ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 631
- 1,577
Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Ndugu Zitto Zubeir Kabwe kesho Novemba 7, 2020 anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na masuala mbalimbali yaliyojili kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.
Pia Kiongozi wa Chama atazungumzia mambo mbalimbali ikiwamo ukiukwaji wa sheria, taratibu, kanuni na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya wapinzani. Mkutano huo utafanyika saa 5:00 asubuhi kwenye Ofisi za Chama zilizopo Magomeni Jijini Dar es Salaam.
Tunawakumbusha waandishi wote msisahau vitambulisho vya Taasisi mnazofanyiakazi. Mwandishi ambaye hatakuwa na kitambulisho hatoruhusiwa kuingia kwenye mkutano huo. Tunaomba mzingatie hayo.
Imetolewa na:
Janeth Joel Rithe
Naibu/Katibu Uenezi, Habari na Mawasiliano kwa Umma
Leo Novemba 6, 2020.