Zitto Kabwe: Uwanja wa Ndege wa Songwe (Mbeya) Upewe Jina la John Mwakangale Ili Kuenzi Mchango wake Katika Mapambano ya Kudai Uhuru wa Tanganyika

Huyu dingi lazima ataeleza jinsi Kleist Sykes alivyomsaidia Mwakangale.
Mama...
Soma historia hiyo hapo chini vipi TANU iliingia huko:

KUMBUKUMBU ZA UHURU: ABBAS MAX WA IRINGA (1918 - 1993)

Abbas Max ana historia ya kusisimua sana kama ilivyo kwa wazalendo wengi waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini kwa bahati mbaya historia imewasahau.

John Iliffe mwanahistoria nguli aliyeiokoa historia ya Tanganyika amepata kusema kuwa historia nyingi ya TANU ipo katika mikono ya watu binafsi.

Iliffe alisema maneno haya katika miaka ya 1960 lakini kwa sasa ni wazi kuwa historia nyingi ya TANU si tu iko katika mikono ya watu binafsi bali iko pia katika masanduku na makabati yaliyoachwa na wazalendo wale waliopigania uhuru ambao takriban wote wameshatangulia mbele ya haki.

Historia hii ndani ya makabati na masanduku ya hawa wazalendo ni picha za "black and white" na nyaraka zilizoandikwa kwa mkono na type writer.

Siku chache zilizopita katika kutayarisha vipindi kwa ajili ya Nyerere Day nilitembelewa na waandishi na katika kuhitimisha mazungumzo yetu wakawa wanataka kujua majina ya wazalendo waliopigania uhuru wa Tanganyika lakini wamesahaulika.

Ndipo nilipolitaja jina la Abbax Max katika video ambayo tulikuwa tunarekodi.

Hii video fupi ipo hapo FB.

Mtoto wa Abbas Max, Ally Abbas Max baada ya kuiona hii video siku ya pili tu akanitumia picha ya baba yake na ''cuttings'' za gazeti kuhusu historia ya marehemu baba yake katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Ally Abbas Max kwa miaka mingi alikuwa Marekani na sikutegemea kama atakuwa na kumbukumbu za baba yake huko alikokwenda ughaibuni.

Ally amenitia moyo sana aliponiambia kuwa baba yake ameacha nyaraka na zimehifadhiwa hadi leo zaidi ya miaka 30 toka kufariki kwake, ni kiasi cha kuzifungua tu na bila shaka mengi yatajulikana jinsi yeye na wenzake walivyofungua tawi la kwanza la TANU Iringa mwaka wa 1955.

Naeleza hapa yale niliyoweza kupata kutoka kwa Ally Abbas Max nikichanganya kidogo na yangu.

Inawezekana watu wengi wasijue kuwa Chief Adam Sapi Mkwawa ni mtu wa kwanza kuingia TANU Iringa.

Chief Mkwawa aliwaalika Abdul Sykes na Dossa Aziz Kalenga katika sherehe ya kupokea fuvu la babu yake Chief Mkwawa kutoka Ujerumani.

Hili fuvu liliwasili Dar es Salaam tarehe 9 Julai 1954 siku mbili tu baada ya TANU kuasisiwa.

Katika mazungumzo ya faragha baina ya Chief Adam Sapi Mkwawa, Dossa Aziz na Abdul Sykes, Chief Adam Sapi akakata kadi ya TANU kwa siri.

Abbas Max amewaeleza watoto wake kuwa Abdul Sykes alikuja Iringa wakati tayari TANU ishapamba moto Dar es Salaam na alifikia nyumbani kwake.

Abdul Sykes alikuwa njiani anaelekea Njombe kumtembelea mume mwenzie.

Abbas Max akaamua kumpeleka Njombe na gari yake Peugeot Pickup 203.

Mazungumzo baina yao yalikuwa kuhusu TANU, Nyerere na juhudi za kudai uhuru.

Abbas Max akamwambia Abdul Sykes amwambie Nyerere aje Iringa ili wafungue tawi la TANU na wao wawemo ndani ya juhudi hizi za kupigania uhuru.

Haukupita muda Abdul Sykes akamtumia Abbas Max taarifa kuwa Nyerere atafika Iringa akitokea Lindi, Songea na Njombe.

Abbas Max alitoka na wazalendo wenzake kwenda kumpokea Julius Nyerere njiani nje ya mji wa Iringa.

Nyerere alikuwa ameongozana na Ally Mwinyi Tambwe na Rajab Diwani na dereva wa TANU Omari Simba.

Nyerere alimfahamisha Abbas Max kuwa ili kufungua tawi la TANU kwanza lazima awe na wanachama 12 wanye kadi za TANU.

Watu walikuwa wanaogopa kuingia chama na hiki kikawa kikwazo kikubwa kwa Abbas Max.

Nyerere aifanya mkutano wa hadhara Iringa lakini ulihudhuriwa na watu wachache.

Juu ya haya yote Abbas Max aliweza kupata watu waliokuwa tayari kujiunga na TANU na hawa walikuwa: Saleh Masasi ambae Nyerere alilala nyumbani kwake, Hussein Issa, Hussein Kandoro, Yasin Hamid, Ahmed Mahmoud, Abdulrahman Mwangili, Juma Lipinjime na Khalfani Ally, Abbas Max akiwa Mwenyekiti.

Katika mkutano wa Kura Tatu Tabora mwaka wa 1958 Abbas Max akachaguliwa kuwa mjumbe wa Halmashauru Kuu ya TANU hivyo ikabidi ajiuzulu uenyekiti.

Nafasi yake ikachukuliwa na Chogga.

Chogga ameacha historia ya pekee katika wanasiasa ndani ya TANU waliokuwa mwiba wa koo kwa Julius Nyerere.

Itapendeza sana kama wanahistoria wataandika historia hii yake kwani mwaka wa 1968 Chogga na wenzake walifukuzwa TANU.

Ikutoshe tu kuwa Abbas Max anasema kuwa Chogga alisababisha TANU ifungiwe iringa.

Hii ikapelekea Abbas Max na wenzake waendeshe harakati zao chinichini kupitia Jambo Club waliyoianzisha baada ya TANU kupigwa marufuku.

Safari ya pili Nyerere alipokwenda Iringa alifikia nyumbani kwa Abbas Max.

Abbas Max alitembea kote na Nyerere Nyanda za Kati Kusini katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Charles Mzena ambae wakati wa kupigania uhuru alikuwa Special Branch alipata kumwambia Salum Khamis wakati huo uhuru ushapatikana kuwa, ''Chief Adam Sapi Mkwawa alikuwa ndiyo chief wa Wahehe lakini Abbas Max wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika alikuwa na nafasi yake juu ya Chief Adam Sapi.''

Abbas Max alikuwa na kawaida katika misafara ile na Nyerere kuwa wakati wa kula yeye alikuwa akisubiri hadi dakika ya mwisho wakati chakula kimetengwa na wanaanza kula yeye atampora Nyerere sahani yake na kumpa ya kwake.

Nyakati zile zilikuwa ngumu na Nyerere alikuwa akiwindwa.

Abbas Max alikuwa akisema, ''Hakuna huku wa kunidhuru mimi.''

Historia ya Abbas Max katika kupigania uhuru wa Tanganyika ina mengi sana.

Mimi Inshaa Allah nasubiri siku wanae watakapofungua Nyaraka za baba yao Abbas Max na kuziweka hadharani zisomwe na wanahistoria.

Tunamuomba Allah awarehemu wazee wetu hawa waliopigania uhuru wa nchi yetu kwa hali na mali zao.

Amin.
 
Sasa nchi yote ikijaa majina ya wanasiasa itakuwaje? Acheni kupoteza identity ya maeneo ya wenyeji kwa mambo ya kipuuzi.

Jina linasaidia nini shirika? Apeleke udini wake kigoma.
 
Kuna wazee naona exposure walikuwa nayo kitambo

Ova
 
Kila kitu kiwe majina ya watu sio sawa mengine yabaki majina ya mahali au eneo kama ni hivyo basi na mafundi waliojenga hapo wawekewe majina Yao
Songwe liko poa sema zito katafuta namna ya kurudi kwenye media discussion
 
Anauliza Zitto Kabwe: Kwanini sio John Mwakangale International Airport?

View attachment 3085778

===

My Take
Naunga mkono hoja.Jina la Uwanja wa Ndege wa Songwe (Mbeya) libadilishwe sio tuu Kwa sababu za Kuenzi Mchango wa mzalendo huyo Bali pia kuondoa mkanganyiko wa kutumia jina la Mkoa tofauti na uwanja uliko.

Uwanja uko Mkoa wa Mbeya ila unatumia jina la Mkoa wa Songwe,hii ni zaidi ya kichekesho.
Kuna waziri alisema jina Kambarage liondolewe kwenye JKNIA (DSM) kwakuwa wazungu hawawezi kulitamka
 
Anauliza Zitto Kabwe: Kwanini sio John Mwakangale International Airport?

View attachment 3085778

===

My Take
Naunga mkono hoja.Jina la Uwanja wa Ndege wa Songwe (Mbeya) libadilishwe sio tuu Kwa sababu za Kuenzi Mchango wa mzalendo huyo Bali pia kuondoa mkanganyiko wa kutumia jina la Mkoa tofauti na uwanja uliko.

Uwanja uko Mkoa wa Mbeya ila unatumia jina la Mkoa wa Songwe,hii ni zaidi ya kichekesho.
Jina la Songwe Airport, linatokana na jina la sehemu uwanja huo ulipo! Uwanja huo upo kwenye kata iitwayo kata ya Songwe!! Kwahiyo usidhani kwamba linatokana na mkoa jirani wa Songwe!

Hiyo kata ipo tangu Rais wa kipindi hicho, hayati Benjamin Mkapa alipokuja kuzindua uwanja huo mwaka 2005.

Hivyo, jina Songwe, ni sahihi kabisa kuuita uwanja huo! Kuwa na amani mkuu!!
 
Ila linaleta mkanganyiko
 
Koo tajwa hapo Juu umewahi isikia popote ukiacha uwanja wa 8/8 Uyole Mbeya?
Kuna ulazima gani waandikwe je vizazi vingap vinafanya makubwa hapa nchini kila mmoja akililia kukumbukwa kama ukoo wenu mnaotaka huyo mnyakyusa wenu akumbukwe hizo project si zitajaa majina ya watu. NI UPUUZI KILA PROJECT KUANDIKWA MAJINA YA WATU
 
Havijawahi kuwa vizazi vingi,wanaofanya makubwa Huwa ni wachache
 
Back
Top Bottom