Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

ChoiceVariable

JF-Expert Member
Joined
May 23, 2017
Posts
66,537
Reaction score
75,687
zitto.jpg

Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

=======

MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO

Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe

Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar

========

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.

Kama Zanzibar isingekuwa inapangiwa na kutawaliwa na Tanganyika ingekuwa kama Mauritius au Saychelles 👇👇

View: https://twitter.com/AfricaFactsZone/status/1787528342389879247?t=spKjGQ9yyEpYSftfw0IDbg&s=19
20240507_141215.jpg
20240507_141212.jpg
20240507_141218.jpg

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Mfanyakazi Online Media
 
Hakuwez kuwa sawa, kama asilimia 85 ya mapato yanatokea bara, na bara ndio wenye mahitaji makubwa huoni ni kuupendelea upande fulani?
Zanzibar inajitegemea Kwa Mapato yake ,kinachotoka Bara kwenda huko ni 2% tuu na wakati Bara mnakomba 98% ya Mapato yanayotokana na Muungano zikiwemo zaidi ya Bilioni 400 ambazo TRA anakusanya Bado taasisi zingine kama uhamiaji ,Utalii nk.
 
Pia itakuwa busara tukisema na madeni tushare kwa pro-rata

Kudaiwa na zanzibar is not a point kama deni la nje ni tril 90 walelete madai yao yaoigizwe kwenye deni tukisha rekebisha muungano tutalipa tu
 
Zito Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zito ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.
View attachment 2978631

My Take
Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano maana wananyonywa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lisu.
View attachment 2978630
Anaongelea TRA ilhali anafahamu fika kuwa Zanzibar wana mamlaka yao ya mapato ZRA, ambayo Zanzbar inatumia mapato yake yote kwa 100%

Kama suala la mapato ni la Muungano, ZRA ni ya kazi gani Zenji? Si iwe tu hiyohiyo TRA...!!?

Kumbe kweli Zitto ni "mpumbavu"
 
Zanzibar inajitegemea Kwa Mapato yake ,kinachotoka Bara kwenda huko ni 2% tuu na wakati Bara mnakomba 98% ya Mapato yanayotokana na Muungano zikiwemo zaidi ya Bilioni 400 ambazo TRA anakusanya Bado taasisi zingine kama uhamiaji ,Utalii nk.
Malalamiko mwisho lini? nyie maccm?
Tukisema tuandike katiba mpya tuondoe manunguniko hamtaki

Nyie ni viumbe wa ajabu sana
 
Zanzibar inajitegemea Kwa Mapato yake ,kinachotoka Bara kwenda huko ni 2% tuu na wakati Bara mnakomba 98% ya Mapato yanayotokana na Muungano zikiwemo zaidi ya Bilioni 400 ambazo TRA anakusanya Bado taasisi zingine kama uhamiaji ,Utalii nk.
Zanzibar Wana bodi Yao ya Kodi wanachokusanya Zanzibar ni Chao tu hawakileti Tanzania bara
 
Zito Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zito ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.
View attachment 2978631

My Take
Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano maana wananyonywa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lisu.
View attachment 2978630
Zito huwa yuko makini sana, huchagua angel moja muhimu na kuielezea kifasaha sana kwa lugha rahisi, ya busara na ya staha sana.....

sasa sikilizia mamluki wa kibaraka, kwanza watachangamka kidogo, japo watakua wamechanganyikiwa vibaya zaidi 🐒
 
What is the poorest country in the world?

Africa
  • Somalia.
  • South Sudan.
  • Sudan.
  • Tanzania.
  • The Gambia.
  • Togo.
  • Uganda.
  • Zambia.
 
Zito huwa yuko makini sana, huchagua angel moja muhimu na kuielezea kifasaha sana kwa lugha rahisi, ya busara na ya staha sana.....

sasa sikilizia mamluki wa kibaraka, kwanza watachangamka kidogo, japo watakua wamechanganyikiwa vibaya zaidi 🐒
Zito ni mchumi mwenzangu, takwimu zinaongea hatutaki porojo.
 
Back
Top Bottom