GE2025 Zitto Kabwe: Polisi atakayebeba Kura Bandia ni halali yetu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Akihutubia iku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma katika mwendelezo wa Operesheni Majimaji ya chama hicho, Zitto ameeleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura.

"Tunajua CCM wanatumia kura bandia, kura bandia zinapigwa halafu zinaletwa kwenye kituo cha kupigia kura. Isivyo bahati, kule Kigoma tulimkamata Afisa wa Polisi akiwa amepakia kura bandia. Afisa yule alichokipata sidhani kama atarudia jambo lile," amesema Zitto.

Katika kauli hiyo, Zitto amesema chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa mbinu chafu kama hizo.

"Ninataka nitangaze rasmi hapa, na maafisa wa polisi watusikie: hatutajali magwanda yao, hatutajali nyota zao, hatutajali mitutu yao. Polisi atakayebeba kura bandia ni halali yetu," ameongeza kwa msisitizo.

Suala la maafisa wa usalama kuhusishwa na uingizaji wa kura bandia ni mojawapo ya hoja kubwa zilizowasilishwa na ACT Wazalendo katika mashauri kadhaa waliyoyafungua kupinga matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, hasa katika baadhi ya maeneo ya Kigoma.

Zitto amesisitiza kuwa Operesheni Majimaji inalenga kulinda demokrasia na kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 unakuwa huru na wa haki.

Zitto kwa mbwembwe fake, sijawahi mkubali huyu msanii wa bongo movie hata siku moja. Ni mupuuzi mno, katawaliwa na uchawi sana.
 
Zito anavuta Bangi amekuwa chizi kajitoa fahamu zote kwa Akili zake mbovu kaamua kutumia kivuli cha chadema kusaka kiki za kijinga jinga akizani watanzania ni wapumbuvu kama yeye, Chadema ni jicho na Tochi mwanga Nuru ya wapenda haki wanaojitambua kamwe hawezi kuidhoofisha atabakia kubwabwaja wee hadi achoke
 
Kwa nini hakufanya hivyo kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2024?
 
Chadema waliona mbalisana, N.N.E.

Wameamua kushughulika na mzizi sio matawi.
Lisu na Heche they're true. Leaders.

DJ alizingua vyakutosha.
 
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Akihutubia iku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma katika mwendelezo wa Operesheni Majimaji ya chama hicho, Zitto ameeleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura.

"Tunajua CCM wanatumia kura bandia, kura bandia zinapigwa halafu zinaletwa kwenye kituo cha kupigia kura. Isivyo bahati, kule Kigoma tulimkamata Afisa wa Polisi akiwa amepakia kura bandia. Afisa yule alichokipata sidhani kama atarudia jambo lile," amesema Zitto.

Katika kauli hiyo, Zitto amesema chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa mbinu chafu kama hizo.

"Ninataka nitangaze rasmi hapa, na maafisa wa polisi watusikie: hatutajali magwanda yao, hatutajali nyota zao, hatutajali mitutu yao. Polisi atakayebeba kura bandia ni halali yetu," ameongeza kwa msisitizo.

Suala la maafisa wa usalama kuhusishwa na uingizaji wa kura bandia ni mojawapo ya hoja kubwa zilizowasilishwa na ACT Wazalendo katika mashauri kadhaa waliyoyafungua kupinga matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, hasa katika baadhi ya maeneo ya Kigoma.

Zitto amesisitiza kuwa Operesheni Majimaji inalenga kulinda demokrasia na kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 unakuwa huru na wa haki.

Kukubali kushiriki kwenye hili zoezi ni kuipa legitimacy ile staged election ya watawala.
 
Mlitaka afanye nn?
Mbn hata ninyi CDM ni matapeli tu.
* 2015 mliunda ukawa - majimbo mengi mliyavuruga kwa kutowaachia wenzenu i.e Jimbo la buyungu ilikuwa wapewe nccr lkn baadae mkaweka mgombea

Jimbo la bukoba mjini cuf lkn mkaweka mgombea wa CDM

Kosoeni wengine, nanyi jikosoeni
Haukuwa umoja wa kisheria, na wala hakukuwa na vigezo vinavyokubalika kwa wote nchi nzima. Hata sasa kuna waliohama cdm ili wakagombee uchaguzi pengine, kama kuna waliohama kwa kutokubaliana na msimamo ww chama, ulitegemea nini katika kuachiana majimbo kwa mtu wa chama kingine?
 
Suala la maafisa wa usalama kuhusishwa na uingizaji wa kura bandia ni mojawapo ya hoja kubwa zilizowasilishwa na ACT Wazalendo katika mashauri kadhaa waliyoyafungua kupinga matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, hasa katika baadhi ya maeneo ya Kigoma.
Huyu Zitto ameshakuwa mpumbavu! Sasa kama maafisa kuingiza kura bandai vituoni walishalitoa mahakamani kama ushahidi kuna kesi yoyote walishinda? Na mwaka huu kura zitaingizwa tena kwa kusindikizwa na mitutu atawafanya nini?
 
Mlitaka afanye nn?
Mbn hata ninyi CDM ni matapeli tu.
* 2015 mliunda ukawa - majimbo mengi mliyavuruga kwa kutowaachia wenzenu i.e Jimbo la buyungu ilikuwa wapewe nccr lkn baadae mkaweka mgombea

Jimbo la bukoba mjini cuf lkn mkaweka mgombea wa CDM

Kosoeni wengine, nanyi jikosoeni
Mwisho wa siku hayo majimbo si yalienda UKAWA? Mlitaka tuweke wagombea dhaifu ili mshinde kirahisi?
 
Rais Mtarajiwa LISSU ,Mtanzania namba Moja mwenye Uwezo mkubwa wa Akili, Uzalendo, Mwenye Haki, Mpaka Mafuta wa Mungu ( Kwa hizo sifa tu nloandika, Samia alisoma hapa, anajisikia vibaya)... Huyu Mh Lissu Kesi yake ya UHAINI imejikita kwenye Maneno ya 'Tutakinukisha '.

Haraka sana mtu Mmoja Ofisi ya DPP, Kwa ushirikiano wa CCM wakaelekeza Polisi wamkamate na kumpa Kesi ya UHAINI.

Kwa Upande wa pili, Zitto Licha ya Hotuba zake zinazohimiza Machafuko, Majuzi amenukuliwa akisema " POLISI ATAKAYEBEBA KURA FEKI HUYO MI HALALI YETU".... Kwa Zitto, Polisi huyo atatakiwa Kusulubishwa/Kuwajibishwa na Wanachama wake wa ACT Yaan Apigwe !!.

Maajabu ni kwamba CCM, DPP, na Polisi , wako kimyaa, hawajaangaika kusema na kumkamata Zitto Kwa UHAINI !!.

Baadae nawaambia kwann Zitto Kabwe kabadili Gia angani na kuanza kushambulia CCM.
 
Back
Top Bottom