Zitto Kabwe tumia vizuri hii fursa ya CHADEMA kususia chaguzi zote nchini

Zitto Kabwe tumia vizuri hii fursa ya CHADEMA kususia chaguzi zote nchini

Wahenga walishasema siku zote adui yako muombee njaa, pia wakasema wakati wa shida ndiyo muda wa kujipatia fursa kwa wenye uelewa mkubwa.

Baada ya Chadema kupitia mwenyekiti wake kutangaza kususia chaguzi zote nchini ,hii ni fursa adhimu kwa chama cha ACT Wazalendo kujiimarisha na kuwa chama kikuu cha upinzani nchini kufikia uchaguzi mkuu mwaka 2020.!

Ikumbukwe kuwa Zito Kabwe alifukuzwa kinyama Chadema baada ya kuhoji uenyekiti wa milele wa Mbowe ,hivyo hana sababu yoyote ya kuwaonea huruma wala kuungana na Chadema katika kipindi hiki kigumu wanachopitia .

Wazalendo na wapenda mabadiliko wa nchi yetu wanatuma salamu kwa Zito Kabwe na kumwambia kuwa nyota ya mafanikio kwake sasa inawaka na nyota ya chadema inazima rasmi.

Zito Kabwe huko uliko anza kushangilia na kuwazomea wabaya wako Chadema huku ukijiimarisha kisiasa na ukijiandaa kuwa kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni mwaka 2020.
Ikumbukwe kuwa hamna aliyewahi kushindana na Zito Kabwe alafu akabaki salama, kususia chaguzi zote ndiyo kifo na mwisho wa Chadema.

Kwa heri ,Mbowe ,kwa heri Chadema na karibu ACT Wazalendo na karibu Zito Kabwe kama kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani bungeni.
Huyu jamaa anaupeo Mdogo sana wa kifikiri bora kipara kipya unajua kabisa huyu anajitambua sema anajitoa ufahamu


Sent using Jamii Forums mobile app
 
DJ dikteta Mbowe hataki wenzake waende bungeni baada ya yeye kushindwa vibaya kule Hai
 
Back
Top Bottom