatizo gani hadi kuomba maridhiano?
Maridhiano ni mashauri baina ya pande zinazokinzana
Katika maingira yetu maridhiano ni kutokana na nini? Kwamba, katiba haina majibu ?
Altenative haikuwa kisasi bali kusimamia haki
Kudai haki hakuna alternative, haki ikiwepo inatakiwa itolewe. Mbowe anadai nini?
Uhuni wa uchaguzi wa serikali za mitaa ni kielelezo CCM inaweza kufanya chochote 'with impunity'
Hawa ndio wa kukaa nao kuomba maridhiano?
Kuna maridhiano ya kitu gani ambayo pengine hatuyajui?
Ninachokiona ni upande mmoja kupora haki.Lini haki ikaombwa kwa maridhiano?
Mbali na kosa la maridhiano ambalo halina justifications ya aina yoyote, kitendo cha kuwaacha Wapinzani wengine nje ni kuua united front !
Katika hilo Mbowe ameangalia impact yake siku za usoni?
Hayo yanatuacha na majibu mawili.
Kikao cha kamati kuu CDM na Mbowe hawakuwa makini.
Na kama walikuwa makini waliongozwa na agenda nje ya masilahi mapana ya chama chao
1. Maridhiano yanayohusu nini. Kuna ugomvi gani unaohitaji maridhiano.
2. Kutowashirikisha Wapinzani wengi ni upofu kwa kuangalia mambo kimkakati na kitalaam
Upofu huo unatokana na ''fatique'' ya kuongoza
kwamba Mbowe na kamati kuu CDM hawana mbinu mpya, mkakati wala hawana maono.
Njia rahisi na ya mkato dhidi ya changamoto zao ni kukumbatia Unyonge
WaMimi namuunga mkono Zitto, haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa.
Kama upinzani nchini unacholilia ni kutendewa haki, hadi ukajitoa uchaguzi wa serikali za mitaa, tulitaraji huo upinzani uidai hiyo haki, lakini sijaona juhudi za upinzani wowote nchini Tanzania ukifanya juhudi zozote kudai haki.
Magufuli alipoingia tuu alipiga marufuku mikutano ya siasa kinyume cha katiba, kilichotokea kwenye ushawishi/ununuzi wa viongozi wa upinzani kuunga mkono juhudi, sote tunakijua. Kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa, sote tunakijua.
Mbowe akaona inatosha, Chadema haina uwezo wa kudai haki, hivyo ameomba poo kwa Magufuli kumaanisha sasa uendeshaji wa siasa za Tanzania ni kwa hisani ya Magufuli. Badala ya mapambano ya kudai haki, Mbowe ame opt kutafuta suluhu kwa maridhiano ya kisiasa.
P
Mkuu leo umerudi kwenye form,kweli there is no gambling like politicsMimi namuunga mkono Zitto, haki haiombwi wala hailetwi kwenye kisahani cha chai, inadaiwa.
Kama upinzani nchini unacholilia ni kutendewa haki, hadi ukajitoa uchaguzi wa serikali za mitaa, tulitaraji huo upinzani uidai hiyo haki, lakini sijaona juhudi za upinzani wowote nchini Tanzania ukifanya juhudi zozote kudai haki.
Magufuli alipoingia tuu alipiga marufuku mikutano ya siasa kinyume cha katiba, kilichotokea kwenye ushawishi/ununuzi wa viongozi wa upinzani kuunga mkono juhudi, sote tunakijua. Kilichotokea uchaguzi wa serikali za mitaa, sote tunakijua.
Mbowe akaona inatosha, Chadema haina uwezo wa kudai haki, hivyo ameomba poo kwa Magufuli kumaanisha sasa uendeshaji wa siasa za Tanzania ni kwa hisani ya Magufuli. Badala ya mapambano ya kudai haki, Mbowe ame opt kutafuta suluhu kwa maridhiano ya kisiasa.
P
Huu mjadala ni mpana sana........Ok: kwa mtazamo wako hakuna haja ya maridhiano, kwamba wapinzani hawana haja ya kukaa meza moja na ccm kwamba haki haiombwi, sasa hebu niambie; kwenye mazingira tuliyonayo Tz, ccm ndio chama dola na madhila yote wanayofanyiwa wapinzani, unasema haki haiombwi, unataka CDM wafanye nini? waendelee kugomea chaguzi ccm iendelee kujiokotea tu viti, CDM waandae vijana waingie msituni?, au waendelee tu kuwanunia ccm mpk mwisho wa dunia huku haki zao zikiendelea kukandamizwa?!
Napenda nijue solution ya kudumu toka kwako, sio solution feki itakayowafanya ccm waendelee kufanya wanayofanya kwa wapinzani, coz unaona walichofanya CDM wamekosea, naamini unapinga tu CDM walichofanya, but hujui action gani ya kufanya kumaliza tatizo, hebu tuwekee hapa hiyo solution tuione.
Sent using Jamii Forums mobile app
Nikiwa jirani wa Zitto Kabwe hapa Mwandiga Kigoma mahali alipozaliwa sijashangaa kabisa kuona upuuzi anaouandika huyu bwana mdogo kwenye mitandao ya kijamii ikiwemo jana ambapo ameshinda siku nzima anaibeza siku ya Watanzania kuadhimisha miaka 58 ya yangu Uhuru.
Hili suala naona kama halitiliwi mkazo inavyopaswa lakini ukweli ni kuwa Zitto hana asili ya Tanzania. Baba yake aliyekuwa Dereva wa Taxi ni mzaliwa wa DRC [emoji1078] na Mama yake ni Mzaliwa wa Burundi [emoji1060].
Kwa hiyo Zitto sio mtu anayeguswa na Tanzania na ndio maana kila kitu kizuri kwa nchi hii yeye hupinga na amekuwa akiendesha harakati za kuichua Tanzania ndani ya nchi na kimataifa.
Jana kashupalia kumshambulia Mbowe kwa kuhudhuria sherehe za Uhuru kule Mwanza, sasa mjiulize kuna ubaya gani kwa viongozi wa vyama vya upinzani kuhudhuria sherehe za uhuru? Kwa sababu zile sio sherehe za CCM ni sherehe za nchi.
Ndio maana viongozi wetu wote walikuwepo Rais, Makamu wa Rais, Rais wa Zanzibar, Waziri Mkuu, Makamu wa Pili wa Zanzibar, Maspika wote hadi wastaafu, Majaji wakuu na Marais Wastaafu wote ispokuwa Rais Mstaafu Kikwete ambaye sote tunajua yupo Marekani kwa majukumu muhimu ya kimataifa.
Mawaziri na Wabunge wenzake walikuwepo, Mabalozi wa nchi mbalimbali, viongozi wa dini nakadhalika.
Kwa tunaomjua na ajenda zake haki hii haiwezi kumpendeza hata kidogo, na mimi nimeamua leo niuseme huu ukweli ili Watanzania mjue.
Mnamuona anavyopambana kupinga miradi mikubwa ya maendeleo, yaani Zitto anatamani Watanzania wakose umeme, kwa hiyo anauchukia kabisa mradi wa bwawa la Nyerere utakaozalisha megawati 2,115 za umeme, anasikia raha kuona watu wanavyohangaika kusafiri kwa treni na ndege na hivyo hapendi kabisa kuona reli inajengwa na ndege zinanunuliwa, hapendi kuona vituo vya afya na hospitali zinajengwa, anafurahishwa kuona Watanzania wanakosa dawa hospitali, wanakosa mahali pa kupata matibabu na hivyo wanakufa. Anachukia kabisa kusikia Tanzania inapata mikopo nafuu kwa ajili ya kuwajengea wananchi miradi ya barabara, maji nakadhalika, na ndio maana anawatisha wananchi kuwa deni la Taifa kubwa mno wakati Wataalamu wa uchumi wanasema ni deni stahimilivu na fedha zinakopwa kwa mambo ya msingi kwa wananchi.
Kwake yeye Zitto taarifa za kuwa uchumi wa Tanzania ni mzuri hazifai, anashupalia shingo na kusikia raha kuwaaminisha Watanzania kuwa hali ya uchumi ni mbaya sana na yupo tayari kupika takwimu za kuonesha uchumi umezorota ili kuwatisha wawekezaji wasije kujenga viwanda na watanzania wakapata ajira na nchi ikapata kodi.
Na mengine mengi, naifahamu vizuri familia ya Zitto. Nashangaa kwa nini mmoja wa viongozi wa Kigoma ambaye baada ya Mama yake kukosa maziwa alipelekwa kunyonya kwa Mama yake Zitto hasemi ukweli huu kuwa huyu dogo hawezi kuguswa na mazuri ya Tanzania.
Zitto Kabwe pengine anaweza kufurahia uhuru wa DRC alikotoka Baba yake au Burundi alikotoka Mama yake. Na kama Watanzania mmesahau alipokuwa Chuo Kikuu Zitto alishaitwa mara kadhaa na Idara ya Uhamiaji kuhojiwa kuhusu uraia wake, kwa tunaofahamu hapa ndio palikuwa pa kupata ukweli wote na kama idara yetu ya uhamiaji ingekuwa shapu ingeumwaga ukweli huu ili Watanzania wajue.
Ndio maana kwa sisi majirani zake hapa Mwandiga hatushangai kuona jinsi anavyotumiwa na wazungu kuivuruga Tanzania, wazungu wanafanya hivyo kwa Zitto kwa sababu wanajua michezo hiyo hiyo ndio wanayoifanya DRC na Burundi ambako hakujatulia miaka na miaka na kila uchao ni mauaji tu. Wanatamani waivuruge Tanzania ili waje kuvuna rasilimali zetu kama wanavyovuna madini kule DRC.
Nampongeza Rais Magufuli na serikali yake kwa jinsi alivyombana Zitto, endelea hivyo hivyo na mwakani iwe ndio mwisho wa huyu mtoto mpuuzi. Alizoea huko tulikotoka walikuwa wanamkweza na kumfanya aonekane wa maana wakati ni kibaraka mkubwa na mtu asiyetakia mema Tanzania. Ni mpinzani asiye na faida kwa nchi. Muda wote anawaza machafuko tu.
Mbowe kazungumza maridhiano yeye anaona Mbowe kakosea, anataka fujo? Anataka vita? Hapo sasa watanzania ndio mnaweza kupata picha ya aina ya mtu huyu. Anachukizwa sana na hali ya amani ya Tanzania kwa sababu anajua hiyo ndio silaha kubwa inayomkwamisha.
Nawasihi watanzania wenzangu mpuuzeni, tujenge nchi yetu, wakati ni huu na kwa bahati nzuri tumepata Serikali ambayo inamwelekeo wa kututoa katika lindi la umasikini, ufukara na uombaomba. Tushike hapo hapo.
Mwananchi wa Mwandiga
Kigoma
Disemba 10, 2019
Lile tamko mlilotoa mwaka 2015 na dhamira ya kwenda korti za ICC,ICJ mlishafuta?Kwani Chadema walipinga Magufuli sio Rais? Kiswahili inaonekana kigumu sana kwako kuelewa.ccm oyeee
Nashukuru kaka umempa ngumi za chembe jamaa haeleweki kipindi kile yeye anakutana na JK kasahau? Kapaniki kweli hjadi yericko nae kamchana kwenyr Instagram.Zitto kapanic kwa lile walilofanya CHADEMA jana, kashtukizwa hakutegemea, anatamani ile nafasi ingekuwa yake kwa tabia zake za ki_opportunist, toka jana ni twitter, insta habanduki huko, eti leo Zitto anataka siasa za mapambano anawafundisha CHADEMA!, wonders shall never end, wakati ule anaenda kukutana na JK watu wanamuuliza kulikoni anasema JK ni sawa na babake, vipi leo Magufuli sio sawa na babake pia?!