Mkalukungone Mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 3,141
- 7,205
"Thamani ya uhai katika nchi yetu inapotea. Matendo ya utekaji wa watu kama vile kina Mdude, Kina Soka, Kina Sativa na watu wengine inawafanya watu kama watendaji wa Vijiji kuona kwamba wanaweza nao pia kukamata, kutesa mpaka kuua." Amesema Zitto.
Zitto amebainisha kuwa Ibara ya 14 ya Katiba ya Tanzania inasisitiza kuhusu kulinda Uhai wa binadamu, akiwataka watendaji na watumishi wote wa serikali na vyombo vya dola kuheshimu Katiba ya nchi sambamba na kuhakikisha vyombo vya dola ikiwemo Polisi kunakuwa sehemu salama kwa raia.
Katika maelezo yake, Zitto amebainisha kuwa ikiwa chama hicho kitashika dola, kitahakikisha kinaondoa mamlaka ya Kijeshi kwa baadhi ya vyombo vya serikali ikiwemo mamlaka ya wanyamapori TAWA na Mamlaka ya Misitu nchini TFS, akizitaja mamlaka hizo kuwa miongoni mwa zile zinazotuhumiwa kutesa wananchi kinyume cha sheria na taratibu za nchi.