Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

=======

MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO

Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe

Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar

========

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785636663323996254?t=s92jVBKH81hHu1XZDDDIwg&s=19

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785629244741005525?t=aa-cd8j2wSKWNuS9EY_8Dw&s=19

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Mnafiki zitto anadai zanzibar inapata 4.5 % ya mikopo lakini hasemi zanzibar inalipa hiyo mikopo asilimia ngapi. Alipaswa aseme pia asilimia ngapi ya mikopo inalipwa na zanzibar na asilimia ngapi inalipwa na Tanganyika.
Zito anasema mapato ya muungano Tanganyika wanachukua asilimia 98 alipaswa aweke figure ukusanyaji wa hayo mapati ya muungano Tanganyika yanakusanywa asilimia ngapi na zanzibar ngspi. Je kama ingekuwa nje ya muungano zanzibar wangekusanya zaidi ya hicho wanachopewa je Tanganyika ingekusanya kidogo kuliko inachochukua?

Tuje kwenye ajira za muungano zanzibar wanachukua asilimia 21 ya nafasi zote za ajira za muungano; jiuliza swali hili: je hivi ukitathmini wafanyakazi wa kazi za muungano kama mqjeshi, polisi, uhamiaji nk wanaofanyia kazi zanzibar kama kituo cha kazi wanafikia hiyo asilimia 21? Bila muungano serikali ya zanzibar ingeajiri polisi, jeshi uhamiaji nk kwa idadi inayolingana na ukubwa kwa asilimia 21 ya nafasi za ajira wanazopewa sasa? Jibu lake ni hapana. Kwa wale wasiojua hesabu , chukua idadi ya watumishi wa sasa wa idara za muungano jumla yake halafu chukua wale wanaofanyia kazi zanzibar kama vituo vyao vya kazi, kisha tafuta asilimio yao; hiyo ndiyo ilipaswa kuwa mgao wa nafasi za zanzibar sio asilimia ya sasa 21.

Impact ya kuwapa wanzazibari asilimia 21 ya ajira zote maana yake unakuwa na kabila moja la wazanzibari lenye watumishi asilimia 21 wakati makabila ya Tanganyika hakuna kabila linaloshikilia asilimia 21 ya ajira zote., fikiria watu ambao hawazidi asilimia mbili za idadi ya watanzania wanashikilia asilimia ishirini na moja ya nafasi zote halafu watu kama zitto wanaona sawa. Wasukuma na wingi wao karibia robo ya watanzania wote katika nafasi za utumishi za-muungano wanaweza wasifikie idadi hiyo
 
Ni kweli Zanzibar kuna TRA lakini mapato yanabaki hukohuko, fedha za mikopo mama anagawa robo, lakini zote zinalipwa na Tanganyika, Zitto anatafita Kura za ACT Zanzibar na data za kubuni
Mama alitamka hadharani sehemu ya mikopo inayoenda Zanzibar mfano fedha za covid karibu robo ilienda Zanzibar, mwaka juzi fedha za sherehe za muungano ziligawanywa nusu kwa nusu, Leo utuambie eti ni 2%
 
Huyu kilaza ndio aliahidiwa uwaziri wa fedha na Kikwete, Zanzibar haijachangia kiendesha serikari ya muungano kwa zaidi ya miaka 55 ya muungano.
Hizo takwimu kapewa na wakina Jusa, hajaeleza katika mapato ya muungano Bara inakusanya asilimia ngapi na Zanzibar inakusanya asilimia ngapi.
Hawa ndio wale utasikia wamepewa. PhD kwa maandiko yasiyoeleweka.
Wacha porojo eleza wewe
Hebu zitaje hizo Taasisi angalau 8,ambazo zinafanya hayo makusanyo huko Zanzibar...
Twende kwa data...
Siasa ziwekwe kando...

temeke ina wapiga kura more than a milion, ina wabunge 6, zanzibar in wapiga kura kama laki tano tu, ina wabunge 50 bara, hao wote wanakula posho, na bado wanalaumu bara.
Wewe kweli ni mbumbumbu unafananisha znz na temeke pole sana

Kwa mujibu wa taarifa za mapato yaliyokusanywa na Tra Dar peke yake inachangia asilimia 86.4 ikifuatiwa na Kanda ya kaskazini asilimia 6.8, Kanda ya ziwa asilimia 2.7 nyanda za juu kusini asilimia 1.5 Kanda ya Kati asilimia 1.8 na kusini mashariki 0.8 Kama porojo onyesha kiwango kinachochangiwa na Zanzibar halafu ndio uone hiyo asilimia 2 wanayopewa ni halali au hisani
 
Mkuu Zanzibar nishafika,,,
Safari ya kwanza nilifika Chukwani,Safari ya pili nikakaa Airport, kona ya kuelekea baraza la wawakilishi...
Kariakoo kwenye mabembea,Shamba,Fumba,Kwa Mchina nishapita hadi hapo Darajani kwenye Masoko.

Bidhaa nyingi Zanzibar zinatoka Uarabuni...yani hadi Simenti mnaagiza kutoka Uarabuni....

Nenda mikoa ya bara ukajionee bidhaa zilivyogharama.

Acha kupotosha watu....
sawa lakini hata kama ni hizo bidhaa, zote huwa zinalipiwa mara mbili - kwa TRA na ZRA
 
Anaongelea TRA ilhali anafahamu fika kuwa Zanzibar wana mamlaka yao ya mapato ZRA, ambayo Zanzbar inatumia mapato yake yote kwa 100%

Kama suala la mapato ni la Muungano, ZRA ni ya kazi gani Zenji? Si iwe tu hiyohiyo TRA...!!?

Kumbe kweli Zitto ni "mpumbavu"
Zitto asipoisemea na kuitetea Zanzibari chama chake kitapotea kama upepo.

Hapa anatetea SUK aliyomo, huu mchezo hautaki hasira, ukiwa na hasira hupati mkate!.
 
Onyesha hiyo 20% ulikoitoa maana hiyo hoja ndio Zito kaioinga hapo Juu Kwa kusema ni 4.5% only.

Pili mbona huzungumzii hoja yake ya kwanza?

Msitafute excuses TRA peke yake inakusanya zaidi ya Bilioni 400 kutoka Zanzibar hapo sijataja taasisi zingine za Muungano mfano Uhamiaji nk.
Bajeti ya Zanzibar ni kiasi gani?
 
Ule uwe mkoa tu maana sisi waTanganyika hatuna mpango wa kuiacha ile ardhi na bahari yake. Ule ni urithi wa baba Nyerere na Karume hauuzwi. Akitokea mtoto anataka kuuza tunamvamia kama nyuki wanavyovamia mvuna asali.
😂😂😂Hawajui hilo, yaani hata hawa wanaojiita wazanzibar siyo wenye lile eneo, yale ni masalia ya biashara tu.. kuiachia ni kama kumwachia mtoto wa kambo urithi wa familia.

Wanaojiona siyo sehemu ya Tanzania warudi kwao uarabuni... Waiache nchi ya watu weusi
 
Uvunje Muungano Kwa maslahi ya nani?

Hoja nzuri Huwa inawasikishwa Kwa upotoshaji na kuhubiri chuki?

Acheni ujinga.

..kila upande unaamini muungano hauwatendei HAKI.

..suluhisho ni Tanganyika na Zanzibar kurudi mezani ili kusuluhisha malalamiko yanayoendelea.

..tatizo ni kwamba haijulikani ni nani atasimamia maslahi ya Tanganyika wakati serikali yake imefutwa.
 
Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

=======

MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO

Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe

Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar

========

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785636663323996254?t=s92jVBKH81hHu1XZDDDIwg&s=19

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.

View: https://twitter.com/MfanyakaziNews/status/1785629244741005525?t=aa-cd8j2wSKWNuS9EY_8Dw&s=19

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Jibu liko wazi kwa maslahi yao. Baba wa Taifa alisema "I can't leave my country to dogs" CCM can't leave our beloved country to dogs.
 
Anaongelea TRA ilhali anafahamu fika kuwa Zanzibar wana mamlaka yao ya mapato ZRA, ambayo Zanzbar inatumia mapato yake yote kwa 100%

Kama suala la mapato ni la Muungano, ZRA ni ya kazi gani Zenji? Si iwe tu hiyohiyo TRA...!!?

Kumbe kweli Zitto ni "mpumbavu"
Mpumbavu mamako kuzaa bwege km weww
 
Hebu c
Anaongelea TRA ilhali anafahamu fika kuwa Zanzibar wana mamlaka yao ya mapato ZRA, ambayo Zanzbar inatumia mapato yake yote kwa 100%

Kama suala la mapato ni la Muungano, ZRA ni ya kazi gani Zenji? Si iwe tu hiyohiyo TRA...!!?

Kumbe kweli Zitto ni "mpumbavu"
Hebu nichanganulie kidogo hapa mkuu

T- Tanzania
ZRA - Zanzibar
Je, ya Tanganyika iko wapi? That means TRA ni overall , je TRA hai operate Zanzibar?

Swali lingine nje ya hilo kwanini mtu akitoka na mzigo Zanzibar pale bandarini lazima alipe ushuru, wakati huo huo anayetoka Tanzania bara kwenda visiwani halipi?
 
Matajiri ni wapemba waarabu.
Generally tuseme waarabu,wazanzibari hawana hurka ya maendeleo,hawapendi kusoma na wanapenda umwinyi.
Zanzibar kama ingeachwa yenyewe ingebaki MASIKINI KUTUPWA.
Nenda Zanzibar halafu ukaone maisha yao.
Mtu anafanya kazi akishapata hela ya kula basi anarudi nyumbani kupumzika,elimu hawataki wanashikilia kusomeshana elimu ya majini tu.
Kaka leo umenifungua macho! kumbe ndio maana 'wadau' wakaamua katika utawala huu wa MAMA, tujitahidi kuwapa taugh WAZENJ angalau na wao wasogee ili twende kwa umoja wetu! Hatuwezi kuwa na watu ndani ya nchi yetu wenye hali mbaya kama unayoisema, halafu tukabaki salama!
 
Hebu c
Hebu nichanganulie kidogo hapa mkuu

T- Tanzania
ZRA - Zanzibar
Je, ya Tanganyika iko wapi? That means TRA ni overall , je TRA hai operate Zanzibar?

Swali lingine nje ya hilo kwanini mtu akitoka na mzigo Zanzibar pale bandarini lazima alipe ushuru, wakati huo huo anayetoka Tanzania bara kwenda visiwani halipi?

..Huo ni uonevu kwa Tanganyika.

..Tanganyika anastahili kuwa na mamlaka yake ya kukusanya mapato yake.

..wanaolipishwa ushuru kwa kuleta mizigo toka Zanzibar maana yake hawakulipa ushuru walipoteremsha mzigo Zanzibar.

..kumekuwa na jitihada za muda mrefu za wafanyabiashara wasio waaminifu kujaribu kutumia Zanzibar kama uchochoro wa kukwepa kulipa kodi.

..Zaidi haileti mantiki mfanyabiashara anayetaka kuuza bidhaa Tanganyika, aagize bidhaa toka nje halafu azipeleke Zanzibar kwanza, badala ya kuzileta moja kwa moja Tanganyika.
 
Zanzibar inajitegemea Kwa Mapato yake ,kinachotoka Bara kwenda huko ni 2% tuu na wakati Bara mnakomba 98% ya Mapato yanayotokana na Muungano zikiwemo zaidi ya Bilioni 400 ambazo TRA anakusanya Bado taasisi zingine kama uhamiaji ,Utalii nk.
hivi mapato yanayotokana na muungano ni yepi? tuelewesheni ambayo zanzibar inastahili.
 
Back
Top Bottom