Haina ubishi kwamba kukamatwa kwa Erick Kabendera imekuwa pigo kubwa sana kwa Zitto Kabwe ambaye amekuwa akimtumia Erick kusambaza taarifa zake anazozitengeneza kwa lengo la kuishambulia Serikali ya Rais Magufuli kwenye vyombo vya habari vya Mwananchi Communication Ltd yaani Magazeti ya The Citizen na Mwananchi.
Baada ya Erick kukamatwa Zitto amepaniki na ndiye amekuwa mdomo wa Erick kuliko hata wazazi wake, waandishi wa habari wenzake na waajiri wake ambako amekuwa akiandikia habari zake.
Zitto anatumia mitandao ya Kijamii kila saa kupost kitu fulani ilimradi kuonesha Erick kashikwa kwa kuonewa na kuvidhalilisha vyombo vya dola vya Tanzania.
Yaani Mwananchi Communication wakiandaa ukurasa wa gazeti wanampa kwanza Zitto apost ndipo baadaye Watanzania wengine wanapata gazeti wasome. Mfano ni post yake ya leo tarehe 03 Agosti 2019 aliyoipost saa 6:33 usiku ikionesha ukurasa wa mbele wa gazeti la Citizen na kuweka picha ya Mama yake Erick ameshika tama na kuandikiwa anahuzunika na kuomba mwanae aachiwe.
Zitto ameshasahau kuwa juzi alipost habari iliyowahi kuandikwa na Erick miaka ya nyuma ikieleza kuwa Mama yake aliwahi kumuonya juu ya kuandika habari za kuishambulia Serikali.
Tuache hayo, ukweli ni kwamba Erick Kabendera amekuwa akitumiwa na Zitto kupika habari na kuichafua Serikali na kisha kuzisambaza kwenye vyombo vya habari vya kimataifa likiwemo jarida maarufu la The Economist na mengine.
Upo ushahidi wa hata fedha ambazo Zitto humlipa Erick kwa kazi hiyo na pia upo ushahidi wa vikao vya Zitto na Erick wakipanga namna ya kuidhohofisha Serikali. Nadhani ni suala la muda tu teknolojia itatoa msaada ili Watanzania wawajue vibaraka hawa wanaotumiwa na wazungu kudhohofisha Tanzania.
Wakati Watanzania kwa maelfu wakimiminika kwenye kila post ya Zitto Kabwe na kumshambulia kwa uchochezi anaoufanya wa kujaribu kuponda jitihada za Serikali, inashangaza kuona Zitto Kabwe aliyeshikilia bango kutaka Erick Kabendera aachiwe na Polisi ya Tanzania amekaa kimya juu ya Juliet Dorie Kulangwa ambaye anashikiliwa na Polisi ya Italia kwa tuhuma za kuhusika na dawa za kulevya.
Nadhani hapo kisu kimegusa mfupa.
Kampuni ya Mwananchi Communication ambao ndio wamiliki wa magazeti ya The Citizen na Mwananchi ambako Juliet ni mwandishi wao wamekaa kimya na kufunika habari hii licha ya Juliet kukamatwa takribani mwezi mzima uliopita. Zitto nae analijua jambo hili lakini kabana kimya.
Kwa hiyo kwake Zitto na washirika wake magazeti ya Mwananchi na The Citizen wanaona Polisi Tanzania ikimshikilia Erick Kabendera kwa tuhuma za kuhusika katika uvunjaji wa sheria NI KOSA lakini Polisi Italia ikimshikilia Juliet Dorie Kulangwa kwa kuvunja sheria NI SAWA (double standard) na wanakaa kimya kama vile hakuna mwandishi wa habari aliyepo rumande.
Na suala la Juliet kuhusika na uhalifu limekuwa linazungumzwa siku nyingi na vyombo vya Dola vya hapa nchini vilishaanza kufuatilia, amekwenda kukamatwa Italia. Kama ambavyo Erick Kabendera amekuwa na tuhuma za mashaka ya uraia na upotoshaji wa taarifa kwenye vyombo vya habari tangu siku nyingi hadi juzi kati alipotiwa mikononi mwa vyombo vya dola baada ya kukaidi amri ya kufika Polisi.
Hapa sasa ndio namkumbuka Rais Magufuli aliposema tupo katika vita kubwa na tunaowagusa hawafurahii, na watakuja na mbinu nyingi za kutaka kuturudisha nyuma. Watu hao ndio hawa hawa akina Zitto Kabwe na sasa Mungu anawaumbua.
Maana sasa Zitto aliyesifika kwa kuibua mambo mazito sasa amekuwa mwana udaku kama alivyokuwa Mange Kimambi ambaye baadaye kaona anamaliza nguvu zake bure.
Na gazeti la The Citizen na Mwananchi kama kweli nyie ni wanahabari wenye weledi chapisheni taarifa ya kushikwa kwa mwandishi wenu kule Italia.
Tunawajua sana jinsi wahariri wa magazeti haya wanavyotumiwa na vibaraka na wahalifu, ndio maana wamekuwa wakali dhidi ya Serikali ya Rais Magufuli iliyodhibiti mianya ya upigaji, madawa ya kulevya na vibaraka wanaotumiwa na wazungu kuhujumu nchi.
Mwananchi Communication acheni kumshurutisha Mama yake Kabendera ili aseme na nyie mpate Story. Mama huyo tunamfahamu hawezi kwenda kwenye chombo cha habari kuomba aandikiwe habari hiyo. Yeye alishatimiza jukumu lake la kumuonya mwanae juu ya miendo yake ya kuiandika vibaya Tanzania. Haya mengine mmeyasababisha nyie Mwananchi na Zitto wenu. Mmelikoroga na mjue kulinywa.
Bahati nzuri Serikali hii haibabaishwi na kelele za kina Zitto ndio maana kabaki anabwabwaja kama kuku anayetaka kutaga yai na hakuna mtu anayemjibu. Hata Cyprian Musiba sasa kaachana nae. Anguko baya sana hili.
Serikali gani duniani itamwacha mwandishi wa aina ya Erick Kabendera abaki anatamba kuichonganisha kwenye Jumuiya ya kimataifa na kuivuruga nchi kwa uandishi wa aina ile?
Waandishi wa Habari wakati mwingine mnajiweka pabaya nyinyi wenyewe ama kwa tamaa zenu ama kwa kutojielewa. Sasa Erick yupo ndani hao waliokuwa wanamtuma wakamtoe sasa.
JITAFAKARINI.
Kwa herini ndugu zangu.
_Makala hii imeandikwa na Mwandishi wa Habari, aliyewahi kufanya kazi Mwananchi Communication Ltd._