Hivyo unadhani Lisu akipigwa ban na mi ccm, Membe anaweza kuwa mbadala?!Suala la kujitoa nilishalifikiria lakini kwa sasa naona halitasaidia sana kwa sababu ile ile kwamba, kuna uwezekano mkubwa NEC wameshapa makaratasi, na hata kama zoezi halijakamilika, watasema tu wameshachapa ili mradi tu Membe asiondolewe kwenye karatasi za kupigia kura!
Lakini kwa upande mwingine, ma-CCM hayaaminiki haya kwahiyo inaweza kuwa risk kujitoa moja kwa moja!!! Nasema hayaaminiki kwa sababu Lissu akiyabana kisawasawa kiasi cha kukosa pumzi, wala hayaoni aibu haya kutumia kila hila kama ile ya kumsimamisha kufanya kampeni na hata kusema amekiuka hili na lile na hivyo anaondolewa!!
So, huku Membe kajitoa, TL anapigwa zengwe la kufa mtu... what next?! Kama ma-CCM yaliweza kufuta uchaguzi kule ZNZ baada ya kuona yamebanwa hata kupumua hayawezi unadhani yanaweza kushindwa kumpiga ban mgombea?!
Membe sidhani kama anaweza kumreplace Lisu, nakuhakikishia wakimpiga Lisu ban watu hawatapiga kura kabisa.