Ni kweli kabisa Magufuli alikuwa na siasa za uongo:
• Alitudanganya amejenga flyovers
• Alitudanganya amejenga SGR
• Alitudanganya amehamishia serikali Dodoma
• Alitudanganya amejenga vituo vya afya na hospital za willaya na rufaa
• Alitudanganya amekarabati shule kongwe
• Alitudanganya elimu bure
• Alitudanganya kufufua shirika la ndege, reli, na kukarabati na kujenga reli mpya
• Alitudanganya anajenga na kupanua miundombinu ya barabara
• Alitudanganya anajenga bwawa la Mwl Nyerere
• Alitudanganya anapambana na rushwa, mafisadi, wauza madawa ya kulevya na uhakifu mwingine
• Name them
Ni kweli kabisa alitudanganya na aliendesha siasa za uongo na ulaghai.
Nakuuliza katika hayo, kipi cha pekee ambacho watawala waliotangulia hawakufanya?
Daraja la juu la Ubungo, mchakato wake ulianza tangu awamu ya 4. Na je, hilo ni daraja la kwanza kujengwa Tanzania?
Reli ambayo mpaka leo haijafika hata Dodoma, hivi unaifahamu reli ya uhuru (ilijengwa na wakoloni), SGR ya TAZARA, ni kilometer elfu ngapi?
Elimu bure hii ambayo haina hata ubora, waulize waliosoma miaka ya nyuma, ambapo ukiwa university ulikiwa unapewa high learning allowance. Shule za msingi na sekondari, wanafunzi walikuwa wanapewa madaftari, kalamu na vitabu bure.
Hivi unajua kuwa tuliwahi kununua ndege 13 mpya, zote jet, siyo hizi za mchanganyiko na pangaboi? Suala siyo kununua bali ni kufanya shirika liweze kutoa huduma na kutengeneza faida, kitu ambacho mpaka leo tumeshindwa.
Kwenye ujenzi wa barabara za lami, una ujasiri wa kusema wakati wa utawala wa Magufuli ndiyo zimejengwa sana? Awamu ya 4, zilijengwa 12,000km, awamu ya 5 zimejengwa 2,800km. Zipi ni nyingi kwa uelewa wako?
Hilo bwawa la umeme la Nyerere ndiyo la kwanza? Unayajua mabwawa ya Kidatu, Mtera, Kihansi, mitambo ya kufua umeme wa gas?
Kuhusu kupambana na rushwa na ufisadi na wizi, umejiuliza Sabaya anafanya nini jela? Amejiuliza Makonda utajiri wake mkubwa uliupataje? Umesoma report ya CAG juu ya wizi na ufisadi mkubwa uliofanywa na utawala wa Magufuli? Magufuli aliwahadaa watu, na kujifanya mkali sana, watu wakawa waoga, akatumia nafasi hiyo yeye na watu wake kufanya ufisadi mkubwa unaowekwa wazi sasa na report za CAG.
Hospitali za wilaya na vituo vya afya, hivi unafahamu kuwa hospitali na vituo vya afya, vyote vilivyojengwa wakati wa Magufuli, ukiviweka pamoja, thamani yake haifikii hospitali moja tu kama ile ya Mloganzila au Taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete?
Unajua kuwa aliuporomisha ukuaji wa uwekezaji toka 28% mpaka 4%? Unajua kuwa aliporomosha ukuaji wa utalii toka 15% mpaka 3.6%? Unafahamu kuwa alidondisha thamani ya mauzo ya mazao ya kilimo kwa 50%?
Ni mjinga pekee yake, ndiye anaweza kuamini kuwa eti Magufuli alifanya mambo makubwa kuliko utawala mwingine wowote uliopita.
Mtu unazungumzia kufuta ada mashuleni, huzungumzii aliyezijenga. Umazungumzia ukarabati wa hospitali, huzungumzii alizijenga hizo hospitali, wewe kweli ni mzima?
Kama kuna jambo pekee alilofanikiwa kwa kiasi kikubwa Magufuli, basi ni kutengeneza kundi la wajinga ambao hata ukawaonesha guni la mahindi na kibaba, watakuambia kibaba kina ujazo mkubwa zaidi kuliko gunia.