BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Kupitia Ukurasa wake wa X (Twitter) Kiongozi wa Chama Mstaafu kutoka ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ameandika "Nitashangaa sana kushindwa hii kesi. Kampuni ya PAET, mtoto wa ORCA, alipokuja nchini mwaka 2001 alikuta tuna gesi imeshavumbuliwa. Hawakuwekeza hata senti tano nyekundu kutafuta Gesi Asilia kule Songosongo.
Fedha yote iliyowekwa kujenga mitambo ya kunyonya gesi na kujenga bomba kuja Dar es Salaam ilikuwa ni mkopo wa Benki ya Dunia kwa Tanzania. Hawakuweka mtaji hata thumni. Mradi mzima ulikuwa debt financed. Hapakuwa na equity.
Walipewa mpaka mwaka 2026 watukabidhi tuendeshe wenyewe au tutafute mwekezaji mwengine au tuwaongezee muda. Wamekuwa waki lobby tuongeze muda ( na kuna hoja kwenye hili ingawa sio kwa mikataba kama hii ya mwaka 2021).
Sasa wameamua kutushitaki kututisha ( blackmailing). Ofisi ya AG inapaswa kupata wanasheria wabobezi kutoka pia nje ya Serikali na kuunganisha nguvu na wana harakati kama ilivyokuwa kwa kesi ya City Water. Tutawashinda"