Uchaguzi 2020 Zitto Kabwe kuzungumza na Vyombo vya Habari kesho Novemba 7, 2020

Kabla ya yote aseme kwanini yeye ni kiongozi kwenye ukiukaji wa sheria. Au amesahau alichomfanya mzee wetu Membe?
 
Usiingilie yakwetu kwani si mlimfukuza Membe? Sisi tunampa hifadhi siku akiamua kurudi kwao atakuja
 
Haki membe aombe radhi ili arudi nyumbani tuu.

Kwa manyanyaso aliyopewa na Zitto nimeamini msemo wa wahenga kwamba HERI KULA TEMBELE LANGU KWA AMANI KULIKO PILAU LA MASIMANGO
 
Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Ndugu Zitto Zubeir Kabwe kesho Novemba 7, 2020 anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na masuala mbalimbali yaliyojili kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.

Pia Kiongozi wa Chama atazungumzia mambo mbalimbali ikiwamo ukiukwaji wa sheria, taratibu, kanuni na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya wapinzani. Mkutano huo utafanyika saa 5:00 asubuhi kwenye Ofisi za Chama zilizopo Magomeni Jijini Dar es Salaam.

Tunawakumbusha waandishi wote msisahau vitambulisho vya Taasisi mnazofanyiakazi. Mwandishi ambaye hatakuwa na kitambulisho hatoruhusiwa kuingia kwenye mkutano huo. Tunaomba mzingatie hayo.

Imetolewa na:

Janeth Joel Rithe
Naibu/Katibu Uenezi, Habari na Mawasiliano kwa Umma
Leo Novemba 6, 2020.

Baada ya wananchi kuwatosa kwenye box la kura na barabarani saizi maandamano ni kwenye mitandao na press conference. Tafuta kazi ufanye we muha
 
Zitto atazuiwa...na pengine ndio lengo lakee
 
Haki membe aombe radhi ili arudi nyumbani tuu.

Kwa manyanyaso aliyopewa na Zitto nimeamini msemo wa wahenga kwamba HERI KULA TEMBELE LANGU KWA AMANI KULIKO PILAU LA MASIMANGO
Kwani Membe na yeye anatamani kukaa na wabakaji wa demokrasia?
 
Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Ndugu Zitto Zubeir Kabwe kesho Novemba 7, 2020 anatarajia kuzungumza na vyombo vya habari kuhusiana na masuala mbalimbali yaliyojili kwenye Uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 28, 2020.

Pia Kiongozi wa Chama atazungumzia mambo mbalimbali ikiwamo ukiukwaji wa sheria, taratibu, kanuni na uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu unaoendelea kufanywa na vyombo vya dola dhidi ya wapinzani. Mkutano huo utafanyika saa 5:00 asubuhi kwenye Ofisi za Chama zilizopo Magomeni Jijini Dar es Salaam.

Tunawakumbusha waandishi wote msisahau vitambulisho vya Taasisi mnazofanyiakazi. Mwandishi ambaye hatakuwa na kitambulisho hatoruhusiwa kuingia kwenye mkutano huo. Tunaomba mzingatie hayo.

Imetolewa na:

Janeth Joel Rithe
Naibu/Katibu Uenezi, Habari na Mawasiliano kwa Umma
Leo Novemba 6, 2020.

Ujinga mtupu!! Kakosa ajira anambwerambwera tu, atulize kipago.
 
Hichi ndio kilichofanya mitandao ifungwe washindi wa kura za mabegi
 
Back
Top Bottom