Zitto Kabwe: Ubadhirifu wa 2020/21 ni mara mbili ya mwaka uliotangulia. Kulikuwa na ubadhirifu kwa jina la uzalendo

Zitto Kabwe: Ubadhirifu wa 2020/21 ni mara mbili ya mwaka uliotangulia. Kulikuwa na ubadhirifu kwa jina la uzalendo

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
1650491737485.png

Kuna watu walikuwa wanajifanya wazalendo mpaka kupiga wengine risasi. Lakini ni wazalendo gani wanampiga mtu risasi akiwakosoa, wanataifisha pesa za watu kwenye bank, waharibu biashara na uwekezaji wa watu, wanajipendelea na kutumia pesa ya umma kujenga kwao na kufikia mpaka kuweka mbuga, wanaiba kura kwa kupitia usalama na Polisi, wanatumia pesa nje ya budget, wana rekodi maadui wao wa kisiasa, wanauwa waandishi wa habari wanao wapinga, wanadanganya Watanzania kuhusu covid……
 
Huu ufisadi wa Magufuli ndio unamuuma sana Zitto zaidi ya ule wa Escrow, EPA nk

Huyu mmoja alikuwa anaiba huku anajiita mzalendo ili kutudanganya, yule mwingine alikuwa anaiba kimya kimya, hawa kwangu wote ni wezi tu.

Najua Zitto anashindwa kumlaumu yule mmoja kwasababu aliwahi kusema huyo alikuwa ni sawa na baba yake, anamfichia aibu.

Anajua kulalamika kama vile ni mzalendo wa kweli, kumbe akiambiwa habari za Katiba Mpya naye hataki kuzisikia. Maana yake huyu mnafiki anataka tuendelee kuibiwa na marafiki zake ili nae agaiwe, ila tukiibiwa na wale wasio rafiki zake ndio anaumia.

Kuendelea kumshangilia huyu tapeli na hizi kelele zake za kila siku kwa Magufuli ni kujidumaza akili tu, anawazubaisha wajinga, na kwa ujinga wao wanazidi kumshangilia.
 
Hii nchi bila upigaji barabara zote za vijijini zingekua na lami. Tiba ya cancer kila mkoa, kila kata ingekua na affordable homes to rent. Unapata one bedroom flat kwa laki moja. Mishahara ya kima cha chini kuanzia laki sita. Tatizo la maji lisinge kuwepo.
 
Najua Zitto anashindwa kumlaumu mmoja kwasababu aliwahi kusema huyo alikuwa ni sawa na baba yake, anamfichia aibu.

Anajua kulalamika kama vile ni mzalendo wa kweli, kumbe akiambia habari za Katiba Mpya naye hataki kuzisikia, maana yake huyu mnafiki anataka tuendelee kuibiwa na marafiki zake ili nae agaiwe, ila tukiibiwa na wale wasio rafiki zake ndio anaumia.

Kuendelea kumshangilia huyu tapeli na hizi kelele zake za kila siku kwa Magufuli ni kujidumaza akili tu, anawazubaisha wajinga.
Huyu anatumika vibaya, Watanzania wa leo siyo wa jana. Tunajua kupambanua mambo, heri huyo anayemwita fisadi huku yaliyofanyika yanaonekana, hawezi zungumzia awamu ya nne wala ya sita kwa sababu ndiyo wanaofadhiri proganda zake ili kutusahaurisha uovu wao, Mimi binafsi sidanganyiki na hawa walamba asali.
 
Hii nchi bila upigaji barabara zote za vijijini zingekua na lami. Tiba ya cancer kila mkoa, kila kata ingekua na affordable homes to rent. Unapata one bedroom flat kwa laki moja. Mishahara ya kima cha chini kuanzia laki sita. Tatizo la maji lisinge kuwepo.
Mambo mazuri sana haya.

Sasa tufanyeje mkuu 'Sky Eclat.' ili tuyapate haya!

Naona sasa "kula ni kwa urefu wa kamba", wengine wanasema wapo wanaokula "free range", hakuna kamba yoyote inayowazuia kula.
 
Mambo mazuri sana haya.

Sasa tufanyeje mkuu 'Sky Eclat.' ili tuyapate haya!

Naona sasa "kula ni kwa urefu wa kamba", wengine wanasema wapo wanaokula "free range", hakuna kamba yoyote inayowazuia kula.
Kwanza kabisa kunahitajika utawala wa haki na sheria ambao msingi wake ni Katiba ambayo kila anaevunja sheria anawajibishwa.

Kule Uingereza Boris Johnson, Waziri Mkuu alifanyiwa party ofisini kwake kipindi cha lock down. Jana amelazimika kuomba msamaha hadharani akiwa bungeni na bado kuna jitihada za kumuondoa madarakani. Dhana yao kubwa ni kuwa akiwa kama Waziri Mkuu anajua sheria na alipaswa kuziheshimu. Kuna waliofiwa na ndugu na jamaa kipindi cha lock down na walishindwa kuhudhuria mazishi iweje yeye afanyiwe party.

Tukifika kwenye level ya kuweza kuwawajibisha viongozi wa juu, wachini pia watakua a nidhamu.
 
Huu ufisadi wa Magufuli ndio unamuuma sana Zitto zaidi ya ule wa Escrow, EPA nk

Huyu mmoja alikuwa anaiba huku anajiita mzalendo ili kutudanganya, yule mwingine alikuwa anaiba kimya kimya, hawa kwangu wote ni wezi tu.

Najua Zitto anashindwa kumlaumu yule mmoja kwasababu aliwahi kusema huyo alikuwa ni sawa na baba yake, anamfichia aibu.

Anajua kulalamika kama vile ni mzalendo wa kweli, kumbe akiambiwa habari za Katiba Mpya naye hataki kuzisikia. Maana yake huyu mnafiki anataka tuendelee kuibiwa na marafiki zake ili nae agaiwe, ila tukiibiwa na wale wasio rafiki zake ndio anaumia.

Kuendelea kumshangilia huyu tapeli na hizi kelele zake za kila siku kwa Magufuli ni kujidumaza akili tu, anawazubaisha wajinga, na kwa ujinga wao wanazidi kumshangilia.
Zitto ni mdini sana na ni mnafiki aliyepitiliza chadema walifanya jambo jema kumtema mchawi huyu.
 
Hii nchi bila upigaji barabara zote za vijijini zingekua na lami. Tiba ya cancer kila mkoa, kila kata ingekua na affordable homes to rent. Unapata one bedroom flat kwa laki moja. Mishahara ya kima cha chini kuanzia laki sita. Tatizo la maji lisinge kuwepo.
Mabomba yangetoa maziwa,sukari,mafuta ya kula na petrol tungepewa bure,bahari ingechimbwa mpaka kigoma bila kusahau kila kijana angejengewa nyumba upewe mtaji na kulipiwa mahari.
 
Kama Magufuli aliiba hivyo na bado akatuletea maendeleo yote yale; wao awamu ya nne hawakuiba mbona walishindwa kutufanyia chochote cha maana?

Awamu ya sita ambayo haiibi, imeongeza kodi, tozo, imekopa kwa namna isiyomithilika na bado inachukua misaada mbona haijafanya hata 25% tu ya aliyoyafanya Magufuli kwenye mwaka wake wa kwanza?

We need more leaders like Magufuli kuliko hawa wanaojiita watoto wa mjini wanaoiibia hii nchi bila hata aibu. Makamba acha kumtumia Zitto, njoo wewe mwenyewe utuelezee matatizo ya umeme. Tuelezeeni mna-absorb vipi shocks zinazosababishwa na athari za mgogoro wa Ukraine na Urusi.

Mwenzenu Magufuli alituvusha salama kwenye Covid-19.
 
Bora baba mlevi lakini nyumba yake anaijali huyu pimbi kakalia kumponda magufuli lakini moyo unamsuta ni mjinga na mpumbavu kuamini kwamba kuna wizi mkubwa wakati kila unapoenda unakutana na mradi ulio achwa na marehem kafanya mengi sana ndani ya mda kidogo .Pia watanzania tusivo na akili tumegeuka kwa sasa ni nani anae sikiliza kero za wananchi na kuzitatua hapo hapo ama alivo ondoka marehem ugumu wa maisha umepanda ama umeshuka....?Hebu tuwe na akili kidogo hata na shukrani kwa Jpm.
 
Back
Top Bottom