Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Zitto Kabwe: Tanzania Bara (Tanganyika) inachukua 98% ya Mapato yote ya Muungano, Zanzibar inaambulia 2% tu

Alichoongea ni nini kama sio ratio?
Kwenye pato la muungano Zanzibar inachangia % ngapi na Bara wanachangia % ngapi? jibu kwanza kabla ya kukimbilia kwenye porojo za wanasiasa. Zitto ni mchumi so nina uhakika anaujua ukweli ila anatafuta kiki tu
 
Anaongelea TRA ilhali anafahamu fika kuwa Zanzibar wana mamlaka yao ya mapato ZRA, ambayo Zanzbar inatumia mapato yake yote kwa 100%

Kama suala la mapato ni la Muungano, ZRA ni ya kazi gani Zenji? Si iwe tu hiyohiyo TRA...!!?

Kumbe kweli Zitto ni "mpumbavu"
Duuuh
 
Kwenye pato la muungano Zanzibar inachangia % ngapi na Bara wanachangia % ngapi? jibu kwanza kabla ya kukimbilia kwenye porojo za wanasiasa. Zitto ni mchumi so nina uhakika anaujua ukweli ila anatafuta kiki tu
kwenye kundi la wahuni huyo hawezi kosa.
 
Kaka leo umenifungua macho! kumbe ndio maana 'wadau' wakaamua katika utawala huu wa MAMA, tujitahidi kuwapa taugh WAZENJ angalau na wao wasogee ili twende kwa umoja wetu! Hatuwezi kuwa na watu ndani ya nchi yetu wenye hali mbaya kama unayoisema, halafu tukabaki salama!
Wajinga sana hao mkuu.
Walikua wanadai wangekua wenyewe basi wangeendelea kama Dubai kisa waarabu,je kuna mwarabu anayekubali kuwekeza sehemu watu wasiojielewa na wavivu.
We mtu anafungua duka akipata tu hela ya kula kafunga.
Uwe unaishi Unguja halafu jishaue uende forodhani au darajani usiku ukachelewa kurudi aisee kama hauna hela ya boda utatembea maana saa tatu tu usiku daladala zimelala.
Kusoma hawataki nimesoma nao hao jamaa aisee wavivu kinyama kusoma na huwa hawataki kazi za kusumbuka.
Kama kweli Zanzibar wachapakazi basi Bakhresa angewekeza Zanzibar,na kama kweli Zanzibar kuna room of adjustment basi wangewekeza huko.

Halafu imagine mtu anaropoka eti Zanzibar inatubeba.
 
Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

=======

MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO

Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe

Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar

========

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Mfanyakazi Online Media
Naunga mkono hoja ya Tito Tanzania bara inachuwa mapato mengi kuliko Zanzibar wanaopaswa kulalamika ni Wa-Zanzibar sio WA-Tanganyika.
 
Kama watu hawautaki muungano ,Waheshimiwe maamuzi yao
 
Kwa hiyo wewe na hiyo elimu yako unafananisha Zanzibar na temeke? Pole sana wewe kweli ni mbumbumbu
Yani check ulivyokuwa hauna hoja, umebaki kusema mbumbu...😂😂
Ukiona elimu ni gharama ,jaribu ujinga...Banza hakukosea...
 
Hii dunia inachekesha sana.
Kabla hayo kusemwa itabidi tujadili mambo kama mawili kama si matatu;
1)Je Zanzibar inakusanya ama inazalisha kiasi gani cha mapato?
2)Je hiko kiasi cha mapato ukikiingiza pamoja na kinachokusanywa bara ni asilimia ngapi kwa kinachokusanywa bara?
3)Je ZRA kazi yake nini huko Zanzibar na je haibaki na mapato?
4)Je Tanzania bara haitoi ruzuku serikali ya Zanzibar?

Mwenye uelewa atujibu haya maswali.

Na hawa wazanzibari waache kulalamika hovyo,kuna kero nimeziona Zanzibar ambazo ni uonevu wa wazi na huku bara hatukuzipigia kelele;
1)Kwenda Zanzibar lazima kukata ticket uwe na kitambulisho cha aina yeyote.
2)Kuna kazi Zanzibar huwezi kupata kama hauna kitambulisho cha Mkazi wa Zanzibar,ilhali huku bara Mzanzibari anaweza akapata kazi bila kitambulisho cha NIDA,ila Zanzibar NIDA hawataki wanataka kitambulisho cha mkazi wa Zanzibar.
3)Leseni ya udereva ya bara haina nguvu tena huwenda isifanye kazi huko Zanzibar,ila huku bara leseni ya udereva kutoka kisiwani ina nguvu vizuri tu.
4)Kuna utata mbara akitaka kununua ardhi Zanzibar,ila Mzanzibari kununua ardhi bara ni kitu cha kawaida.
5)Zanzibar udini mwingi sana yani kuna uhuru mdogo wa kuabudu kwa dini ya upande wa pili,japo mimi muislam ila nimeliona hili.

Sasa atakayekuja kulalamika tunaionea Zanzibar namuona hana akili ama ni kichaa anahitaji matibabu ya akili.
 
Yani check ulivyokuwa hauna hoja, umebaki kusema mbumbu...😂😂
Ukiona elimu ni gharama ,jaribu ujinga...Banza hakukosea...
Anabisha nini huyo!?
Temeke na Zanzibar hazina tofauti sana kama anabisha alete uthibitisho sio kutukana tu.
 
Anabisha nini huyo!?
Temeke na Zanzibar hazina tofauti sana kama anabisha alete uthibitisho sio kutukana tu.
Nawaomba Data za Makusanyo ya Zanzibar,na uchangiaji wake katika pato la Taifa....
Halafu aje alinganishe na mapato ya manispaa ya Temeke, manispaa yenye Bandari kubwa Tanzania....anabaki kutukana tu hapa...

Hana data kazi kutukana....
 
Zitto alipaswa kujenga hoja yake kwa kuonyesha kwanza,
1. Zanzibar wanachangia asilimia ngapi kwenye mapato ya muungano (huwezi kusema wanapewa 2% lakini hapo hapo ukaogopa kusema kuwa wanachangia chini 1%).

2. Kwanini Zanzibar wanafaidika na pesa za mapato yasiyo ya muungano kutoka mapato ya Tanganyika.

3. Kiwango cha faida ya pesa za miradi mbalimbali iliyo ya muungano na isiyo ya muungano kinachoelekezwa Zanzibar.
 
Nawaomba Data za Makusanyo ya Zanzibar,na uchangiaji wake katika pato la Taifa....
Halafu aje alinganishe na mapato ya manispaa ya Temeke, manispaa yenye Bandari kubwa Tanzania....anabaki kutukana tu hapa...

Hana data kazi kutukana....
Hajielewi huyo.
Tufananishe kiuzalishaji Temeke ndio wilaya yenye viwanda vingi kwa mkoa wa Dar es salaam kuanzia keko kuja mpaka huku viwanda vidogo Mbagala.
Na kuna makampuni kibao ya usafirishaji kama TRH na mengineyo.
 
Zito ni msomi wa uchumi, Ratio au uwiano wa Idadi ya watu ni upi kati ya bara na Zanzibar

Zitto Kabwe amewashangaa wale ambao wanahoji kuhusu Muungano hasa huku Bara akisema hawajui kitu kwani wanaotakiwa kuhoji ni Wazanzibar.

Zitto ambae ni mtaalamu wa kujenga hoja Kwa takwimu amesema Kwa masuala ya Muungano yanayohusu Mapato, Zanzibar hupata asilimia 2% pekee na ndio imekuwa mojawapo ya Changamoto za Muungano Kwa miaka Mingi.

Aidha Kwa wale msiojua TRA inakusanya zaidi ya Bilioni 400 Kila mwaka kutoka Zanzibar ambazo Kwa sehemu kubwa zinatumika Bara.

=======

MAPATO KARIBU YOTE YA MUUNGANO HUCHUKULIWA NA TANZANIA BARA - ZITTO

Zitto Kabwe amesema Mapato yote ya Muungano kutoka mambo ya muungano, Zanzibar inatumia 2% tu, wakati Tanganyika inatumia 98%. Ziada ya mapato ya Muungano ukiondoa matumizi ya muungano yote inachukuliwa na Tanganyika," Zitto Kabwe

Pia ameeleza kuwa Zanzibar wanapata 4.5% tu ya mikopo na misaada ya kimataifa kutoka nje. Zanzibar inaidai Serikali ya Muungano matrilioni ya fedha ambazo hawapati kama mgawo wao. Ukweli ni kwamba hata mtaji wa kuanzisha Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zilitumika fedha za Zanzibar

========

My Take
Naunga mkono hoja ya Zito, Wazanzibar ndio wanapaswa kulaumu na kulalamika kuhusu Muungano kwamba wanapunjwa na sio Tanzania Bara kama wanavyodanganywa na kina Lissu.

Unajaribu kujiuliza, Chadema na Lisu wake na kina Mbowe wanahubiri Mgawanyiko,chuki na Utengano wa Tanzania Kwa maslahi ya nani hasa?

Mfanyakazi Online Media
 
Mikopo/miradi inayofadhiliwa na world bank inayokuja kwa jina la Tanzania ,inaweza ikawa donor fund project, n.k kwa kuwa Zanzibar na Tanganyika ni nchi moja ambayo ni Tz
kwahiyo ulitaka na zanzibar wapate wakati wana rais na serikali yao? na ratial yake je? chukua watanganyika 58m ongeza wazenji 2m gawanya kwa kila mtu uone kama hautapata hiyo ratio, kwanza wanapata kingi sana.
 
Hivi mnajua Zanzibar zaidi ya asilimia 90 ya shehia zinafikika kwa lami? Yaani shehia ni mlinganisho wa kitongoji kwa huku bara...

Zote zile ni hela za bara, zile hela wakilalamika kdg wanapewa gawio...

Hivyo basi, Muungano haukomi, yaani hata kitokee nini, jasho letu lipo jingi sana huko , hamuwezi kutuchuna afu mje mvunje ndoa.
 
We jamaa bwana.
Kwahiyo hawawezi wakala pesa zetu kizembe😂😂😂😂😂.
 
Back
Top Bottom