Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.
Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.
Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.
=======
MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO
Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe
Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar
========
View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785636663323996254?t=s92jVBKH81hHu1XZDDDIwg&s=19
My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.
View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785629244741005525?t=aa-cd8j2wSKWNuS9EY_8Dw&s=19
Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?
Mnafiki zitto anadai zanzibar inapata 4.5 % ya mikopo lakini hasemi zanzibar inalipa hiyo mikopo asilimia ngapi. Alipaswa aseme pia asilimia ngapi ya mikopo inalipwa na zanzibar na asilimia ngapi inalipwa na Tanganyika.
Zito anasema mapato ya muungano Tanganyika wanachukua asilimia 98 alipaswa aweke figure ukusanyaji wa hayo mapati ya muungano Tanganyika yanakusanywa asilimia ngapi na zanzibar ngspi. Je kama ingekuwa nje ya muungano zanzibar wangekusanya zaidi ya hicho wanachopewa je Tanganyika ingekusanya kidogo kuliko inachochukua?
Tuje kwenye ajira za muungano zanzibar wanachukua asilimia 21 ya nafasi zote za ajira za muungano; jiuliza swali hili: je hivi ukitathmini wafanyakazi wa kazi za muungano kama mqjeshi, polisi, uhamiaji nk wanaofanyia kazi zanzibar kama kituo cha kazi wanafikia hiyo asilimia 21? Bila muungano serikali ya zanzibar ingeajiri polisi, jeshi uhamiaji nk kwa idadi inayolingana na ukubwa kwa asilimia 21 ya nafasi za ajira wanazopewa sasa? Jibu lake ni hapana. Kwa wale wasiojua hesabu , chukua idadi ya watumishi wa sasa wa idara za muungano jumla yake halafu chukua wale wanaofanyia kazi zanzibar kama vituo vyao vya kazi, kisha tafuta asilimio yao; hiyo ndiyo ilipaswa kuwa mgao wa nafasi za zanzibar sio asilimia ya sasa 21.
Impact ya kuwapa wanzazibari asilimia 21 ya ajira zote maana yake unakuwa na kabila moja la wazanzibari lenye watumishi asilimia 21 wakati makabila ya Tanganyika hakuna kabila linaloshikilia asilimia 21 ya ajira zote., fikiria watu ambao hawazidi asilimia mbili za idadi ya watanzania wanashikilia asilimia ishirini na moja ya nafasi zote halafu watu kama zitto wanaona sawa. Wasukuma na wingi wao karibia robo ya watanzania wote katika nafasi za utumishi za-muungano wanaweza wasifikie idadi hiyo