Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zito Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zito ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.
View attachment 2978631

My Take
Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano maana wananyonywa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lisu.
View attachment 2978630

Zito awaokote wasiojielewa.

Wale wasiojua:

Mikopo inachukuliwa na Tanganyika kwa jina la Tanzania. Na siku zote mkopaji ndiye anayedaiwa. Lakini kuanzia mwaka 2022 Zanzibar imekuwa ikipewa 20% ya mikopo hiyo huku Zanzibar ikiwa na watu 3% tu ya watu wote.

Kuanzia mwaka 2022, misaada ambayo imekuwa ikitolewa kwa Tanzania, Zanzibar imekuwa ikichukua 20% wakati idadi ya watu na ukubwa wa eneo la Zanzibar ni chini ya 4% ya nchi.

Makubaliano wakati wa Muungano, Zanzibar inastahili kupewa 8%, ambayo bado ilikuwa kubwa sana kulinganisha na kile wanachopata Tanganyika. Lakini sasa, kimya kimya imetoka kwenye 8% mpaka 20%. Wakati huo huo, bado kuna gharama nyingine kama umeme, Zanzibar imekuwa hailipii kwa maelezo kuwa mapato yake ni madogo!!
 
Zanzibar Wana bodi Yao ya Kodi wanachokusanya Zanzibar ni Chao tu hawakileti Tanzania bara
Kwani nani kasema hawana ZRA? Kama hakiji Bara TRA wanafanya nini Zanzibar?

Uwe unaelewa maana ya mambo ya Muungano na Mambo yasiyo ya Muungano.

Hoja ya Zito ni kwenye mambo ya Muungano,Bara ndio wananufaika zaidi licha ya Zanzibar kuchangia.
 
Zito awaokote wasiojielewa.

Wale wasiojua:

Mikopo inachukuliwa na Tanganyika kwa jina la Tanzania. Na siku zote mkopaji ndiye anayedaiwa. Lakini kuanzia mwaka 2022 Zanzibar imekuwa ikipewa 20% ya mikopo hiyo huku Zanzibar ikiwa na watu 3% tu ya watu wote.

Kuanzia mwaka 2022, misaada ambayo imekuwa ikitolewa kwa Tanzania, Zanzibar imekuwa ikichukua 20% wakati idadi ya watu na ukubwa wa eneo la Zanzibar ni chini ya 4% ya nchi.

Makubaliano wakati wa Muungano, Zanzibar inastahili kupewa 8%, ambayo bado ilikuwa kubwa sana kulinganisha na kile wanachopata Tanganyika. Lakini sasa, kimya kimya imetoka kwenye 8% mpaka 20%. Wakati huo huo, bado kuna gharama nyingine kama umeme, Zanzibar imekuwa hailipii kwa maelezo kuwa mapato yake ni madogo!!
Onyesha hiyo 20% ulikoitoa maana hiyo hoja ndio Zito kaioinga hapo Juu Kwa kusema ni 4.5% only.

Pili mbona huzungumzii hoja yake ya kwanza?

Msitafute excuses TRA peke yake inakusanya zaidi ya Bilioni 400 kutoka Zanzibar hapo sijataja taasisi zingine za Muungano mfano Uhamiaji nk.
 
Zenj wangejitawala wangekuwa mbali sana,wanapiga kazi ila Bara watu Wana mdomo na fitina hatari.

Just imagine licha ya Samia kutoka Zanzibar kuwaokoa kwenye uchumi ulikokuwa unakuta wameishia kumjazia fitina 😁😁
Wapo wachache wangepiga pesa nyingi sana .Hiyo covid tu walipata pesa kibao ila mpaka waombe maana zipo bara.
Bara hata mtaji wa BOT hawamjui umetoka wapi, huku bara wengi hawajitambui kazi elimu za kufoji.

Zenji wangefika mbali sana kwa kweli kama Dubai.
 
Zito ni mchumi mwenzangu, takwimu zinaongea hatutaki porojo.
Yes,
hiyo sasa ndio inaitwa hoja sio maoni na mtazamo wa yule kibaraka ambae mamlulki wake wanasema ana hoja wakati ni stori na porojo tupu 🐒

with that,
tunaweza discuss na hata kua na mjadala wa kitaifa kuweka record sawa na tunasonga mbele.

habari ya kuropoka kama kibaraka bila staha inapoteza maana ya anachokusudia kuiibua, wenye hekima na busara wanashindwa kustahimili kuishi kwenye joto la utovu wa kimaadili kwenye lugha za viongozi 🐒
 
Sasa hapo ndio uneongea nini? Kwanza Huwa mnawapelekea Watangabyika kutawala kule View attachment 2978632
Fatma haoni irony ya kumuita Ali Hassan Mwinyi mtanganyika kwa sababu tu alizaliwa kivure Tanganyika. Kuwa alisoma primary Zanzibar na aliishi huko sehemu kubwa ya maisha yake yote. Wakati wa uhuru wa Tanganyika alikuwa Uingereza na aliporudi alirudi Zanzibar kama mkuu wa chuo. Wakati wa mapinduzi alikuwa Zanzibar, sio Tanganyika. Anasahau kuwa babu yake alizaliwa Nyasa mwaka 1905 na hivyo kwa tafsiri yake hakuwa mzanzibari. Ana selective memory. Hajawahi kuzungumzia ubaya wa babu yake lakini kutwa anashupalia ubaya wa watanganyika!

Amandla...
 
Nadhani tuwe na "" Tanzania revenue authority znz, na Tanzania revenue authority mainland""
Kila mmoja akusanye kwa maendeleo yake! Mengine tuendelee kuyatatua polepole!
Maana ya Muungano itakuwa haipo.Suluhu ni Nchi Moja ,jambo ambalo Wazanzibar hawataki kusikia.
 
Fatma haoni irony ya kumuita Ali Hassan Mwinyi mtanganyika kwa sababu tu alizaliwa kivure Tanganyika. Kuwa alisoma primary Zanzibar na aliishi huko sehemu kubwa ya maisha yake yote. Wakati wa uhuru wa Tanganyika alikuwa Uingereza na aliporudi alirudi Zanzibar kama mkuu wa chuo. Wakati wa mapinduzi alikuwa Zanzibar, sio Tanganyika. Anasahau kuwa babu yake alizaliwa Nyasa mwaka 1905 na hivyo kwa tafsiri yake hakuwa mzanzibari. Ana selective memory. Hajawahi kuzungumzia ubaya wa babu yake lakini kutwa anashupalia ubaya wa watanganyika!

Amandla...
Nyie watu wa Bara ndio mumeyaleta haya Kupitia mropokaji Lisu
 
Back
Top Bottom