Zitto Kabwe unapompambania Erick Kabendera mkumbuke na Juliet Dorie Kulangwa anayeshikiliwa na Polisi Italia

We jamaa kweli una njaa,unataka kuteuliwa?
Kuikosoa serikali unakuwa umevunja sheria IPI?
Kwanini hoja za kabendera na gazeti la economist,hazijibiwi kwa hoja?badala yake zinajibiwa kwa mabavu?
Jenerali Ulimwengu,ambaye alishawahi kuwa mbunge,kuna kipindi awamu ya tatu ya Mkapa,alivuliwa Uraia,kisa kuokosoa Serikali.
Mwandishi wa habari Kabendera Shinani,alivuliwa uraia wake miaka ya 96,akajiua.
Mwanaharakati Eyakuze,aliikosoa serikali,akanyanganywa passport yake!
Huu ni mwendelezo tu,
Kila anayeikosoa serikali,utasikia Uhamiaji,wanasema walikuwa wanamchunguza
 
Serikali hii inachafuliwaje wakati safi? Safi tena safi sana. Utaogopaje kukaguliwa meno kama umepiga mswaki?
 
Ndiyo uzuri wa demokrasia inayotoweka. Una uhuru wa kutoa mawazo yako hata kama siyo sahii wala hayakubaliki.
 

Shida ya maccm mkiambiwa ukweli mnasema mnachafuliwa. Hivi aliyeibua uchafu wa akina mikataba ya madini kusainiwa London (waziri Karamagi), tena hotelini si ni zitto huyu huyu na tukampongeza?? Iweje leo akikosoa maovu ya serikali ya sasa iwe nongwa???

Zitto endelea na kutupa mwangaza sisi ambao tuko nje ya ulingo wa siasa
 

Wakati huo akiwa hajala ya mbuzi akaota mapembe na kuonja asali akachonga mzinga.
 
Waliopiga kampeni na kumteua huko wanamwita kachanganyikiwa! Sasa huyu kusema bull dozer ni shida??
 
Mwandishi wa habari ni raia wa kawaida wa Tanzania, kama ana makosa ana kamatwa tu, mbona raia wengi tuna kamatwa na polisi nchini?,ni kawaida, cha msingi waende mahakamani wakajipange huko,tatizo kubwa naliona hapa waandishi wa habari wengi wamejiingiza kwenye siasa na uana harakati kama njia ya kutoka na kupata umaaufu ambao hauna maana hivyo kusahau maadili ya kazi yao, wakikamatwa wanasiasa wana kuja kuanza kuwa tetea na kutuaminisha kuwa wameonewa, ni mahakama pekee ndio inaweza thibitisha kuwa umeonewa au la.
 
Hovyooooo!
 
Kwani ni kosa kufanya siasa?, Kabendera amekamtwa kwa kufanya siasa?
 
Mwananchi inapaswa kumkingia kifua huyo mwandishi wake aliyekamatwa Italia kwa tuhuma za madawa ya kulevya.
 
Well spoken,hata katika nchi zilizo endelea mwandishi wa aina ya huyo Kabendera hawezi kuwa mtaani anatamba.
 
Kwani ni kosa kufanya siasa?, Kabendera amekamtwa kwa kufanya siasa?
Siasa sio kosa , kufanya siasa kwa mazingira ya uandishi wa habari hapo kuna shida maana utakuwa na upande , mbaya zaidi utaletewa habari za kisiasa una publish bila kujua madhara yake, kama ukiwa ni mfuasi wa chama fulani na ni mwandishi wa habari basi kuwa positive , kosoa serikali positively inapofanya makosa, na tuambie nini kifanyike ili mambo hayo yasijirudie, sio tu kuegemea kwenye negativity kila siku kila leo miaka yote , una mislead watu kwa maslahi yako binafsi huo ni ubinafsi kwa taifa, watu wengi tuna shindwa kuelewa kuwa nchi yetu ni hii, hata ukiandika mabaya kiasi gani hayana maana , tuweni muda mwingine positive kwa nchi yetu, at the end of the day sisi bado tutabaki kuwa watanzania .
 
hakuna sababu ya kumshililia kama si raia akiachiwa ataenda huko kwao na mchezo umeisha. SIONI SABABU YA KUMNYIMA DHMANA.
 
Makala zake kule The Economist alikuwa anaficha jina wote sawa kea hilo, Lakini 'motive' tofauti.
Kwahyo ndivo mlivomtesa aseme kua alikua yeye.je unaamini hayoyote ndo msingi waushindi kwake mahakamani?
 
Hawezi kuteuliwa kwani hanajina lake kamili hapa
 
Dah! Julieth Kulangwa kumbe ameingia kwenye biashara ya kuuza ngada, binti mrembo kadanganywa na nani?
 
Sasa mwandishi wa habari na muuza unga vinahusiana vipi?
Zitto ana uthubutu kuliko wapinzani wengine
Anaikosoa serikali kwa hoja na vithibitisho
Sasa mlitaka serikali isikosolewe? Yesu alikoselewa alipokuja duniani sasa serikali ya awamu hii tu ndio isikosolewe kwa lipi haswa?
Kubalini kukosolewa mrekebishe penye uhitaji tusonge mbele
Praise team mna shida mahali! Safisheni tongotongo moune yaliyopo mbele yenu mtajua Kwa nini wanaokosoa wanakosoa
Stop being naive!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…