Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

..Huo ni uonevu kwa Tanganyika.

..Tanganyika anastahili kuwa na mamlaka yake ya kukusanya mapato yake.

..wanaolipishwa ushuru kwa kuleta mizigo toka Zanzibar maana yake hawakulipa ushuru walipoteremsha mzigo Zanzibar.

..kumekuwa na jitihada za muda mrefu za wafanyabiashara wasio waaminifu kujaribu kutumia Zanzibar kama uchochoro wa kukwepa kulipa kodi.

..Zaidi haileti mantiki mfanyabiashara anayetaka kuuza bidhaa Tanganyika, aagize bidhaa toka nje halafu azipeleke Zanzibar kwanza, badala ya kuzileta moja kwa moja Tanganyika.
Nimekusoma ,

Lakini sidhani kama Tanganyika kaonewa ni kama mpango kazi haiwezekani likawa halikuonekana hili

upande wa wafanya biashara nimeelewa fact yako, ila bado kuna wale local business partners bado itahitaji kufanya biashara kuna namna kunatakiwa kurekebishwa , haikai sawa kama nchi moja ila ukitaka kwenda huku inalipa ushuru
 
hivi mapato yanayotokana na muungano ni yepi? tuelewesheni ambayo zanzibar inastahili.
Mikopo/miradi inayofadhiliwa na world bank inayokuja kwa jina la Tanzania ,inaweza ikawa donor fund project, n.k kwa kuwa Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja ambayo ni Tz
 
Nimekusoma ,

Lakini sidhani kama Tanganyika kaonewa ni kama mpango kazi haiwezekani likawa halikuonekana hili

upande wa wafanya biashara nimeelewa fact yako, ila bado kuna wale local business partners bado itahitaji kufanya biashara kuna namna kunatakiwa kurekebishwa , haikai sawa kama nchi moja ila ukitaka kwenda huku inalipa ushuru

..ukiachilia mbali kutokuwepo kwa serikali ya Tanganyika, muungano unaendeshwa kienyeji-enyeji mno.

..hoja alizotoa Zitto Kabwe ni uthibitisho wa uendeshaji wa muungano wetu usiofuata taratibu.

..kuna mapesa mengi yanatoka serikali ya muungano upande wa Tanganyika kwenda Zanzibar. Mapesa hayo yanapelekwa nje ya taratibu. Halafu baadae Zanzibar wanalalamika kwamba hawapati swahili yao iliyowekwa kisheria.

..Mfano mdogo, Tanesco inaposamehe deni la umeme la Zanzibar, serikali inakuwa imetumia kifungu gani cha sheria ya mgawanyo wa mapato kati ya Muungano, Tanganyika, na Zanzibar?
 
😂😂😂Hawajui hilo, yaani hata hawa wanaojiita wazanzibar siyo wenye lile eneo, yale ni masalia ya biashara tu.. kuiachia ni kama kumwachia mtoto wa kambo urithi wa familia.

Wanaojiona siyo sehemu ya Tanzania warudi kwao uarabuni... Waiache nchi ya watu weusi
Waarabu janja janja mingi. Siku tunatoa mguu hapo utawaona. Baada ya kupinduliwa hawakutarajia Nyerere na Karume watafanya mambo chap chap namna ile, walitarajia kujipanga na kurudi, mpaka leo ukute kuna waarabu wanaamini Zanzibar ni ya babu zao na watarudi kuimiliki.
 
Waarabu janja janja mingi. Siku tunatoa mguu hapo utawaona. Baada ya kupinduliwa hawakutarajia Nyerere na Karume watafanya mambo chap chap namna ile, walitarajia kujipanga na kurudi, mpaka leo ukute kuna waarabu wanaamini Zanzibar ni ya babu zao na watarudi kuimiliki.
Zanzibar is ours
 
😂😂😂Hawajui hilo, yaani hata hawa wanaojiita wazanzibar siyo wenye lile eneo, yale ni masalia ya biashara tu.. kuiachia ni kama kumwachia mtoto wa kambo urithi wa familia.

Wanaojiona siyo sehemu ya Tanzania warudi kwao uarabuni... Waiache nchi ya watu weusi
Wewe ndio wale wale mbumbumbu huna ujualo pole sana
 
Sawa na mkoa? Wewe kweli ni wale wale mbumbumbu pole sana

..Waznz kama mna nia ya dhati ya kupata haki zenu ndani au nje ya muungano basi waungeni mkono Chadema kwani ndio wenye watu huku Tanganyika.

..Wanaowanyima Waznz haki zao ni Ccm. Na Ccm hushirikiana na baadhi ya Waznz kama Samia Suluhu, Hussein Mwinyi, na wengine.

..Waznz wamekuwa wakilalamika kuwa vikosi vya Jwtz hupelekwa Znz kila wakati wa uchaguzi. Wanawalaumu Watanganyika. Lakini sote tunajua Hussein Mwinyi ndiye aliyekuwa Waziri wa Ulinzi mwenye dhamana na Jwtz kwa muda mrefu. Je, Jwtz wakifanya vurugu Znz, Hussein Mwinyi hawajibiki au hastahili lawama?
 

Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

=======

MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO

Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe

Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar

========

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Mfanyakazi Online Media
Kwani wao ni % ngapi ya Population?
 
Kwani wao wanachangia asilimia ngapi ya pato
Na kama tunawaonea basi muungano uvunjike tu
 
Mkuu Zanzibar nishafika,,,
Safari ya kwanza nilifika Chukwani,Safari ya pili nikakaa Airport, kona ya kuelekea baraza la wawakilishi...
Kariakoo kwenye mabembea,Shamba,Fumba,Kwa Mchina nishapita hadi hapo Darajani kwenye Masoko.

Bidhaa nyingi Zanzibar zinatoka Uarabuni...yani hadi Simenti mnaagiza kutoka Uarabuni....

Nenda mikoa ya bara ukajionee bidhaa zilivyogharama.

Acha kupotosha watu....
Picha ya kanakwamba ni muumini wa Muungano,,,yafuatayo kwangu ni chukizo...
  • Kwenda Zanzibar ni lazima uwe na kitambulisho kabla ya kupanda boti.
  • Uhuru finyu wa kidini, hasa kwa siye wa dhehebu tofauti.
  • Kuna baadhi ya kazi za taaluma hauruhusiwi kuzifanya Zanzibar kama wewe ni Mbara ,,
 
sawa lakini hata kama ni hizo bidhaa, zote huwa zinalipiwa mara mbili - kwa TRA na ZRA
Mkuu,
Hata Bara kuna malipo ya kodi na ushuru mara mbili mbili....
Wenye biashara wanalipa TRA,Manispaa na serikali za kata...

Pia kumbuka Zanzibar wana mkataba wa soko huria na Oman na Dubai...bidhaa zaingia kwa kodi pungufu kuliko Bandari ya Dar.
 
Wacha porojo eleza wewe



Wewe kweli ni mbumbumbu unafananisha znz na temeke pole sana
Yani shida yenu ndiyo hapo elimu duni...
Weka data hapo za kuonesha makusanyo yenu na siyo ngonjera....

Wilaya ya Temeke ndiyo ina miliki chanzo kikubwa cha mapato Tanzania, unataka uifananishe na Zenji.
Kwa kipi hasa labda....?

Mzuri wa kutusi ila elimu, sifuri.
 
Mnafiki zitto anadai zanzibar inapata 4.5 % ya mikopo lakini hasemi zanzibar inalipa hiyo mikopo asilimia ngapi. Alipaswa aseme pia asilimia ngapi ya mikopo inalipwa na zanzibar na asilimia ngapi inalipwa na Tanganyika.
Zito anasema mapato ya muungano Tanganyika wanachukua asilimia 98 alipaswa aweke figure ukusanyaji wa hayo mapati ya muungano Tanganyika yanakusanywa asilimia ngapi na zanzibar ngspi. Je kama ingekuwa nje ya muungano zanzibar wangekusanya zaidi ya hicho wanachopewa je Tanganyika ingekusanya kidogo kuliko inachochukua?

Tuje kwenye ajira za muungano zanzibar wanachukua asilimia 21 ya nafasi zote za ajira za muungano; jiuliza swali hili: je hivi ukitathmini wafanyakazi wa kazi za muungano kama mqjeshi, polisi, uhamiaji nk wanaofanyia kazi zanzibar kama kituo cha kazi wanafikia hiyo asilimia 21? Bila muungano serikali ya zanzibar ingeajiri polisi, jeshi uhamiaji nk kwa idadi inayolingana na ukubwa kwa asilimia 21 ya nafasi za ajira wanazopewa sasa? Jibu lake ni hapana. Kwa wale wasiojua hesabu , chukua idadi ya watumishi wa sasa wa idara za muungano jumla yake halafu chukua wale wanaofanyia kazi zanzibar kama vituo vyao vya kazi, kisha tafuta asilimio yao; hiyo ndiyo ilipaswa kuwa mgao wa nafasi za zanzibar sio asilimia ya sasa 21.

Impact ya kuwapa wanzazibari asilimia 21 ya ajira zote maana yake unakuwa na kabila moja la wazanzibari lenye watumishi asilimia 21 wakati makabila ya Tanganyika hakuna kabila linaloshikilia asilimia 21 ya ajira zote., fikiria watu ambao hawazidi asilimia mbili za idadi ya watanzania wanashikilia asilimia ishirini na moja ya nafasi zote halafu watu kama zitto wanaona sawa. Wasukuma na wingi wao karibia robo ya watanzania wote katika nafasi za utumishi za-muungano wanaweza wasifikie idadi hiyo
Kaka umejaribu kufafanua vzr. ila kwakusaidia tu ni kwamba, suala la 21% ni la kisheria tu ila utekelezaji wake haujawahi kufanyika kwa kiwango hicho! nenda kwenye taasisi zote za muungano utaniambia, Mchengerwa alitaka kututania lkn. akashindwa! jamani muwe na amani, hata kama Rais ni Mzanzibari, Watanganyika bado tupo!
 
Yani shida yenu ndiyo hapo elimu duni...
Weka data hapo za kuonesha makusanyo yenu na siyo ngonjera....

Wilaya ya Temeke ndiyo ina miliki chanzo kikubwa cha mapato Tanzania, unataka uifananishe na Zenji.
Kwa kipi hasa labda....?

Mzuri wa kutusi ila elimu, sifuri.
Kwa hiyo wewe na hiyo elimu yako unafananisha Zanzibar na temeke? Pole sana wewe kweli ni mbumbumbu
 
Back
Top Bottom