JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kuzungumza na viongozi wa vyama vya siasa leo Januari 3, 2022, (Rais Samia: Vyama vya siasa ruksa kufanya Mikutano ya hadhara ) kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa neno:
"Wakati Rais Samia anakula kiapo kwa mara ya kwanza aliahidi kukutana na wanasiasa na kutengeneza mazingira ya siasa zenye tija.
“Rais ametembea kwenye maneno yake na vitendo vilivyofanyika ni lazima apongezwe, haikuwa kazi rahisi sote tunajua.
“Wakati tunafanya mkutano wa kwanza wa vyama Desemba 2021, maneno yalikuwa mengi sana, baadaye tulipofanya mkutano wa Kituo cha Demokrasia (TCD) maneno yalikuwa pia, ni lazima apongezwe.
“Ni wajibu wetu kutumia majukwaa kuwasemea Watanzania, tutatumia majukwaa ya kisiasa na huo ndio wajibu wetu, nadhani tumeanza vizuri mwaka wa mageuzi ya kisiasa.”