Zitto Kabwe ni mgonjwa alazwa Marekani, madaktari wamtaka asisafiri

Wewe ukizeeka lazima uwe mchawi tena wa kula nyama za watu

Sent using Jamii Forums mobile app
Kombinesheni ya hatari!
FB_IMG_1581350070283.jpeg
 
Hii ni kwa mujibu wa mdhamini wake alipokuwa anaiambia Mahakama kisa cha Zitto kutokuwepo mahakamani leo ambapo kesi yake ya uchochezi imesomwa tena.

========

Heri Kimbita ambaye Mdhamini wa Zitto Kabwe, ameiambia Mahakama leo kwamba, Zitto Kabwe anaumwa na amelazwa huko Marekani. Madaktari wake wamemzuia asisafiri na kumuambia apumzike siku zisizopungua kumi ili waangalie afya yake inaendeleaje.

Kesi yake imeahirishwa hadi tarehe 19 Februari 2020.

Leo Mahakama ilikuwa itoe maamuzi kama ndugu Zitto ana kesi ya kujibu ama vinginevyo.

Zitto anadaiwa Oktoba 28, 2018 akiwa katika mkutano na waandishi wa habari, uliofanyika katika Makao Mkuu ya ofisi ya Chama cha ACT Wazalendo, alitoa maneno ya uchochezi yenye kuleta hisia ya hofu na chuki.

Ilidaiwa kuwa katika tarehe hiyo hiyo, Zitto alitoa maneno ya uchochezi dhidi ya Jeshi la Polisi akisema, “Tumekuwa tukifuatilia kwa kia yanayojiri yote huko Uvinza, tunasikitika kusema kuwa taarifa tunazozipata kutoka Uvinza zinaogofya mno, kwani tunaambiwa kuwa wananchi zaidi ya 100 wa kabila la Wanyantuzu wamepoteza maisha kwa kupigwa risasi na Polisi, wengine wakisema kuuawa hata wakiwa kwenye matibabu hospitalini baada ya kujeruhiwa kwenye purukushani na jeshi la polisi...”
Tunamuombea kwa Mungu apate nafuu ya haraka.
 
February 10, 2020
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkuu
Kisutu, Dar es Salaam, Tanzania

Habari toka mahakamani, Mh. Zitto Kabwe kiongozi Mkuu wa ACTWazalendo amepata udhuru na kushindwa kufika Mahakamani kutokana na ushauri wa daktari kutokana na hali yake ya kiafya.

Source: VOA Swahili
 
Back
Top Bottom